Kinachoimarisha uwezo na ujuzi wa mtoto

Mpendwa Msomaji, baada ya kukuandalia makala inayopendwa kuhusu; SIFA ZA MUME MWEMA, sasa nimekuandalia makala hii kuhusu;

Kinachoimarisha uwezo na ujuzi wa mtoto.

Unaalikwa pia kusoma kuhusu; Jinsi ya kumshawishi mwanamke kufanya mapenzi.

Kinachoimarisha uwezo na ujuzi wa mtoto

By, Melkisedeck Shine.

Nini kinaimarisha au kuharibu uwezo wa mtoto?

Imeandikwa na Dismas Lyassa

Kuna baadhi ya vyombo vya habari hasa redio zimenipigia simu kutaka kujua ufafanuzi kuhusu mtoto mdogo ambaye ameweza kutaja majina ya viongozi; kwamba nini hasa kimechangia hali hiyo na je anaweza kuendelea kuwa hivyo au la. Lakini pia wakataka kujua mambo gani yanayosababisha mtoto kuimarika au kuharibika uwezo wake katika kupambanua mambo.
Nimekuwa nikishughulika na mambo haya kwa mwaka wa 12 sasa. Jambo la kwanza na la msingi sana ni kwa wazazi kutambua kwamba wao wanayo nafasi ya angalau kuzaa mtoto mwenye hali nzuri au hali mbaya kwa maana ya uwezo wa mtoto katika kupambanua mambo.
Wazazi wana nafasi kubwa ya kuzaa watoto ambao watakuwa mzigo kwa taifa au watakuwa faida kwa taifa.
KABLA YA KUZALIWA NA BAADA YA KUZALIWA
Wakati mtoto anapokuwa tumboni, ni wakati muhimu sana wa kumtengeneza mtoto tabia na hali ya maisha yake. Kuwa na uhusiano mbaya na mwanamke wakati ni mja mzito, sio tu kwamba unahatarisha maisha ya mama, bali unahatarisha maisha ya mtoto aliyeko tumboni.
Kinamna gani hasa?
Sote tunafahamu uja uzito ni ujenzi wa mtoto, anajengwa kwa maana ya kuwa na viungo vya mwili, ubongo na kadhalika. Ni ndoto kumteja mwanamke akiwa mja mzito kisha kuamini kwamba utapata mtoto mzuri; badala yake tarajia kupata mtoto ambaye huenda utakuwa na kazi kubwa ya kupiga makelele na ikawa bado ngumu kukuelewa.
Mfano; Mke anaaga kwamba anakwenda kutembea kwao, mwisho wa mwezi unafika anaona mabadiliko katika mwili, anapiga simu kwa mumewe kwamba “Mume wangu mpenzi nikwambie kitu…oohh nahisi nina uja uzito”.
Mume akajibu: Usiniambie ujinga huo, hiyo mimba siielewi, kaa hukohuko, hadi utakapojifungua, niangalie sura ya mtoto ndipo tutajua kama tunaendelea pamoja au tunaachana.
Trust me….mtoto akayezaliwa atakuwa ni problem problem problem….huenda akawa mwenye mapepe kupitiliza na asiyependa shule wala hatakuwa na usingivu…ubongo wake ‘umevurugwa’; kama ambavyo mama alivurugwa, mtoto pia hakuwa na raha yoyote, ni shida tu aliyokuwa nayo, huenda mama hata kula wakati mwingine hakuweza kula vizuri…hakuna shaka kwamba alikuwa ni mwenye msongo wa mawazo uliopitiza.
Kwani msongo wa mawazo una athari gani?
Mtu anapokuwa na msongo wa mawazo, mzunguko wake wa damu unakuwa hauko sawa, kwamba kama ni damu ambayo inaingia kwenye moyo aidha itakuwa inaingia kwa wingi au kidogo, hapo ndipo huweza kuwa mwanzo wa magonjwa kama ya moyo, yanayoweza kusababisha kisukari na mengineyo.

Mtoto huwa anajengwa au kuharibiwa uwezo wake wa kupambanua mambo namna gani?

