Vidokezo vya Hatari katika Mapenzi

Mpendwa Msomaji, baada ya kukuandalia makala inayopendwa kuhusu; Wanawake wavumilivu jamani, sasa nimekuandalia makala hii kuhusu;

Vidokezo vya Hatari katika Mapenzi.

Unaalikwa pia kusoma kuhusu; Ndoa nyingine ngumu sana. Soma kisa hiki.

Vidokezo vya Hatari katika Mapenzi

By, Melkisedeck Shine.

VIDOKEZO VYA HATARI KATIKA MAPENZI..!

UKIYAONA HAYA CHUKUA TAHADHARI MAPEMA.

(1). kama mpenzi wako anataka SEX.

Hiki ni kidokezo hatar kwa wasichana hapa wanapaswa kuwa makini.

Lakini pia jiangalie isije ni wewe ndio chanzo cha kufanya atake sex mapema hivyo. Kuwa makini na jinsi unavyojiweka, maongez unayoongea na hata mavaz unayovaa. Kama maziwa, mapaja yapo nje usishangae akiomba alale na wewe . Hapa wewe utakuwa ndio chanzo.

(2).Anapokuwa mzito kukutambulisha kwao.

Kama mpo kwenye uhusiano zaid ya mwaka mmoja, na hana hata dalili za kutaka kukupeleka kwao au ukimgusia kuhusu swala hilo kila siku anasema bado ni mapema, kuwa MAKINI. Kuna uwezekano mkubwa hakuna upendo hapo.USIPOTEZE MUDA WAKO.

(3).NI Msiri kujua mambo yake.

Kama si mwepesi kujieleza kwako mambo yake na hata ukimuuliza anajibu kwa ufupi tu,. Kama uhusiano ni mchanga, it's okay.. Lakin kama mna muda mrefu huyo mtu kwako atakuwa amejiegesha tu. KUWA MACHO.

Wengine hata kushika simu zao hawataki na kama ukijaribu kufanya hivyo wanakuwa wakali kama pilipili.

(4).Asiyejitoa kwako.

Mapenzi ni kujitoa, bila kujitoa hujapenda. Kujitoa si kwa pesa tu hata kwa muda wako kumpigia simu, kumjulia hali, kumtia moyo, kumfaraji n. k

Kama huyaoni haya kwa mpenzi wako au mpaka ulalamike na umlazimishe ndio afanye hayo, Tambua mapema hapo hamna upendo ni "KUMSUKUMA PUNDA MZIGO UFIKE .. "

(5).Anaomba Pesa mara kwa mara.

Kama kila wakat ni mtu wa kutangaza shida na pindi unapomuambia hauna kwa wakati huo, anachukia hata kupokea simu au kujibu text zako anasitisha. kuwa makini. Huyu ni mchimbaji mdogo wa madini na wewe ndiye mgodi wake.

Usipochukua tahadhar atachimba mpaka mchanga na kukuacha na umasikini wa kukutosha.

(6).Mkali na asiyekubali kushuka.

Hapa kuna shida, kuna watu wengine ni wakali na wana hasira za kupitiliza, jambo dogo linaweza likaleta ugomvi wa wiki nzima.

Wapo wengine pia wao kusema 'samahan nimekosea ni kama teja /mwizi na kituo cha polisi' hawezi kukubali hata kama kosa ni lake tena lipo wazi kabisa.

Watu wa namna hii, hawatakupa furaha kwenye maisha yako. Ila kama ukiweza KUCHUKULIANA nae sawa, hapo ni wewe maana kila mtu ana Kifua chake.

(7).Kuomba msamaha kila wakati.

Yule asiyeomba msamaha na huyu anayeomba msamaha kila mara wote ni sawa tu. Kuna watu wengine wao kusema samahan sio shida ila tatizo Lao hawajirekebishi katika yale wanayokosea, leo amekosea hili kaomba msamaha haijapita wiki karudia tena yaan ni kawaida yake.

