KUHUSU WANAWAKE

Mpendwa Msomaji, baada ya kukuandalia makala inayopendwa kuhusu; Kila mtu dunia hii anahistoria yake, sasa nimekuandalia makala hii kuhusu;

KUHUSU WANAWAKE.

Unaalikwa pia kusoma kuhusu; HADITHI YA MFALME ALIYEKUWA NA MBWA WAKALI KUMI.

USIKOSE HIIπŸ‘‰ DONDOO KUHUSU TEZI DUME

KUHUSU WANAWAKE

By, Melkisedeck Shine.

BABA NIFUNDISHE KUHUSU WANAWAKE

"Nikufundishe nini mwanangu kuhusu wanawake? Baba yako nimezeeka ghafla nikiwa na ufahamu mdogo na mwanangu umeshakua kiasi cha kuhitaji elimu hii adhimu, nikupe neno gani?, labda hivi,

1.KUHUSU TAMAA ZAO.
-Mwanamke yeyote anaweza kukutamani kimapenzi isipokuwa Mama yako.

2. KUHUSU HULKA ZAO.
-Wanawake wote huonesha upendo wao waziwazi isipokuwa wale waliotendwa kabla.

3.KUHUSU KUACHANA.
-Mwanaume kumuacha mwanamke anayempenda ni kama simba kuacha kula swala, Mwanamke kumuacha mwanaume ni rahisi kama swala kumkimbia Simba mzee
.
4.KUHUSU TABIA.
-Jihadhari na maneno ya vijiweni kwamba wanawake wote wako sawa kitabia. No, lakini kumbuka hakuna Mwanamke asie Mwanamke.

5. KUHUSU MPENZI WA ZAMANI.
-Kujaribu kumsahau mwanamke uliyewahi kumpenda ni kama kumkumbuka mtu usiyemjua. Ni ngumu.

6. KUHUSU KUOA.
-Muhimu kuoa, na ni ngumu sana Kumjua mke mwema kabla ya kuoa, ni waigizaji wazuri sana. Kumbuka maneno ya Albert. " Muhimu kuoa, ukipata mke mwema utakuwa na furaha, ukipata mke mwovu utakuwa mwanafalsafa.

7. KUHUSU USALITI.
-Vizuri kujiandaa kisaikolojia kusalitiwa, la usipojiandaa ama waweza kuua mtu au hata kujiua. ukiua mtu maisha yako yatakosa furaha siku zote, ukijiua mwenyewe, hao waliokusaliti wanaweza kuishi kwa furaha zaidi ya ulivyokuwa hai.

8.KUHUSU PESA NA MAPENZI.
-Mapenzi bila pesa yanapatikana kwa wingi sana huko mbinguni, hapa duniani ni ngumu mno, lakini usihofu sana, kuna makubaliano bila pesa. Omba mungu.

9. KUHUSU UONGO.
-Wahenga walisema Ukweli unauma, Na mimi nakuambia "Uongo unaua"

10. KUHUSU KUWAJUA WANAWAKE.
-Ewe mwanangu, kutaka kumjua mwanamke unahitaji miaka mingi ya kuishi kuliko idadi ya nywele zao. Usihangaike na vitabu, makala, majarida, filamu, nyimbo na hotuba za wanaofundisha mandhari za wanawake. Kuna kanuni moja tu ya kupenda, " ili ubaki salama katika kupenda sharti ujipende kwanza".

…Basi mwanangu hayo ndio machache naweza kukuhusia, na wewe una nafasi ya kujifunza zaidi na kufundisha kwa ufanisi zaidi kuliko Mimi…

Umependa elimu gan hapo??
Shea uwezavyo na wengine.

NIMEOKOTA MAHALI HII.

Usisahau kushare makala hii uliyoisoma kuhusu; KUHUSU WANAWAKE. Share Facebook, Twitter bila kusahau WhatsApp.

Makala hii kuhusu, KUHUSU WANAWAKE, imeonekana kupendwa na wasomaji wengi. Makala nyingine zinazopendwa ni kama hizi zifuatazo;

β€’ Mawaidha kwa Bwana Harusi mtarajiwa, endelea kusoma...

β€’ UMETOKA KAZINI UMEKUTA PANYA 6 ndani, endelea kusoma...

β€’ Nguvu ya umoja na ushirikiano, endelea kusoma...

β€’ USIPITE BILA KUSOMA HII, endelea kusoma...

β€’ KAMA ULIZALIWA BAADA YA MWAKA 90 HAYA AMAMBO YALIKUPITA, endelea kusoma...

β€’ Kuangalia picha za ngono, endelea kusoma...

β€’ Haya ndio maisha ya ndoa, endelea kusoma...

β€’ Nguvu ya umoja na ushirikiano, endelea kusoma...

β€’ FAHAMU NGUVU ZAKO ZA KUZALIWA, endelea kusoma...

β€’ Simulizi ya mapenzi, endelea kusoma...

Unaweza kusoma makala mpya nzuri kila unapotembelea website hii wakati wowote. Baada ya kusoma makala hii kuhusu; KUHUSU WANAWAKE, sasa endelea kusoma makala hizi nyingine nzuri nilizokuandalia;

FURSA.PNG

Fursa Ya Kazi Na Ajira Yenye Malipo Mazuri

Au soma zaidi hapa

.