Maneno makuu ya kimapenzi yenye thamani kwa mwanamke

By, Melkisedeck Shine.

elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

Maneno makuu ya kimapenzi yenye thamani kwa mwanamke

KATIKA uhusiano wa kimapenzi yapo maneno mawili yenye thamani kubwa na yenye kubeba ujumbe mzito wa kimapenzi kwa mpenzi umpendaye kwa dhati, maneno hayo ni, 'nakupenda' na 'nitakuoa'.

Maneno haya mawili kwa wenye kujua thamani yake si rahisi kuyatamka ovyovyo kwa yeyote yule asiye na mpango naye wa kumpenda wala kumuoa.

Kutamka maneno hayo kwa hitaji la kumlaghai mpenzi ama mchepuko katika kumpata kimapenzi ni uhuni na tena ni dhambi kubwa.

Cha kushangaza mara nyingi tumekuwa tukishuhudia ama kuona wapenzi wengi wakisimulia au kuelezea kwa namna alivyoweza kulaghaiwa na kuumizwa moyo na mtu aliyedhani kuwa kweli angeweza kumpenda kutoka moyoni mwake na kumuoa.

Utaona huyo akisimulia kwa namna alivyoweza kukutana kwa mara ya kwanza na mchepuko huyo aidha kwa njia ya kuonana naye ana kwa ana, kwa njia za mitandao ya kijamii ama kwa njia ya mawasiliano ya simu.

Kuonana huko ndiko kulikomsababisha apagawe, achanganyikiwe, alainike na kuingia mtegoni kwa maneno matamu aliyoyasikia masikioni mwake. Masikini! kumbe ni uongo mtupu, huku kwa upande wake akiambulia kujiuliza kama anapendwa kweli.

Bila shaka kwa mwenye kulitaka lake jibu huwa ni rahisi sana, nakupenda. Wapo pia wale wanaotanguliza neno hilo pasipo hata kuulizwa.

Hiyo yote ni katika kujaribu kuuteka moyo wa yule anayemtamani kimapenzi ili aweze kumuaminisha kuwa napendwa lakini pia kupata uhakika wa uwezekano wa kuoa au kuolewa.

Ni katika hali ya namna hiyo, wengi wamekuwa wakidanganywa na kuachwa solemba. Lakini kama wangeweza kujua kuwa, suala la kupenda, kuoa au kuolewa lina thamani ya pekee katika maisha ya watu wenye mapenzi ya dhati asingeweza kutamka maneno hayo kwa asiyempenda.

Kwa jinsi hiyo, kwa anayejua maana na umuhimu wa maneno hayo si rahisi mara moja kukubaliana na mpenzi wa aina hiyo.

Kichekesho%20Kipya Usikose 📕Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE👧👗👠 Tsh 2,500/= tuu! Kinamwelezea🔎Mwanamke🔍 kinagaubaga✔
👉Bofya hapa KuchukuaKizuri

Lakini pia kwa mwenye mapenzi ya kulaghai na asiyependa kutamka maneno hayo badala yake utaona akitafuta namna au mbinu nyingine ya kumnasa mchepuko huyo.

Aina ya maneno atakayotumia kama hatakuwa makini katika kuujua ukweli ama uongo wake, yanaweza kukuteka kisaikolojia na pia kukusababisha uweze kweli kuamini maneno hayo.

Kwa mfano, mpenzi anaweza kukutamkia kuwa, "usiwe na wasiwasi kuhusu hilo, ni vizuri kwanza tujuane, halafau wewe mwenyewe upime kama kweli nakupenda au la.

“Halafu kuhusu suala la mimi na wewe kuoana hilo ni matokeo ya hatua kwa hatua. Kwa maana nyingine si jambo la kukurupuka. Sitaki uone kama nakudanganya, nataka uniamini kuwa mimi ni mkweli na hata nitakapokutamkia nakupenda uone kweli imetoka moyoni mwangu"

Aina ya uongeaji wa namna hiyo ni katika kumpoteza mpenzi ama mchepuko kwa lengo la kumpata kimapenzi.

Mpenzi huyo atakapoingiwa na tamaa kwa kuamini maneno hayo kwa haraka pasipo kuchukua muda mrefu wa kuyatathmini na kuyafanyia kazi maneno hayo ni rahisi kuingia kichwa kichwa kulaghaiwa kiulaini na baadaye kuumizwa moyo wake.

Pia kumbuka kwamba, anapotamkiwa mchepuko maneno ya aina hiyo, iwe kwa njia ya kuonana ana kwa ana, kwa njia ya mitandao ya kijamii au kwa njia ya simu kwamba, 'nakupenda sana' na pia ikibidi kwa kuongeza kutoa ahadi ya kumuoa huku akijua fika hana nia naye, ni kumsaliti mpenzi, mchumba, mke ama mume wako.

Aidha, utumiaji wa maneno 'nakupenda na nitakuoa' bila kujali thamani ya maneno hayo ni kumuumiza mpenzi au mchepuko huyo moyo wake.

Pia kumsababisha aumie kisaikolojia, kutafuta njia ya kujiua kwa sababu tu ya kushindwa kuamini kwa kile kilichotokea baada ya kusikia kuwa maneno uliyomtamkia ni katika kuhitaji kumpata kimapenzi.

Kwa jinsi nyingine, utumiaji wa maneno hayo yanaweza kukusababisha yakushushie thamani ya mapenzi baina yako na yule unayependa kwa dhati.

