Kisa cha kusisimua: Funzo kwa mabinti

By, Melkisedeck Shine.

Kijana maskini na mwenye maisha duni alimpenda msichana mmoja
Baada ya kutumia muda mwingi kumfikiria msichana huyo,
Siku moja akaamua kumwita na kumwambia ukweli ya kwamba amempenda na angehitaji kumuoa.

Msichana kwa nyodo na jeuri akasema "sikiliza tena unisikilize kwa makini wewe maskini mshahara wako unaopokea kwa mwezi hautoshi hata kwa matumizi yangu ya siku moja sasa utawezaje kunitunza mm!

Kwaufupi mm sio levo zako hivyo basi sahau kabisa kuhusu kunipata mimi
Nenda katafute maskini mwenzio atakae endana na maisha yako,
Mwisho akamwangalia kwa dharau na kisha akaenda zake.

Kwanzia siku ile kijana hakubahatika tena kumuona msichana yule lkn kwakuwa alimpenda basi hakuweza kumsahau kirahisi rahisi siku zilienda na miezi ikasonga,
Miaka 10 baadae wawili hawa walikuja kukutana katika supermarket moja hivi mjini

Kijana alipomwona msichana alitabasamu lakin kabla hajasema chochote msichana kama kawaida yake kwa dharau akasema "we maskin upo! hivi na ww unaingiaga supermarket eh!

Akaongeza huku akisema walau sasahivi nakuona umependeza inaonekana boss wako kakuongeza mshahara
ila kwa kifupi naomba nikwambie sasahivi nimeshaolewa mume wangu anafanya kazi kwenye kampuni moja hivi ya mtu binafsi kampuni maarufu sana na mshahara wa mume wangu ni shilingi milioni moja na laki mbili kwa mwezi na malupulupu mengine kibao,
Unafikiri ww na umaskini wako kuna siku utakuja kufikia kiwango cha mshahara anachopokea mume wangu!

Macho ya kijana yalitokwa na machozi kwa kuona msichana hajabadilika na anaendelea kuwa na maneno ya kejeri na dharau.

Mara hii mume wa yule dada akaingia ktk supermarket
Ile kumuona yule kijana mume akasema "ooh! Kiongozi upo hapa! Leo imekuwa bahati umekutana na mke wangu!" Kisha akamgeukia mke wake na kusema "mke wangu huyu ndo boss wangu

Na unajua nn mke wangu usishangae kumuona boss wangu anakuja kununua vitu mwenyewe hapa supermarket ukweli ni kwamba boss wangu hana mke, anasema alisha wahi kumpenda msichana mmoja lakini hakufanikiwa kumpata na amekuwa na ndoto ya kuja kukutana tena na msichana huyo ndio maana mpaka sasa bado hajaoa.

Akaendelea kusema hebu fikiria ni bahati kiasi gani alikuwa nayo msichana huyo kama angekubali kuolewa na boss wangu leo hii siangekuwa
maisha!

Muda wote msichana alikuwa kimya hajui hata ajibu nn kwa dharau alizomuonyesha kijana tangu mwanzo.


UJUMBE WANGU
Kwenye maisha mambo huweza kubadilika kama vile upepo unavoweza kubadili mwelekeo kulingana na masaa Hivyo basi usimdharau na kumbeza mtu yeyote kwa sababu ya hali aliyonayo,
Maana kila mtu anafungu lake alilopangiwa na Mungu,

Lakini pia kumbuka hakuna ajuaye kesho
Wakati mwingine mtu unayemdharau leo ndiye huyohuyo ambaye kesho utasimulia mafanikio yake.

Kwako unayesoma ujumbe huu nakuombea Mungu akakufungulie milango ya baraka na kuyapa thamani maisha yako ili pale ulipozomewa ukashangiliwe na wale wote waliokudharau punde wakapate kukupigia magoti kwa uweza wa Mungu.

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Kisa cha kusisimua: Funzo kwa mabinti;

a.gif Sababu 5 zinazosababisha wanawake warembo wazuri wasiolewe

Wanawake wengi warembo husalia peke yao na kufa katika hali hiyo kutokana na sababu tofauti… endelea kusoma

a.gif Kisa cha kusisimua cha kijana na mke wake na mama yake

Kuna kijana mmoja daktari alikwenda kuposa. Binti aliyemposa akamuwekea masharti mazito. Akamwambia chagua mawili imma kunioa mimi au kukaa na mama yako, kwa sababu ukinioa mimi sitokubali mama yako aje hata harusini kwangu! Yule kijana aliemewa. Hakujua la kufanya. Mke anamtaka, lakini mama yake pia anampenda… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kumfanya mwanamke afurahi na akupende kwa kumfanyia mambo anayoyataka

Kuna mambo ya msingi ambayo mwanamke anahitaji kutoka kwa mwanamme ili kufurahi na kutulia katika mahusiano japokuwa sio rahisi kukwambia mojakwa moja… endelea kusoma

[Fumbo Kwako] πŸ‘‰Je, glass ina Maji kiasi gani?

[Video Nzuri] πŸ‘‰Cheki hawa wanavyoonyeshana ubabe

[Chemsha Bongo Kwako] πŸ‘‰Ni namba gani inayofuata hapa chini mwisho?

KADI-MSAMAHA-MZAZI.JPG

a.gif Sababu ya Wasichana wengi kutoolewa ni hizi

KWANINI MABINTI WENGI HAWAOLEWI..!
zifuatazo ni baadhi ya sababu kwanini mabinti wengi wanashindwa KUOLEWA…. endelea kusoma

a.gif Huu ndio ukichaa wa mapenzi

πŸ”΅Kushika mimba ukadhani ni mtego ili uolewe.
πŸ”΅ Kutafuta mkamilifu wakati tabia zako tunakuvumilia tu.
πŸ”΅ Kutafuta msichana mrembo wakati huna pesa.
πŸ”΅ Kutafuta mke mwema kanisani wakati we unaenda kanisani wakati wa maombi ya Christmas tu… endelea kusoma

a.gif ZINGATIA HAYA

KAPIMWE AKILI…
1. Kama wewe ni kijana na una nguvu za kutosha ila kila cku unailalamikia serikali kuwa ajira hakuna, pumbaff kapimwe akili… endelea kusoma

a.gif Ushauri kwa vijana wenye miaka 22 nakuendelea

Ikiwa wewe ni kijana na Una umri wa kuanzia miaka 22 na Kuendelea
Soma hapa ujifunze maisha ya hekima na namna bora ya kuishi na kufanikiwa ungali kijana.. endelea kusoma

[Msemo wa Leo] πŸ‘‰Kufanya Biashara vizuri

[Jarida la Bure] πŸ‘‰Picha Kali Za Kuchekesha

[Hadithi Nzuri] πŸ‘‰Jinsi mke alivyotoboa siri ya Mmme wake

FURSA..! Kuna nafasi za kazi 100.

Au soma zaidi hapa

.

tafuta-rafiki.gif
KADI-TUKUTANE-MZAZI.JPG

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.