.

Kichekesho%20Kipya Usipitwe na Kampeni hii Ni kampeni endelevu ya kuhamasisha ushirikiano, umoja na kusaidiana katika jamii kwa watu wa matabaka yote
πŸ‘‰SOMA ZAIDI HAPA...Kizuri

πŸ‘‰ Soma Hii itakusaidia sanaπŸ‘‡βœ”

IMG_20180125_211540.jpg

Imehaririwa na; Melkisedeck Leon Shine. Tarehe 07 Sep 2016 05:54. [Legal & Authority]


Soma Hii itakusaidia sana

UKIPATA MUDA SOMA ITASAIDIA SANA

Mimi ni mwanamke wa miaka 27, nilikuwa katika mahusiano mabaya yasiyo na tija kwa kipindi cha miaka minne.

Nilipokutana na huyo mwanaume nilifikiri yeye ndie fungu langu, maneno yake matamu na mbwembwe nyingi viliniamninisha kwamba kweli ananipenda na kusema kweli niliingia katika mtego wake.

Nilifanya kila jambo ambalo mwanamke apaswa kumfanyia mwanaume wake, nilijaribu kumuaminisha kwamba nampenda kweli, nilijitoa sadaka maisha yangu kwa ajili yake lakini alikuwa kipofu kuyaona yale niliyokua nikimfanyia.

Alichojua kukizungumza vizuri ni kuwasifia tu wanawake wengine au wanawake wa marafiki zake na kunieleza jinsi gani walivyo wazuri, mitindo gani ya nywele inayompa wazimu na alikuwa akinilaumu kwa kila jambo kwamba mimi namletea kiwingu.

Nikaanza kutojiamini na kujidharau, nikajiona sina thamani tena na sina mvuto kwa sababu alikuwa akiniambia hakuna mwanaume atakaenipenda mimi. Na kuwa nina bahati ya kuwa na handsome kama yeye anayegombaniwa na wanawake wengi.

Siku moja alifanya kosa kwa kuniita mimi nimechanganyikiwa na kwamba mimi sio type yake na hawezi kunioa, niliumia mno siku ile, nilikuwa chuo wakati huo nikikaribia kufanya mtihani wa mwisho kabisa kumaliza chuo.

Sikuweza kusoma, nilichanganyikiwa sana na nililokua nafikiria ni kujitoa uhai tu, nilichukia kila kitu na nikajichukia na mimi mwenyewe. Aisee nilimpenda yule mwanaume.

Ila nashukuru Mungu aliingilia kati, nilikua room kwangu, baada ya kulia sana na kuomboleza juu ya mateso ya kihisia ninayoyapata ikiwemo na kudharauliwa, nilisimama mbele ya kioo na nikatizama mwanamke mzuri aliesimama mbele ya kioo.

Nikajipa matumaini, nikajivuta na kujikusanya, nikafumba macho yangu kwa dakika kumi nikapumua kwa nguvu. Nikajiambia 'i will get it over.' nikaanza kujisomea kwa ajili ya kujiandaa na mitihani.

Nilisoma, nikafanya mitihani salama na nikahitimu chuo kikuu. Baada ya kumaliza chuo kikuu nilikaa kama miezi mitatu nikapata kazi katika kampuni fulani ya mafuta hapa mjini nikiwa katika idara ya rasimali watu.

Sikutaka kupenda tena, nilijikita katika kazi yangu ambayo kimsingi niliipenda sana, wafanyakazi wenzangu wote walinipenda kwa jinsi nilivyokua mcheshi na mkurugenzi alifurahi sana maana nilikua nikifanya kazi kwa bidii zote.

Baada ya kama mwaka mmoja nilikutana na mwanaume, ambae hakutaka hata kusubiri muda mrefu akajitambulisha kwa wazaz wangu, akanitambulisha kwako na akanivisha pete ya uchumba.