Hakuna jibu la moja kwa moja, lakini tafiti nyingi duniani na hata ninavyoelewa ni kwamba mtoto huweza kutengenezwa au kuharibiwa baada ya kuzaliwa kwa mambo kadhaa yakiwemo aina ya vyombo vya habari anavyoviangalia; TV na vipindi gani huwa anaangalia.
Miziki ambayo anapendelea kusikia (kama una mtoto, mwambie niimbie nyimbo, je atakuimbia nyimbo ya namna gani?). kuachishwa kunyonya haraka au kuendelea kunyonya muda mrefu, kuwa na vitabu nyumbani au kutokuwa navyo; kumshawishi asome au kutomshawishi. Kumpa vyakula kulingana na ushauri wa daktari au unampa tu mtoto chakula ili mradi tumbo limejaa.
1. Sio sawa sana kumuacha mtoto wa miaka miwili kuangalia TV; hasa kumuwekea chumbani kwake ili eti acheni nk

Huko Marekani tafiti zinaonyesha asilimia 59 ya watoto wenye umri wa miaka miwili wanaangalia televisheni. Hata hivyo utafiti wa hivi karibuni wa taasisi ijulikanayo kama The American Academy of Pediatrics umeonyesha kuwa kuwapa fursa watoto kuangalia TV na hasa kuwapa muda mrefu kuangalia TV hakuwasaidii chochote zaidi kunawaumiza, watoto ndio kwanza wametoka kuzaliwa, wanatakiwa waachwe wakue akili zao polepole, sio kuanza kuwamezesha vitu visivyo na maana. Mtalaamu wa masuala ya ubongo wa taasisi hiyo Roberta Golinkoff, ambaye ni mwandishi mwenza wa utafiti mwingine Einstein Never Used Flashcards: How Our Children Really Learn—And Why They Need to Play More and Memorize Less.

Mtafiti huyo anasema “Lugha ni muhimu sana kwa maisha ya mwanadamu, na kwamba lugha ambazo wanakutana nazo kwenye televisheni hazina msaada kwao, ni uchafu tu wanaingizwa kwenye ubongo. Mengi ya yale ambayo yanaonekana kwenye televisheni au kama ni vichekesho, havijibu maswali muhimu kuhusu maisha yao ya kila siku huko mbeleni…watu wanahitaji kujifunza vitu vya maana sio vikaragosi au vitu vya vita ama vichekesho”.

