Kichekesho%20Kipya Usikose πŸ“•Kitabu cha Vichekesho Vikuu Vikali 300+βœ” Kina kurasa 270 zenye pichaπŸ“· na vichekeshπŸ˜‚ zaidi ya 300πŸ’¨πŸ‘‰Bofya hapa KuchukuaKizuri

.

πŸ‘‰ HADITHI: Maisha ya ndoaβœ…

MELKISEDECK-SUA.jpg

Je wajua maelfu ya watu hutembelea blog hii kila mwezi.πŸ˜ƒ Kuwa miongoni mwao na wewe kwa kutembelea blog hii kila siku. Baada ya kusoma posti kuhusu;

images-8.jpeg

Leo nimekutayarishia makala kuhusu HADITHI: Maisha ya ndoa.

HADITHI: Maisha ya ndoa

Baada ya kumaliza sherehe ya ndoa yao, mama wa bibi harusi alimpa binti yake notebook yenye namba mpya ya Akaunti ya benki ikiwa na kiasi cha shilingi laki tatu.

Mama alimwambia hivi, "binti yangu, chukua hii notebook, itunze kama kitu cha kuandikia rekodi katika maisha yako ya ndoa, chochote cha kufurahisha kitakachotokea katika maisha yako haya mapya na mumeo, weka pesa katika akaunti hii na uandike katika notebook juu ya hiyo furaha yako/yenu.

Matukio ya kufurahisha yatakavyotamalaki katika ndoa yenu yakizidi nawewe ndio uzidi kuweka kiwango zaidi cha fedha utakayokuwa nayo kama akiba bila kusahau kuweka rekodi ya hiyo furaha.

Fanya hili na mumeo ili mtakapotizama baada ya miaka kadhaa mtambue ni kwa kiasi gani mlikuwa na furaha katika ndoa yenu.

Binti alipokea hayo maelekeza na akaenda kumueleza na mumewe. Wanandoa waliona kwamba ni jambo jema kwao na vilevile ni njia mojawapo ya utunzaji wa fedha.

Wakawa wakisubiri tu panapofuraha kati yao ili wewekeze hizo pesa.

Hivi ndivyo ile notebook ilisomeka baada ya kipindi kirefu kidogo cha ndoa yao;

7 February- Tsh 100,000 - birthday ya kwanza ya mume wangu tukiwa katika ndoa

1 March- Tsh 110,000- Mume wangu amepandishwa cheo kazini.

20 March- Tsh 120,000 - Tumeenda likizo Zanzibar.

29 April - Tsh 125,000 - Ujauzito wa kwanza.

5 september - Tsh 130,000 Mume wangu amenifulia nguo zangu zote chafu baada ya mimi kuwa hoi ujauzito ukinisumbua.

8 October - Nimemnunulia mume wangu saa aipendayo, amefurahi sana….

List ilikuwa ndefu sana……..

Hata hivyo miaka ilisonga na wanandoa wakaanza ugomvi na mabishano baina yao. Wakawa hawana ukaribu tena na kila mmoja akawa anajutia ndoa yao, hakukuwa na mapenzi tena kati yao.

Siku moja binti alimpigia mama yake simu. "mama siwezi kuvumilia tena, tumeamua tuachane, najuta kwanini nilikubali kuolewa na huyu mwanamume!" Binti alisikika na mama yake akiongea.

Mama yake akamjibu, "Mwanangu siungi mkono jambo unalotaka kufanya ila siyo kesi kubwa fanya kile ambacho moyo wako umeamua ila kabla ya hapo fanya kitu kimoja. Unakumbuka ile notebook niliyokupa? Nenda katoe pesa zote benki na utumie na mumeo kabla hamjaachana.!

Hivyo yule binti alienda benki, na wakati amesimama kwenye foleni alichukua ile notebook na kuanza kusoma matukio ya furaha na faraja waliyoyapitia yeye na mumewe.

Jinsi alivyokuwa akizidi kuyasoma yale matukio ndipo kumbukumbu za furaha na mapenzi vilizidi kuujaza moyo wake, na machozi yakiwa yanamtoka, akaghairisha na kurudi nyumbani.

Alipofika nyumbani alimkabidhi mumewe ile notebook na kumwambia aende akatoe zile pesa wagawane kabla hawajatalikiana.

Nae alipoenda benki akiwa katika foleni akisoma ile notebook nae alipatwa na hali ile ile, aliamua asitoe zile pesa. Na akarudi nyumbani.

Akiwa na mkewe, waliamua kufanya mahesabu wajue ni kiasi gani kilichokuwemo katika akaunti, walipofanya majumuisho ya matukio yote ya furaha waliyoyarekodi walijikuta wakiwa na shilingi milioni tatu na laki tano.

