Jifunze kuwajali wazazi kwa kusoma kisa hiki

By, Melkisedeck Shine.

elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

Jifunze kuwajali wazazi kwa kusoma kisa hiki

Lameck alikuwa akiendesha gari kwa kasi sana alipokutana na akina Mama watatu ambao walinyoosha mkono kumuomba lift, ingawa alikua na haraka lakini aliwaonea huruma na kusimama, sehemu waliyokuwa ilikuwa ni kichakani na kwakuwa alikuwa peke yake hakuona sababu ya kuwanyima lift.

“Samahani Baba, tunaomba utusaidie tunaelekea, Usangi kwenye msiba sasa tumechelea na magari hamna…” Mama mmoja aliomba. Lameck aliwaambia waingie kwani hata yeye alikuwa anaelekea huko huko.” Wale akina Mama waliingia kwenye gari aliwasalimia na bila hata kuulizwa walianza kujielezea.

“Tunaenda kwenye msiba, kuna Mama mmoja kafariki huko..” Mama mmoja alianza kuongea na mwingine aliendelea… “ahsante sana mwanangu, ni vijana wachache sana wenye roho nzuri kama wewe, wenzako wametupita kama si watu, magari mazuri kama haya yenu hata hayasimamagi. Huko tunakoenda tu huyo Mama wa watu kaumwa kateseka lakini mtoto wake mwenyewe wa kumzaa hata hakuja kumuangalia, majirani ndiyo walimchangia kupelekwa KCMC…”
“Yaani watoto wasiku hizi mpaka mtu unajuta kuzaa, yule Mama alivyohangaika kumsomesha yule mtoto, alikua anatembea na mfuko wa viazi kwenda kuuza sokoni, anafanya vibarua mtoto mwenyewe hata akili alikua hana kila siku kufeli anarudia madarasa lakini Mama wawatu alivumilia….” Mama mwingine aliongea.
“Tena basi alitelekezwa na mume wake…” Aliongea Mama mwingine “…Alikua mume basi, alizaa na msukuma mmoja aliyekuja kufanya vibarua akamkimbia na kumuacha na mtoto mdogo, Mama wa watu kalea mwenyewe mtoto huyo huyo mmoja ila kajumba kalekale ka nmatope ndiyo Mama wawatu kafia wakati mwanae yuko mjini anakula maisha…!”

“Mama wawatu kila siku analia hata aletewe wajukuu tu awaone…”
“Nakuambia, kila siku anasema mimi sitaki hata pesa zake aniletee tu wajukuu zangu na mimi nifurahie kuzaaa..”
“Kijana yuko mjini wala hana habari! Hawa watoto jamani! Heri Mama wa watu alivyokufa akampumzike, ameteseka sana, nasikia walishamtoa jicho lapili alikuwa haoni kabisa…”
“Usiniambie..”
“Kweli eee, mimi nilienda, majirani walikuwa wamemchangia KCMC wakamtoa jicho linguine, Kansa sio mchezo…”
“Sema kuishi na watu vizuri ni jambo jema sana maana asingekuwa na majirani angekua ashakufa muda mrefu… mtoto wa kumzaa anaweza asikusaidie lakini wa jirani akakusaidia..”

Kule mbele Lameck alikuwa akibubujikwa na machozi, yeye ndiye kijana walikuwa wakimzungumzia na Mama yake ndiyo alikuwa maefariki, tangu alipoenda mjini miaka 15 iliyopita alikuwa ahajakanyaga tena nyumbani, alioa bila hata kumuambia Mama yake na hata alipojua aligoma kabisa kumpeleka mkewe na wanae nyumbani.

Maneno ya wale akina Mama yalimuumiza sana hasa walipozungumzia namna Mama yake alivyohangaika naye wakati akiwa mdogo, picha ya Mama yake akilima vibarua, namna alivyokuwa akitokana jasho, picha za mama yake akinyeshewa na mvua, picha za mama yake akatika ofisi za mwalimu mkuu wakati akimtete asifukuzwae shule, picha za Mama yake akimuwashia kibatari usiku ili asome vyote vilimjia akilini.

Alijiona hanathamani kwani hata baada ya kusikia kifo cha Mama yake alishindwa kufanya kitu amabcho Mama yake alikuwa akimuomba kila mara alipompigia simu. Hakutaka kuileta familia yake, hakutaka mke wake na wanae kuona sehemu alipozaliwa kuona hali ya nyumbani kwao hivyo aliamua kwenda mwenyewe mara moja kumaliza mazishi na kugeuza.

Aliumia zaidi aliposikia kuwa kumbe Mama yake alikuwa na Kansa na alitolewa macho yote, hakua na habari hizo kani ni zaidi ya miaka miwili alikuwa hajawasiliana na Mama yake. Mama yake baada ya kumuona hajibu na hamsaidii chochote alichoka kumpigia simu hivyo hata hakujua kuhusu ugonjwa wake.

Machozi yalianza kumbubujika kama maji, alijihisi kama kizunguzugu na kila alipojaribu kulicontrol gari alishindwa, gari liliacha njia na kuserereka mlimani. Alipoteza fahamu na alipozinduka masaa sita baadaye alijikuta amelala hospitalini, aliambiwa amepata ajali, ndipo alipokumbuka ajali ilivyotokea.