Kama unataka kuwa na mtoto smart, mwache apumzike wala usimsikilizishe uchafu…anachokisikia mara nyingi au anachokiona mara nyingi ndicho kinachojaa kwenye ubongo wake”
Watafiti wengine, Elizabeth A. Vandewater, et al. “Digital Childhood: Electronic Media and Technology Use Among Infants, Toddlers, and Preschoolers.” Pediatrics, 119 (5), 1006-15, anasisitiza kwamba msingi wa kuwa na mtoto bora ni kuhakikisha unamlea vizuri kwa kumuonyesha vitu vizuri, sio uchafu na video au kumuonyesha vipindi vya televisheni visivyo na maana kwake. Kama unampa mtoto nafasi ya kuangalia vikaragosi/vichekesho maana yake unataka mtoto wako awe na mambo ya vikaragosi na mambo yasiyo na maana.
Ni kama shambani unapanda bangi halafu unatarajia kuvuna mpunga. Hufanyi sahihi.
Mtoto anatakiwa kuangaliwa katika uangalifu wa hali ya juu kwa maana ya malezi na hata ulaji wake. Kwa mfano katika saikolojia tunaamini kwamba mtoto ambaye anakumbana na visa au hali Fulani katika maisha yake akiwa na umri wa miaka 1-6 ubongo wake unakuwa ‘stunted’; kwamba ubongo wake unajifunza kufikiri kwamba maisha ndiyo yale aliyoyaona akiwa na umri huo…jambo huko mbele anaweza kubadilika, lakini itegemea zaidi na aina ya watu ambao atakutana nao, kama atakuwa ni mwenye dini au aina nyingine ya ushauri mzito unaoweza kumtoa kwenye hali hiyo.
2.Kama huna sababu za maana sio sahihi kumuachishwa mtoto kunyonya haraka; Mtoto mwenye umri wa miaka 6 ambaye amenyonyeshwa vizuri, walio wengi, huwa na uwezo mzuri zaidi kuliko yule ambaye hakunyonyeshwa vizuri, hii ni katika testi za kuangalia uwezo wa ubongo (IQ tests).
Hili ambalo nalizungumzia juu, limethibitishwa na tafiti mbalimbali, ikiwamo ya raia wa Belarusi na watoto wao; kwamba kulikuwa na makundi mawili, ya kinana ambao walikuwa wakiwanyonyesha watoto wao mara kwa mara bila kuwapa kitu kingine zaidi kwa mwaka mzima. Kundi la pili katika utafiti huo ni la wanawake ambao hao ni wale akina bizeeeeee…bizeeee bizeeee unaijua bizeee wewe….hao ni wale ambao waliwanyonyesha watoto kwa shida, kwamba ndani ya miezi kadhaa hadi mwaka watoto wamekuwa wakipambana na vyakula vingine vya ajabu kama uji na kadhalika huku wakati mwingine wakinyonya kidogo kuliko wanavyokula vitu vingine (kwamba ukijumlisha vitu ambavyo vinaingia tumboni mwa mtoto kwa siku, unakuta uji, maji ya kuchemsha sijui ya dukani na kadhalika ni mengi zaidi hayo kuliko maziwa halisi ya mama); Utafiti ulikuja na matokeo kwamba wale watoto ambao wazazi wao waliwanyonyesha mwaka mzima bila kula kitu kingine zaidi ya maziwa ya mama zao (hata kama ni maji nk basi yalikuwa kidogo kuliko maziwa ya mama zao), hao walikuwa na uwezo mkubwa sana katika kusoma, kuandika na hesabu. Naomba nieleweke kwamba hapa sizungumzii maziwa ya makopo, hayo ni sawa na uji nk..nazungumzia mtoto kunywa maziwa halisi ya mama yake, sio vitu vingine.