Wakati mwingine utumiaji wa maneno hayo hayo yanaweza kumsababisha yule uliye na lengo naye la kumlaghai kimapenzi akuroge, aidha kwa nia njema ya kukupata kimapenzi baada ya wewe kumuongopea ama kukuroga kwa nia mbaya ya kukuumiza na wewe moyo wako.

Wakati mwingine kabla ya kutamka maneno hayo, ni vyema mpenzi akajiuliza mara mbili mbili kwa kile anachotaka kufanya kwa yule aliye na lengo naye la kumdanganya.

Kichekesho%20Kipya Usikose 📕Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE👧👗👠 Tsh 2,500/= tuu! Kinamwelezea🔎Mwanamke🔍 kinagaubaga✔
👉Bofya hapa KuchukuaKizuri

Ajiulize kwamba, je, ni sahihi kumwambia mtu mwingine tofauti na uliyemchagua moyoni mwako, ukampenda kwa dhati yako na pengine hata kumchumbia na kufunga naye ndoa kuwa unampenda na utamuoa mtu mwingine tofauti na yeye?

Hebu ukiwa kama mpenzi na una mchumba, mume ama mke jaribu kubadilika tabia yako kwa kutunza heshima ya penzi la mwenzi wako, ikiwa kama yeye ana kuheshimu na kukutunzia mapenzi yenu, kuwa na hofu ya Mungu ndani yako.

Lakini pia kuwa mkweli kwa maneno unayotamka. Usifanye jambo au kutamka maneno matamu kwa hitaji la kumridhisha kumpata unayemtaka kimapenzi.

Usitumie maneno nakupenda kwa usiyempenda, na wala usimuahidi kuwa utamuoa, haipendezi.

Chanzo www.raiatanzania.co.tz/maneno-muhimu-yenye-thamani-kubwa-mapenzi/


Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Maneno makuu ya kimapenzi yenye thamani kwa mwanamke;

a.gif Mambo muhimu ya kufanya kwa mpenzi wako msichana ili asikuache

1. Hakikisha unakuwa msafi kwa kila kitu hasa unapo kuwa naye.
2. hakikisha unampa uhuru wa kutosha mnapo kuwa mnafanya mapenzi namaanisha awe na maamzi juu ya mwili wake usimrazimishe kama hayuko tiari, umuandae kabula ya kutumbukiza dushelele yako, uhakikishe anafika kileleni kila unapofanya naye mapenzi.. endelea kusoma

a.gif Ushauri wa mapenzi

Kuachwa kusikupe Stress, Haijalishi umeachwa mara ngapi, Jali kile ulichojifunza kutoka kwa mtu aliyekuacha… endelea kusoma

a.gif Kutoa Mimba

Mama mmoja huku akiwa anawasiwasi alienda kwa daktari wa magonjwa ya akina mama na akamwambia
" mwanangu hajafikisha hata mwaka mmoja na mimi nimepata ujauzito tena"
Daktari akamwambia
"ni sawa, kwa hiyo unataka mimi nifanyeje?"
Mama akasema
"nakuomba unisaidie kutoa hii mimba na ninakutegemea mno daktari tafadhali nisaidie"
Daktari baada ya ukimya mfupi na kufikiri kidogo akamwambia yule mama
" Nadhani ninao msaada mzuri zaidi na ambao hautakuathiri kwa kwa namna yoyote kiafya".. endelea kusoma

a.gif Ukipenda Boga, penda na ua lake

mwanaume akiwa ana hema ametoka kazini
kabla ya muda wa kawaida,akamwambia mke
wake Jiandae haraka tuna safiri kwenda
mbeya,mke akamuuliza kuna nini??.. endelea kusoma

a.gif Kila mtu dunia hii anahistoria yake

Kijana wa miaka 24 alikua anaangalia ktk dirisha la treni, mara akahamaki akasema….. endelea kusoma

a.gif Hadithi ya kusisimua, jifunze kitu hapa

By Malisa GJ,
Alikuwepo mama mmoja aliyekuwa chongo na mwanae alimchukia kwa sababu ya kuwa chongo. Mwanae alijisikia aibu kutembea na mama yake mwenye jicho moja na hakupenda watu wajue kuwa yule ni mama yake… endelea kusoma

a.gif Kutangaza Vituo Vya Misaada Kwa Jamii

Kwenye Tovuti ya AckySHINE tunawakutanisha watu wanaotoa misaada mbalimbali kwa jamii hasa yatima, walemavu wasiojiweza na wazee, pamoja na Vituo vya kutolea Misaada.
Tunatoa nafasi kwa vituo vya kutoa msaada kwa jamii kutoa matangazo yao bure kwenye tovuti hii. Hatukusanyi michango yoyote bali tunatangaza vituo vya misaada… endelea kusoma

a.gif Ungekua wewe ndo huyo mama ungefanyaje??

Mke wa Frank anajivunia mume mtulivu, hashindi baa na hatongozi videmu. Akitoka kazini huenda kucheza basketball na hurudi nyakati za dinner. Siku moja mkewe akamhurumia. Anachoka na kazi. Mtu gani asiyependa starehe japo kidogo? Mke akamlazimisha outing, Frank akabisha lakini taxi ikafika. Gonga Club & Lodge… endelea kusoma

elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

.

uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png
uliyesoma.gif
uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.