Mahaba kwa wanawake wa siku hizi

By, Melkisedeck Shine.

Wanawake wengi siku hizi hawajui au hawataki kuonesha mahaba
Nimefanya kautafiti kangu kadogo nimegundua wanawake wengi siku hizi hawaonyeshi mahaba yani kwa ujumla hawako "Romantic". Wanawake wengi siku hizi akipata mwanaume anaona amepata mtu wa kumsaidia shida zake kwa hiyo hata akiwa ndani ya mahusiano anafikiria zaidi kutatuliwa shida zake kuliko mahusiano yenyewe.

💞
Wanawake wa siku hizi wengi, kwa mfano umemtoa out kidogo mkapate walau msosi sehemu nzuri, mkianza kula mpaka mnamaliza hakumbuki hata kukulisha kidogo kimahaba. Unakuta anakula msosi kimpango wake utafikiri anakula na kaka yake. Mnatoka kidogo mnatembea unakuta anatembea na wewe utafikiri anatembea na kaka yake; yani unaweza ukamuacha nyuma kidogo au akawa mbele yako anashindwa kujiongeza kupitisha mkono wake kwenye kikwapa chako na kukushika kimahaba.
💞
Wakati mwingine anakuona jasho linakutoka usoni anashindwa hata kukufuta kimahaba anakutazama tu utafikiri wewe ni kinyago cha mpapure. Wakati anakuaga anaondoka utafikiri anamuaga kaka yake hakupigi hata busu. Mwanamke unazungumza nae hakushiki hata ndevu zako kimahaba, mwanamke unakuwa nae hakufunyii massage wala hakukati mara moja moja kucha zako kimahaba.
💞
Wakati mwingine unakuta umekaa nae mwaka mzima kwenye mahusiano lakini hajawahi kukwambia neno "Nakupenda"mpaka wewe uanze kumwambia kwanza.
💞
Wanawake wengi wa siku hizi wanapenda kudekezwa, kubembelezwa na kupewa pesa ndio maana wengi utasikia wakisema "nataka mwanaume Romantic na mwenye pesa" lakini hawajiulizi je, wao ni Romantic? Au sisi wanaume hatuhitaji hayo mahaba ya wanawake?
💞
Asili ya mwanamke ni mfariji mkuu wa mwanaume lakini siku hizi wanawake wengi wamekuwa stress kwa wanaume.
💞
Note: Hakuna mwanaume mbahili kwa mwanamke Romantic.SALAMU-USIKU-23ND.JPG

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Mahaba kwa wanawake wa siku hizi;

a.gif Mchumba anayefaa kufunga naye ndoa

Maisha ya ndoa yanahitaji maandalizi mazuri, kama waswahili wasemavyo nyote njema huonekana asubuhi, asubuhi ya maisha ya ndoa ni kipindi cha uchumba. Ndugu zangu, kipindi cha uchumba ni lazima tukitumie vizuri na kwa makini na kila jambo, ukitambua hakuna jambo dogo wa kubwa, kila jambo uliangalie katika mapana yake na katika uzito wake… endelea kusoma

a.gif Njia za kuamsha hamu ya kufanya mpenzi ya mwanamke

Andaa mazingira ya kuamsha hisia zake, fanya kitu kitakachowasogeza karibu na kuamsha hisia zake Kwenye akili yake kabla ya kugusa mwili. Mfano, weka mziki au muvi nzuri n.k. Kisha tengeneza mazingira ya kuwa karibu kimwili na kugusana… endelea kusoma

a.gif Ushauri wa ukweli Ili Uwe mwanaume wa Ukweli

1. Ukija kijiweni au pub au kwenye nyama choma acha zile stori za sijui umesoma wapi hadi wapi, sijui una madigirii mangapi. Piga stori nyingine, mbona ziko nyingi tu. Kujielezea sana shule yako ni ushamba fulani hivi, dizaini kama hujiamini so lazima ujivishe nyota. Unaboa… endelea kusoma

a.gif Mambo ya Msingi kuyajua Ili uishi na watu vizuri

Nimezipenda hizi nasaha. Naamini na nyinyi wenzangu hamtakosa japo machache ya kujifunza:-
1. Epuka hasira za ovyo na kila mtu, kuwa msikivu kabla ya kukimbilia maamuzi (elewa kuwa ukiwa na hasira huwezi kupata suluhu ya jambo)
2. Usiwatendee wengine ubaya ukadhani kuwa utakuwa salama (ubaya hulipwa kwa ubaya, ipo siku ubaya wako kwa wengine utakurejea kama sio kuwarejea watu wa kizazi chako).. endelea kusoma

KADI-POLE-MZAZI.JPG

a.gif MAANA YA MAPENZI

Mapenzi Ni Hisia Kali Za Upendo Ambazo Humfanya Mtu Kujisikia Furaha Na Amani Ktk Moyo Wake. Vilevile Mapenzi Yapo Ktk Matabaka Mawili, Tabaka La Kwanza Ni Mapenzi Ya Yanayohusisha Jinsia Mbili Tofauti Au Moja Kwa Dhamira Ya Kuridhishana Kingono. Tabaka La Pili Ni Mapenzi Yanayohusisha Jinsia Mbili Tofauti Au Jinsia Moja Kwa Dhamira Ya Urafiki Na Sio Kingono… endelea kusoma

a.gif Kisa cha kusisimua cha kijana na mke wake na mama yake

Kuna kijana mmoja daktari alikwenda kuposa. Binti aliyemposa akamuwekea masharti mazito. Akamwambia chagua mawili imma kunioa mimi au kukaa na mama yako, kwa sababu ukinioa mimi sitokubali mama yako aje hata harusini kwangu! Yule kijana aliemewa. Hakujua la kufanya. Mke anamtaka, lakini mama yake pia anampenda… endelea kusoma

a.gif Sababu 5 zinazosababisha wanawake warembo wazuri wasiolewe

Wanawake wengi warembo husalia peke yao na kufa katika hali hiyo kutokana na sababu tofauti… endelea kusoma

a.gif Soma hii! Mchagua nazi……

Hakuna mtu aliye mkamilifu kwa asilimia 100. (mfano).. endelea kusoma

[Msemo wa Leo] 👉Siri ya kushinda hasira

[Jarida la Bure] 👉Jarida la kilimo bora cha matikiti

Usipitwe na Nafasi za kazi kwa leo

<<Bofya HAPA kujua zaidi>>

.

SALAMU-ASUBUHI-987HGZ.JPG
kj.gif

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.