Jambo la msingi sana kwa mama kumpata mtoto ambaye atakuwa smart kichwani ni kuhakikisha anamnyonyesha vizuri; kwamba kipaumbele chake kinakuwa ni kuhakikisha mwanae ananyonya zaidi na tumbo la mtoto kuwa na maziwa mengi zaidi ya mama yake mzazi, badala ya vitu vingine.
Haya sio tu maneno ya Dismas Lyassa, bali hata wasomi wengine wanakiri hilo kwamba kunyonyesha ni jambo muhimu sana kwa ukuaji wa mtoto. Msomi mkongwe katika masuala ya ukuaji wa watoto nchini Marekani Ricki Lewis, anasema katika utafiti wake alioupa jina The Forever Fix: Gene Therapy and the Boy Who Saved It…anasema kwamba maziwa ya mtoto yana msaada mkubwa sana katika ukuaji wa mtoto; sio maziwa na mbuzi, ng’ombe kama ambavyo baadhi ya wanawake wamekuwa bize nayo. MAZIWA YALIYO MUHIMU NI MAZIWA YA MAMA.
Mtafiti mwingine, Michael S. Kramer, et al. “Breastfeeding and Child Cognitive Development.” Archives of General Psychiatry, 65 (5), 578-584, anasisitiza hilo la umuhimu wa kumnyonyesha mtoto maziwa halisi ya mama angalau kwa wingi katika kipindi cha mwaka mzima, kuliko kitu kingine chochote.
3. Mtoto ambaye nyumbani kwake angalau kuna maktaba ya vitabu ana nafasi kubwa zaidi ya kufika mbali kimasomo na maendeleo kwa jumla, kuliko yule ambaye hata Biblia au Quran hakuna.
Huu ni utafiti ambao ulifanywa mwaka 2007; watafiti wenzangu wanasema “Success in school depends on more than just native intelligence. It also requires a good work ethic,” anasema mwanasaikolojia, Eileen Kennedy-Moore, katika chapisho lake alilolipa jina la Smart Parenting for Smart Kids.
Anasema “Mtoto anajifunza zaidi kutoka kwenye nini tunachokifanya, kuliko nini tunachokisema”.
Mtoto anajifunza zaidi kutokana na matendo ambayo wazazi wao wanayafanya. Kwa maana kwamba kama mzazi anakuwa bize kusoma vitabu wakati Fulani, kwa sababu watoto hupenda kuwa karibu na wazazi wao, nae atajikuta anasoma vitabu na kuanza kuuliza maswali hii nini huyu nani, hatimaye unamjengea uwezo na upendo wa kusoma.Utafiti huu unaungwa mkono pia na msomi mwingine M.D.R. Evans, et al. “Family Scholarly Culture and Educational Success.” Research in Social Stratification and Mobility, 28 (2), 171-197.
6. Mtoto ambaye mama yake analewa, anatumia dawa za kulevya, sigara na anasa nyingine zenye athari kama hizo kama milungi nk, mtoto ana nafasi ndogo ya kuwa bora kuliko yule ambaye hatumii vitu hivyo.
Utafiti mmojawapo nchini Marekani unaonyesha kuwa asilimia 14 ya watoto ambao wazazi wao wanatumia cocaine, watoto wao uwezo wao (IQs) ulipungua kwa zaidi ya asilimia 70. Hii ni kulingana na utafiti wa Journal of the American Medical Association.
Watafiti waliosimamia utafiti huu ni L.T. Singer, et al. “Cognitive and Motor Outcomes of Cocaine-Exposed Infants.” Journal of the American Medical Association, 287, 1952-1960.
7. Watoto wenye uzito na unene mkubwa kuliko wenye miili ya kawaida

