Sifa 15 za kijana ambaye hajakomaa kwa ajili ya ndoa

Mpendwa Msomaji, baada ya kukuandalia makala inayopendwa kuhusu; Soma hii! Mchagua nazi......, sasa nimekuandalia makala hii kuhusu;

Sifa 15 za kijana ambaye hajakomaa kwa ajili ya ndoa.

Endelea kefurahia makala nzuri kila siku unapotembelea tovuti hii.

Sifa 15 za kijana ambaye hajakomaa kwa ajili ya ndoa

By, Melkisedeck Shine.

SIFA 15 ZA KIJANA AMBAYE HAJAKOMAA KWA AJILI YA NDOA
♨♨♨♨♨♨

1. Anaigiza maisha. Anataka kuonekana amefanikiwa kimaisha, hajui kuwa anajidanganya mwenyewe.

2. Hana mipango inayoeleweka, anajua kuzungumza lakini matendo ni sifuri, hajui kwamba kuanza mahusiano ni kubeba majukum.

3. Anataka ngono kabla ya ndoa, akipewa anasema binti hana hofu ya Mungu, asipopewa anatishia kuvunja mahusiano au anaanzisha mahusiano na msichana mwingine.

4. Ana wivu unaowaka kama moto wa nyika, anaweza kumkataza mchumba wake asiongee na mwanaume mwingine, au asifanye kazi kwa sababu boss wake anamtaka au kwa sababu anahisi kazi ile amepewa na 'mwanaume' .

5. Ana hasira mithili ya mbogo aliyechokozwa, anaweza kumpiga mpenzi wake au kumtukana. Ni katili, mdhalilishaji na anapenda kusikilizwa kwa kila amri atoayo.

6. Hajui lolote kuhusu Mungu, na hana muda wa kutafakari habari za Mungu.

7. Ni Tegemezi, anategemea wazazi au kupiga 'mizinga' kwa ndugu na marafiki ili kumudu mahitaji yake ya kila siku.

8. Si mtoaji kwa sababu hana kitu cha kutoa, ukimweleza shida yako hashindwi kukwambia we unapenda pesa, au anaweza kusema, 'Mi sio babako'

9. Anapowaza kuhusu ndoa anawaza ngono tu, hafikirii kuhusu majukumu ya kulea familia na mipango ya maendeleo ya familia.

10. Hajui kusifia, anachojua ni kukosoa tu. Anataka kupewa sifa zote hata ambazo hastahili.

11. Hujiona bora kuliko wengine na mara nyingi anapenda kushindana na watu bila sababu.

12. Anapenda maisha ya maonesho (show off) : anaweza kupiga picha kwenye gari ya rafiki yake akaandika status, my new ride, anaweza kutamani hata kuombea mkopo; akipanda ndege basi hawezi kuwa na story nyingine zaidi ya safari ya angani. Akipata fursa ya kupiga picha na mtu maarufu basi anadhani na yeye ni maarufu na anadhani mafanikio ya mtu yule yamehamia kwake.

13. Mvivu, hawazi juu ya kesho yake. Anaanza mradi na kuishia mwanzoni (sio njiani) kwa sababu lengo ni kuwanasa wanawake wapumbavu.

14. Anashinda online anachat, na anajua wazi hakuna biashara anayofanya mtandaoni. Mitandao ya kijamii imeteka maisha yake, haongezi tija wala maarifa ya msingi kwa maisha yake.

15. Anazijua sifa zote za wife material lakini hana sifa hata moja kuwa husband material.

#AMKA KIJANA JITAMBUE#

Usisahau kushare makala hii uliyoisoma kuhusu; Sifa 15 za kijana ambaye hajakomaa kwa ajili ya ndoa. Share Facebook, Twitter bila kusahau WhatsApp.

Makala hii kuhusu, Sifa 15 za kijana ambaye hajakomaa kwa ajili ya ndoa, imeonekana kupendwa na wasomaji wengi. Makala nyingine zinazopendwa ni kama hizi zifuatazo;

β€’ KAMA ULIZALIWA BAADA YA MWAKA 90 HAYA AMAMBO YALIKUPITA, endelea kusoma...

β€’ FAHAMU NGUVU ZAKO ZA KUZALIWA, endelea kusoma...

β€’ Salamu za kiinjilisti kwa wadada, endelea kusoma...

β€’ Tabia ambazo zinamfanya mwanamke asiolewe, endelea kusoma...

β€’ Kinachoimarisha uwezo na ujuzi wa mtoto, endelea kusoma...

β€’ Soma hapa wewe kijana wa kiume, endelea kusoma...

β€’ Sera ya mapenzi kwa vipindi tofauti tofauti, endelea kusoma...

β€’ Mambo ya kuzingatia kabla ya kuingia kwenye ndoa, endelea kusoma...

β€’ Sababu ya Wasichana wengi kutoolewa ni hizi, endelea kusoma...

β€’ UMETOKA KAZINI UMEKUTA PANYA 6 ndani, endelea kusoma...

Unaweza kusoma makala mpya nzuri kila unapotembelea website hii wakati wowote. Baada ya kusoma makala hii kuhusu; Sifa 15 za kijana ambaye hajakomaa kwa ajili ya ndoa, sasa endelea kusoma makala hizi nyingine nzuri nilizokuandalia;

A Biblia inasema nini kuhusu mume mwema, soma zaidi...
A Angalia binadamu walivyo, soma zaidi...
A Ujumbe wa leo kwa mtu anayetaka kufanikiwa katika maisha kiuchumi, soma zaidi...
A Wakubwa tuu wataelewa!!!, soma zaidi...
A Neno la kutia Moyo, soma zaidi...
A Ushauri kwa vijana wenye miaka 22 nakuendelea, soma zaidi...
A Jifunze kitu kupitia kisa hiki cha mume na mke, soma zaidi...

FURSA..! Kuna nafasi za kazi 100.

Au soma zaidi hapa

.