Aliulizia kuhusu kina Mama aliokuwa amewabeba akaambiwa walitoka salama bila hata mchubuko, alimshukuru Mungu kwa hilo, hakuwa akisikia maumivu kokote lakini alipojaribu kunyanyuka alishindwa hata kunyanyua kidole. Lameck alikuwa amevunjika uti wa mgongo karibu na shingo hivyo alipooza kuanzia mabegani kushuka chini.

Alipelekwa hospitali kubwa lakini ilishindikana, walimpeleka mpaka nnje ya nchi lakini bado ilishindikana. Ni miaka mitatu sasa bado hajaweza kunyanyuka amelalaa akiwa hawezi kufanya kitu chochote kile. Mke wake ameshaolewa na mwanaume mwingine na wanae wanakuja mara moja moja kumsailimia katika nyumba anayoishi ambayo mkewe ameajiri kijana kwajaili ya kumhudumia.

Lameck amebaki mpweke marafiki wote wamemtenga, hata wanae wanapokuja kumsalimia humuangalia kama kituko flani, huishia tu kumuonea huruma, hana mtu wakuongea naye, Amelia mpaka amechoka, anatamani kufa lakjini hawezi hata kunyanyua mkono kuchukua sumu ajiue. Kila siku nikulia na kumuomba mama yake msamaha.

***MWISHO

Katika kisa hiki nataka ujifunze kitu kimoja kwamba mbali na kuwajali wazazi wako, basi hakikisha na mumeo au mkeo anawajali wazazi wake. Hata kama huwapendi kwa namna gani, wanakunyanyasa na kukudhalilisha, hakikisha mumeo au mkeo anawajali kwani ndiyo wazazi wake.

Laana ya yeye kuwatelekeza wazazi wake kwa sababu yoyote ile haitaishia kwake tu, itakugusa wewe na watoto wako. Hembu leo muambie awapigie simu wazazi wake kama wapo hai na kama Mungu amesha wachukua hembu mkumbueshe kuwatolea sadaka, hata alishe yatima mmoja kwaajili ya wazazi wake.


Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Jifunze kuwajali wazazi kwa kusoma kisa hiki;

a.gif Jifunze kupitia kisa hiki cha mume na mke

Mume alirejea nyumbani na kukuta ujumbe juu ya meza umeandikwa "NIMEONDOKA" ilikuwa jioni, alienda jikoni na kukuta kukavu, aliwaita watoto na kuwauliza wakasema walimuona Mama akiondoka na begi lakini hakuwaambia anaenda wapi. Mume alichanganyikiwa, alijaribu kuchukua simu kumpigia lakini ilikuwa haipatikani, kabla hajafanya chochote mtoto wao wa mwaka mmoja alikuja akilia na kusema ana njaaa… endelea kusoma

a.gif Tafakari kwa Binti kabla ya kuolewa

Ukizungumza na wasichana au wanawake ambao hawajaolewa, unapozungumzia suala la Ndoa, kwa bahati mbaya sana wengi vichwani mwao inajengeka taswira ya harusi. Ukisema Ndoa yeye anawaza gauni jeupe (Shela) lenye mkia mrefu na maids wamelishika huku na huku. Anawaza suti ya mume wake, gari ya kifahari iliyopambwa, sijui wasindikizaji watoto pale mbele. Anawaza Ukumbini, baharini kupiga picha na mwisho usiku wa Honeymoon… endelea kusoma

a.gif Ndoa nyingine ngumu sana. Soma kisa hiki

Misingi mingine ya ndoa zetu ni migumu sana.
Pata simulizi hii toka Marekani… endelea kusoma

a.gif Huu ndio ukichaa wa mapenzi

🔵Kushika mimba ukadhani ni mtego ili uolewe.
🔵 Kutafuta mkamilifu wakati tabia zako tunakuvumilia tu.
🔵 Kutafuta msichana mrembo wakati huna pesa.
🔵 Kutafuta mke mwema kanisani wakati we unaenda kanisani wakati wa maombi ya Christmas tu… endelea kusoma

a.gif Stori ya kweli hii

Kuna story moja ya kweli kabisa binti alikuwa anamnywesha viroba mtoto wa bosi wake. Ni hivi mabosi ni wafanyakazi hivyo binti alikuwa anabaki na mtoto peke yake. Baada ya muda alipata rafiki ambaye alimshswishi kuingia ktk mahusiano ya kimapenzi… endelea kusoma

a.gif Ushauri wa mapenzi

Kuachwa kusikupe Stress, Haijalishi umeachwa mara ngapi, Jali kile ulichojifunza kutoka kwa mtu aliyekuacha… endelea kusoma

a.gif Mambo yakuzingatia kabla ya kuingia kwenye ndoa

Ujumbe wangu kwako Leo: NI VEMA UKAYAJUA
HAYA KABLA YA KUINGIA KWENYE NDOA:
1. Sherehe ya Harusi ni ya siku moja tu, na Ndoa
ni ya maisha yote.
2. Mwanamume/Mwanamke aliyezoea kuchepuka
kabla ya Ndoa, ataendelea kuchepuka hata baada
ya Ndoa… endelea kusoma

a.gif Angalia binadamu walivyo

Angalia Binadamu walivyo!,.. endelea kusoma

elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

.

elimu-sayansi-na-tekinolojia.png
Marafiki-wa-enzi.GIF
familia-mapenzi-na-mahusiano.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.