Wasomi katika Chuo kikuu cha Temple wamebainisha kwamba watoto ambao wana uzito mkubwa, hata darasani pia wanakuwa wazito; bongo lala. Jambo sio wote ila wengi wa watoto wenye miili mikubwa darasani hawana uwezo mkubwa. DARASANI KWENU KUNA MTU MNENE HALAFU ALIKUWA NAMBA MOJA MFULULIZO? Huenda akawa, lakini ni nadra, ndivyo tafiti zinavyoonyesha. Aliyeongoza utafiti huo ni Golinkoff.”
Mtafiti mwingine, Stuart Shore, et al. “Decreased Scholastic Achievement in Overweight Middle School Students.” Obesity, 16 (7), 1535-1538 anapigilia msumari akisema kwamba unene sio jambo zuri kwa mtoto. Ni vizuri kuzungumza na madaktari ili kuona namna gani atakuwa na hali bora kiafya
8. Mtoto kufanya mazoezi huongeza uwezo wake
Mtafiti John Medina katika kitabu chake Brain Rules for Baby amebainisha kuwa pamoja na mambo mengine mtoto ambaye anakuwa na mafanikio bora darasani ni yule anayependa kujichanganya na kupenda michezo. Ni vizuri tukawazoesha watoto wetu kupenda mazoezi.
John Medina amefanya pia utafiti mwingine na kuupa jina . Brain Rules for Baby: How to Raise a Smart and Happy Child from Zero to Five. Seattle: Pear Press, 2010, zaidi akisisitiza umuhimu wa kufanya mazoezi ili kuhakikisha mtoto anakuwa na afya bora, kama mojawapo ya njia ya kumsaidia kuwa mwenye uwezo wa kupambana na mambo mengi katika maisha.
9. Asilimia 52 ya watoto waliosoma chekechekea wana nafasi kubwa ya kufika chuo kikuu kuliko wale ambao hawajasomea chekechea.
Utafiti huu ulifanyika Michigani, Marekani. Kwamba kulikuwa na makundi ya watu wa aina mbili, wale ambao wana umri wa miaka 40. Kwamba ilibainika wale ambao wakiwa na umri wa miaka 3 hadi 4, walisoma chekechekea, walikuwa wengi zaidi vyuo vikuu, kuliko wale ambao hawakusoma chekechekea.
Utafiti ulienda mbali zaidi na kubaini kwamba wengi wa wale ambao hawakusoma chekechekea, hadi wanafika umri wa miaka 40 walikumbwa na visa vingi vya kiharifu huku pia wengi wakionekana kutosoma zaidi (wanakuwa hawana hamu sana ya kusoma), hii inachangiwa na ile niliyoieleza juu kwamba mtoto anapokuwa katika maisha Fulani akiwa na umri wa mwaka hadi miaka sita, ubongo wake unakuwa stunted (unajifunga na kuishi hivyo), ingawa kwa jitihada za wataalamu wa saikokolojia na kadhalika wanaweza kubadilika tabia.
Baadhi ya wasomi ambao wamewahi kufanya utafiti huu ni L. J. Schweinhart, et al…ambaye utafiti wake aliupa jina “Lifetime Effects: The HighScope Perry Preschool Study Through Age 40.” Monographs of the HighScope Educational Research Foundation, 14.
10.Mtoto ambaye baba yake alimzaa akiwa na umri wa miaka 20-30 anakuwa na uwezo mkubwa zaidi (IQ) mara tatu hadi sita zaidi, kuliko yule ambaye amezaliwa akiwa na umri wa 40 na kuendelea juu.
Kwamba baba anapokuwa mtu mzima sana…tafiti zinaonyesha upo uwezekano wa kuzaa mtoto ambaye anakuwa hivyo kama ambavyo nimeeleza juu (Advanced paternal age is associated with an increased risk of neurodevelopmental disorders such as autism and schizophrenia, as well as with dyslexia and reduced intelligence,”…usiogope…haina maana kwamba wote wanakuwa hivyo, ila walio wengi.
Utafiti huu umefanywa pia na watafiti kadhaa akiwamo S. Saha, et al. aliyeupa jina “Advanced Paternal Age Is Associated With Impaired Neurocognitive Outcomes During Infancy and Childhood.” PLoS Medicine, 6 (3).
11. Watoto wa maskini husikia maneno machache, kwa tofauti ya mara nne, kwa mwaka, ukilinganisha na watoto walio kwenye familia za kati na matajiri.
Ni kwamba kwa kadri unavyosikia maneno mengi, ndivyo unavyofahamu mambo mengi. Kwamba wakati watoto wa familia za kina tia mchuzi pangu pakavu wanasikia maneno milioni kwa mwaka, watoto wa familia ya kati na matajiri wanasikia zaidi ya maneno milioni 6, huku watoto ambao wazazi wao wanaishi katika professional class (wasomi nk) wanasikia maneno zaidi ya milioni 11. Watoto wa kimaskini hadi anafika umri wa miaka mitatu, wanafahamu kwa uhakika maneno angalau 500, ukilinganisha na 750 na 1,100 kwa watoto wa makundi yaw a kati na matajiri, hii ni kulingana na utafiti uliofanywa na wakongwe, Todd R. Risley na Betty Hart na kuupa jina Meaningful Differences in the Everyday Experience of Young American Children. Baltimore: Brookes Publishing, 1995.
12. Watoto ambao wanatumia kompyuta kwa sababu mbalimbali angalau saa mbili kwa siku, wana uwezo mara 9.4 zaidi ya wale ambao vitu hivi hawavitumii
Hii ni kulingana na utafiti wa Barry Ip, et al. “Gaming Frequency and Academic Performance.” Australasian Journal of Educational Technology, 24 (4), 355-373.
15. Mtoto ambaye mama yake anatumia bodaboda au anaendesha baiskeli akiwa mja mzito, uwezo wake unakuwa mdogo zaidi katika kuelewa mambo kwa asilimia 1.4, ukilinganisha na wale ambao hawafanyi hivyo.
Huu ni utafiti wa Chuo kikuu cha Columbia, ulioongozwa na V. Rauh, et al. na kupewa jina Seven-Year Neurodevelopmental Scores and Prenatal Exposure to Chlorpyrifos.” Environmental Health Perspectives, 119 (8).
Dismas Lyassa ni Mkurugenzi na Mtaalam wa saikolojia kutoka taasisi ya Global Source Watch, pia ni mtafiti na mchangiaji makala katika majarida mbalimbali ya kimataifa likiwamo Indian Institute of Sexology Journal la India. Anapatikana kwa simu 0754498972 waweza kupiga au whatsp kwa ufafanuzi kwa jambo usilolielewa.
Ombi langu kwako wewe ambaye umefanikiwa kupata ujumbe huu sambaza kwa wingi kwenye magroup ya facebook, whatsap, instargram etc