Tulifunga ndoa baada ya miezi sita, na sasa nimeolewa na mwanaume anaenipenda mpaka najishtukia. Sijui mwanaume huyu alilelelewa na mama wa aina gani, mara kwa mara hua nampigia simu mama yake na kumshukuru kwa kumleta duniani huyu mwanaume alienifanya nijisikie mwanamke imara!

Kwa sasa nimefanikiwa mambo mengi ambayo kimsingi nadhani nisingefanikiwa kama ningeendelea kumng'ang'ania yule

Baada ya kupotezana kwa muda mrefu Alinitafuta siku moja facebook, na kuniomba tuonane ana jambo anataka kuniambia. Nilionana nae katika mgahawa fulani uliopo mjini, nilimuona akiwa amechoka hana hili wala lile, akaniambia hana kazi baada ya kugundulika alifanya ubadhirifu wa pesa ya mradi (alikuwa ni mtu wa starehe sana, pombe na wanawake, asifahamu kwamba pombe na wanawake hupotosha wanaume wenye akili).

Hakuamini kuniona nikiwa na pete ya ndoa, ninaendesha gari zuri na ninafuraha, alidhani nitakua nimechoka kama yeye. Aliniomba msamaha me nikamwambia nimeshamsamehe tokea kitambo aendelee tu na maisha yake.

Nikaja gundua kwamba haikuwa hasara kwangu kwa yeye kuniacha, bali alipata hasara kubwa yeye kuniacha mtu niliyempenda kweli na niliekuwa na ndoto za kumsaidia afanikiwe katika maisha.

Maisha ndivyo yalivyo, safari ya mapenzi hua na mabonde na milima, kuna nyakati utafurahia na nyakati utapata uchungu na kujuta kwanini ulipenda, ila katika hali unayopitia tambua kua kuna makusudi iliyo wazi ya kukuwezesha kuwa na nguvu na ujasiri.

Sasa nakuombea wewe ambae unasoma ujumbe huu leo, Mwenyezi Mungu akakuongoze na kukufariji katika magumu unayopitia, yule ambae amekuacha na amekudharau atakuja kukupigia magoti pale ambapo baraka zako zitakapong'ara.

Tabia ya kua na mahusiano na mtu zaid ya mmoja alafu unawafanyia COMPARISON sio VIZURI hata Mungu hapendi, CHAGUA mmoja wengine waambie UKWELI USIMPOTEZEE MUDA(Nguki et al 2016). Fanya kitu ambacho hata wewe ungependa kufanyiwa. Ucku mwema nyote

πŸ™‰πŸ™‰πŸ™‰Usisahau kushare posti hii kuhusu (Soma Hii itakusaidia sana).πŸ‘ Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasomeπŸ’―βœ”

Nini maoni yako kuhusu, Soma Hii itakusaidia sana? Niandikie hapa
Add a New Comment
or Sign in as Wikidot user
(will not be published)
- +
Kichekesho%20Kipya Usipitwe na Kampeni hii Ni kampeni endelevu ya kuhamasisha ushirikiano, umoja na kusaidiana katika jamii kwa watu wa matabaka yote
πŸ‘‰SOMA ZAIDI HAPA...Kizuri

SOKOINE-UNIVERCITY-OF-AGRICULTURE.jpg

Ujumbe wangu kwako kwa sasa

"Blog hii ni miongoni mwa Blog nzuri ya Kiswahili. Kupitia Blog hii utaweza kujifunza mambo mengi mapya mazuri. Ni wewe tuu kutembelea Blog hii mara kwa mara."

utotoni.gif

.

.

b.gif

Mimi ni Melkisedeck Shine Mmiliki, Mwandishi /Mhariri. Karibu tena kila siku.

MAWASILIANO | KUHUSU MWANDISHI

Blog nyingine maarufu ndani ya AckySHINE.com

| Vichekesho | Videos | Picha | Ujasiriamali | Mahusiano | Kilimo & Mifugo | Katoliki | Afya & Mapishi | Hadithi | Misemo | SMS