Hili nalo ni tatizo, wapo walio na udhaifu katika mambo fulani na wanashindwa kujirekebisha kwa haraka, lakini pia wapo ambao wanacheza tu na AKILI yako huku wakiwa wanafahamu kile wanachofanya. KAZI KWAKO KUJUA YUPO KUNDI GANI KATI YA HAYA.

(8).Complainer /mlalamishi.

Kuna watu hawana dogo wao ni kulalamika mpaka mtu unakosa amani. Kila kitu wao ni kulalamika.

"Mapenzi ni maelewano na palipo na maelewano ndipo palipo Amani "

(9).Mwenye mahusiano ya karibu na wapenzi wake wa zamani.

Aise, hapa kuwa napo makini. Mapenzi si uadui na watu wanapoachana si vibaya kama wakiendelea kuwasiliana lakin lazima kuwe na kiasi na mipaka.

Haiwezakani kila muda wanachat, simu hazikatiki mpaka sa 6 usiku, ukimuuliza anasema ni rafiki tu kwa sasa hamna kitu kibaya. Hapa kuna tatizo. Mipaka na heshima lazima iwepo. Itifaki izingatiwe.

(10).Msaliti.

Kama ana tabia za usaliti wa mara kwa mara. Huyo si mtu sahihi kwako, ni bora UMUACHE AENDE na ubaki na Amani yako.

Usisite kuvunja uhusiano na mtu kama huyo.

"Ni heri kuvunja uchumba kuliko kuvunja ndoa"

,**

Hakuna aliyekamilika, lakini wengi leo hii wapo kwenye MAJUTO na VILIO visivyoisha kwa kushindwa kuchukua TAHADHARI mapema.

Mambo hayo tuliyoyaona ni kama INDICATOR, TAA NYEKUNDE inayotoa tahadhar kuwa kuna kitu Cha HATARI mbele yako. So, UAMUZI NI WAKO KUSIMAMA AU KUENDELEA NA SAFARI.

THINK CAREFULLY & ACT WISELY.
"Marriage is your destiny "

YESU AKUSAIDIE UMPATE YULE ALIYE WAKO.

MITHALI 19 :14

Mwl John Charles Ntogwisangu - 0712463344 /0765166702.

Usisahau kushare makala hii uliyoisoma kuhusu; Vidokezo vya Hatari katika Mapenzi. Share Facebook, Twitter bila kusahau WhatsApp.

Makala hii kuhusu, Vidokezo vya Hatari katika Mapenzi, imeonekana kupendwa na wasomaji wengi. Makala nyingine zinazopendwa ni kama hizi zifuatazo;

β€’ Ujumbe kwa Mke Mtarajiwa, endelea kusoma...

β€’ Unaweza kushare maneno haya kuntu kwa vijana wote ambao hawajaoa na walio kwenye ndoa, endelea kusoma...

β€’ Ujumbe kwa wadada, endelea kusoma...

β€’ Unaweza kushare maneno haya kuntu kwa vijana wote ambao hawajaoa na walio kwenye ndoa, endelea kusoma...

β€’ Wosia mzuri kwako, endelea kusoma...

β€’ Soma Hii itakusaidia sana, endelea kusoma...

β€’ Mapenzi kweli hisia!, endelea kusoma...

β€’ Unajifunza nini hapa?, endelea kusoma...

β€’ Kila mtu dunia hii anahistoria yake, endelea kusoma...

β€’ Tahadhari, endelea kusoma...

Unaweza kusoma makala mpya nzuri kila unapotembelea website hii wakati wowote. Baada ya kusoma makala hii kuhusu; Vidokezo vya Hatari katika Mapenzi, sasa endelea kusoma makala hizi nyingine nzuri nilizokuandalia;

FURSA.PNG

Fursa Ya Kazi Na Ajira Yenye Malipo Mazuri

Au soma zaidi hapa

.