Hongera kwa kusambaza jambo jema….Mungu na akubariki

Usisahau kushare makala hii uliyoisoma kuhusu; Kinachoimarisha uwezo na ujuzi wa mtoto. Share Facebook, Twitter bila kusahau WhatsApp.

Endelea kusoma makala hizi;

a.gif Soma hapa wewe kijana wa kiume
Nawaandikia ninyi vijana wa kiume na wanaume wote,
maana mna nguvu na mmejaliwa na mwenyezi Mungu utashi,
hekima na busara ili muweze kutawala kila kitu tokea kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu huu
soma zaidi
a.gif Sera ya mapenzi kwa vipindi tofauti tofauti
MIAKA YA:
1986-1990. Ukimtongoza binti, alikuwa akijibu
"NIMEKUBALI ila usimwambie mtu..!".. soma zaidi
a.gif Mambo ya kuzingatia kabla ya kuingia kwenye ndoa
NI VEMA UKAYAJUA HAYA KABLA YA KUINGIA KWENYE NDOA:.. soma zaidi
a.gif Sababu ya Wasichana wengi kutoolewa ni hizi
KWANINI MABINTI WENGI HAWAOLEWI..!
zifuatazo ni baadhi ya sababu kwanini mabinti wengi wanashindwa KUOLEWA…. soma zaidi
a.gif UMETOKA KAZINI UMEKUTA PANYA 6 ndani
UMETOKA KAZINI UMEKUTA PANYA 6 ndani.
Panya wa 1- Anakula Vyet vyako vya degree ya pili.­
Panya wa 2- Anakula cheti chako cha Ndoa
Panya wa 3- Anakula Hati ya kusafiria na safari ni kesho… soma zaidi
a.gif Hadithi ya kusisimua, jifunze kitu hapa
By Malisa GJ,
Alikuwepo mama mmoja aliyekuwa chongo na mwanae alimchukia kwa sababu ya kuwa chongo. Mwanae alijisikia aibu kutembea na mama yake mwenye jicho moja na hakupenda watu wajue kuwa yule ni mama yake… soma zaidi
a.gif Wosia wa mama kwa binti anayeolewa
Wanauliza uko wapi wosia wa mama kwa bintie
anaeolewa? Huu hapa!
Binti yangu, hivi sasa wewe ni mke wa mtu na
karibuni utakuwa mama pia. Mungu amenibariki
nishuhudie jinsi nilivyokufunza kupika na kufanya
shughuli nyingine za nyumbani… soma zaidi
a.gif Mtunzi katumia falsafa Nzuri sana!!
Mtoto mdogo alimfuata baba yake na
kumuliza, "
Nini maana ya SIASA?"
Baba akajibu, " Mwanangu ngoja nijaribu
kujibu kwa mfano huu,
Mimi natafuta fedha
ya matumizi, hivyo niite mimi BEPARI,.. soma zaidi
a.gif Mambo 7 ambayo mwanamme hapaswi kumfanyia mke wake
Mambo 7 ambayo mwanaume apaswi kumfanyia mke wake..
1. Usimpige.
2. Usimtukane na kumshushia heshima… soma zaidi
a.gif Stori ya kweli hii
Kuna story moja ya kweli kabisa binti alikuwa anamnywesha viroba mtoto wa bosi wake. Ni hivi mabosi ni wafanyakazi hivyo binti alikuwa anabaki na mtoto peke yake. Baada ya muda alipata rafiki ambaye alimshswishi kuingia ktk mahusiano ya kimapenzi… soma zaidi

Makala hii kuhusu, Kinachoimarisha uwezo na ujuzi wa mtoto, imeonekana kupendwa na wasomaji wengi. Makala nyingine zinazopendwa ni kama hizi zifuatazo;

• Ndoa nyingine ngumu sana. Soma kisa hiki, endelea kusoma...

• MAANA YA MAPENZI, endelea kusoma...

• Ujumbe Kwa mabinti waliookoka, endelea kusoma...

• Soma hapa wewe kijana wa kiume, endelea kusoma...

• Sera ya mapenzi kwa vipindi tofauti tofauti, endelea kusoma...

• Mambo ya kuzingatia kabla ya kuingia kwenye ndoa, endelea kusoma...

• Sababu ya Wasichana wengi kutoolewa ni hizi, endelea kusoma...

• UMETOKA KAZINI UMEKUTA PANYA 6 ndani, endelea kusoma...

• NAMNA YA KUMTAMBUA MWANAMKE MPUMBAVU NA MWANAMKE MWEREVU, endelea kusoma...

• Siku ya Kupata mimba, endelea kusoma...

Unaweza kusoma makala mpya nzuri kila unapotembelea website hii wakati wowote. Baada ya kusoma makala hii kuhusu; Kinachoimarisha uwezo na ujuzi wa mtoto, sasa endelea kusoma makala hizi nyingine nzuri nilizokuandalia;

FURSA..! Kuna nafasi za kazi 100.

Au soma zaidi hapa

.

KUMSHUKURU-MPENZI-4559KJ438.JPG
SALAMU-ASUBUHI-987HGZ.JPG