Kwa mshangao mume akamwambia kwamba leo ndio nimegundua ni kwa thamani gani ninakupenda, ni kwa kiasi gani umeleta furaha kwenye maisha yangu, na ni kwa kiasi gani nilivyo mpumbavu kukata tamaa juu yako na kuzitupa kumbukumbu zote nzuri tulizoshea pamoja.

Wakakumbatiana kwa upendo na mapenzi yao yakachanua upya, wakaandika tena lile tukio la kuwaunganisha pamoja na kwenda kuweka pesa benki.

Na notebook wakaitunza tena katika sehemu iliyo salama kwa ajili ya kuendelea kuandika rekodi.
___

Ndoa sio mchezo wa kuigiza, sio kitu rahisi ila ni nzuri. Mtabishana, Mtagombana na kununiana ila ni kawaida kwa sababu kila mmoja ametoka katika familia zenye historia tofauti.

Usitegemee kila utakachozungumza kitakubaliwa na mwenzako moja kwa moja bila kutoa maoni yake. Ila kabla ya kukata tamaa katika ndoa fikiria nyakati nzuri kabisa mlizoshea pamoja na kuwaweka karibu.

Usikubali kupitwa na πŸ“•Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKEπŸ‘§πŸ‘—πŸ‘ . KinamwelezeaπŸ”ŽMwanamkeπŸ” kinagaubagaβœ”. πŸ‘‰Bofya hapa KuchukuaπŸ‘ˆ

images-19.jpeg

πŸ™‰πŸ™‰πŸ™‰Usisahau kushare posti hii kuhusu; HADITHI: Maisha ya ndoa.πŸ’―βœ” Share facebook, twitter n.k bila kusahau WhatsApp, share wengine nao wafaidike!πŸ‘

SOKOINE-UNIVERCITY-OF-AGRICULTURE.jpg

🐼 Endelea kusoma kuhusu;-πŸ™‰

.

Kichekesho%20Kipya Usikose Jarida la Kilimo Bora cha Bamia Linafafanua Kilimo cha bamia πŸ‘‰Bofya hapa KuchukuaKizuri

.

Kichekesho%20Kipya Usikose Jarida la Kilimo Bora cha Matikiti Linafundisha ulimaji wa matikiti πŸ‘‰Bofya hapa KuchukuaKizuri

.

.

.

Kichekesho%20Kipya Usikose πŸ“•Kitabu cha Mbinu za Kilimo Bora Cha MbogaπŸŒΏπŸ… Kina kurasa 100 na utaalamu wa mazao zaidi ya 10.
πŸ‘‰Bofya hapa KuchukuaKizuri

.

.

.

SOKOINE-UNIVERCITY-OF-AGRICULTURE.jpg

Habari msomaji wangu…?
Jina langu ni Melkisedeck Leon Shine Mwendeshaji wa blog hii.

Karibu Katika Blog yangu ya AckySHINE mahali pa kusoma makala kuhusu mada mbalimbali, vichekesho, picha, pamoja na videos

images-16.jpeg

Msomaji wangu mpendwa, asante kwa kuendelea kupenda kutembelea blog hii. Unakaribishwa tena kila siku kwa ajili ya kusoma makala mpya.

SHINE-MWENYEWE.jpg

Blog ya AckySHINE ni Blog pekee ya Kiswahili kwa posti nyingi, isiyochosha kusoma, yenye posti nyingi nzuri mapya kila saa unapotembelea. Unahakikishiwa kupata kitu kipya utakachopenda kila unapotembelea blog hii, Utapata makala, vichekesho, videos, picha n.k. Kwa sasa kuna posti Mpya 6083 kwa ajili yako, ushindwe wewe tuu kuperuzi Blog hii.

width="102"

Ni matumaini yangu kuwa wewe ni miongoni mwa wasomaji wangu wa kila siku wa blog hii, kama sivyo unakaribishwa kuungana na wasomaji wangu wanaotembelea Blog hii kila siku.

width="111"

Chagua unachotaka hapa…
VICHEKESHO | PICHA | VIDEOS {TV} | UJASIRIAMALI | MAHUSIANO | AFYA & MAPISHI | TEKINOLOJIA | BLOG KWA WAKATOLIKI | eBOOK SHOP | MAKTABA

images-15.jpeg

Maisha ya Binadamu ni ya kujifunza na kujielewesha mambo mapya kila wakati. Katika blog hii unaweza kusoma na kujifunza mambo mapya kila wakati.

MELKISEDECK-SHINE.jpg

KUHUSU BLOG HII | MAWASILIANO | ABOUT AUTHOR | LEGAL GUIDELINES