Kama wewe ni mwalimu soma hii

Mpendwa Msomaji, baada ya kukuandalia makala inayopendwa kuhusu; Mbinu za kumfanya mwanamke akukubali, sasa nimekuandalia makala hii kuhusu;

Kama wewe ni mwalimu soma hii.

Endelea kefurahia makala nzuri kila siku unapotembelea tovuti hii.

Kama wewe ni mwalimu soma hii

By, Melkisedeck Shine.

Kuna mwalimu wa shule ya sekondari alikuwa amezoea kumchapa viboko mwanafunzi mmoja mchelewaji. Mwanafunzi huyu alikuwa akichelewa kipindi cha kwanza kila siku. Hivyo, siku ambazo mwalimu huyu alikuwa na kipindi cha kwanza, mwanafunzi huyu alikuwa anachapwa kwanza kabla ya kuingia darasani. Hali hii iliendelea kwa muda mrefu. Wiki moja ilipita bila yule mwanafunzi kuonekana shuleni.

Wiki lililofuata yule mwanafunzi alifika shuleni kabla ya mwanafunzi mwingine yeyote. Mwalimu yule alipomwona alifurahi sana. Alipoingia darasani alimwita yule mwanafunzi na kumsifia sana mbele ya darasa.

"Rose, simama. Darasa, Mpigieni makofi "Rose" kwa sababu leo kawa wa kwanza kufika shuleni. Kumbe fimbo zile zimesaidia enhe"

Wanafunzi walipiga makofi huku wengine wakimcheka huyo "Rose" Yule mwanafunzi alimwomba mwalimu ampe nafasi aseme jambo. Mwalimu akamruhusu

"Mwalimu, siku zote nilizokuwa nikichelewa kufika shule nilikuwa namuuguza mama yangu. Baba yangu alifariki kabla sijazaliwa. Nimelelewa na mama yangu tu. Simjui ndugu yeyote. Mama yangu alipokumbwa na maradhi alipelekwa hospitalini lakini maradhi yake hayakuonekana. Akaruhusiwa kurudi nyumbani akiwa na dawa za kutuliza maumivu tu." Kwa sababu hatuna pesa, hakuweza kupelekwa popote kwa vipimo zaidi."

Rose alifuta machozi yaliyoanza kutiririka mashavuni. Mwalimu jicho nyanya. Rose akaendelea

"Hivyo, nilitakiwa kufanya usafi wa nyumba, kuchota maji, kumsafisha mama yangu, kumwandalia chakula chake kabla ya kuonda kuja shuleni na kazi zingine zote." Rose alinyamaza kidogo."

"Lakini leo nimewahi kwa sababu mama yangu alifariki wiki lililopita. Kwa hiyo kilichokuwa kinanichelewesha kimeondoka ndo maana leo nimewahi shuleni."

Rose hakuweza kuongea tena. Taratibu akakaa kitini huku akilia kwa kwikwi

Darasa zima liligeuka mahala pa msiba.

WITO: Walimu wasiwe wanapenda kuwapa wanafunzi adhabu bila kuwapa nafasi ya kujieleza sababu za kufanya makosa hayo. Wakati mwingine watoto hao huhitaji watu wa kuwasikiliza kwa sababu kwao hawasikilizwi. Ukionyesha upendo huwa inasaidia kuwabadili kitabia (mbaya kwenda nzuri)

Usisahau kushare makala hii uliyoisoma kuhusu; Kama wewe ni mwalimu soma hii. Share Facebook, Twitter bila kusahau WhatsApp.

Makala hii kuhusu, Kama wewe ni mwalimu soma hii, imeonekana kupendwa na wasomaji wengi. Makala nyingine zinazopendwa ni kama hizi zifuatazo;

β€’ Hadithi ya kusisimua, jifunze kitu hapa, endelea kusoma...

β€’ Haya ndio maisha ya ndoa, endelea kusoma...

β€’ Siri za mafanikio na Jinsi ya kufanikiwa, endelea kusoma...

β€’ SIRI YA HERUFI YA MWANZO YA JINA LAKO, endelea kusoma...

β€’ HADITHI: Maisha ya ndoa, endelea kusoma...

β€’ Hadithi ya kusisimua, endelea kusoma...

β€’ MAKUNDI MANNE YA WATU DUNIANI, endelea kusoma...

β€’ Hii chain ya mahusiano ni shida, endelea kusoma...

β€’ Ujumbe kwa wakina dada, endelea kusoma...

β€’ ZINGATIA HAYA, endelea kusoma...

Unaweza kusoma makala mpya nzuri kila unapotembelea website hii wakati wowote. Baada ya kusoma makala hii kuhusu; Kama wewe ni mwalimu soma hii, sasa endelea kusoma makala hizi nyingine nzuri nilizokuandalia;

A Unamkabidhi Moyo kibaka wa mapenzi unategemea nini!!, soma zaidi...
A KAMA ULIZALIWA BAADA YA MWAKA 90 HAYA AMAMBO YALIKUPITA, soma zaidi...
A UMETOKA KAZINI UMEKUTA PANYA 6 ndani, soma zaidi...
A Wosia mzuri kwako, soma zaidi...
A Wakubwa nisaidieni!!, soma zaidi...
A Ushauri kwa vijana wenye miaka 22 nakuendelea, soma zaidi...
A Jifunze kitu kupitia kisa hiki cha mume na mke, soma zaidi...

Usipitwe na Nafasi za kazi kwa leo

<<Bofya HAPA kujua zaidi>>

.