HADITHI YA MFALME ALIYEKUWA NA MBWA WAKALI KUMI

Mpendwa Msomaji, baada ya kukuandalia makala inayopendwa kuhusu; Kujichua kwa wanawake, sasa nimekuandalia makala hii kuhusu;

HADITHI YA MFALME ALIYEKUWA NA MBWA WAKALI KUMI.

Unaalikwa pia kusoma kuhusu; Tabia ambazo zinamfanya mwanamke asiolewe.

HADITHI YA MFALME ALIYEKUWA NA MBWA WAKALI KUMI

By, Melkisedeck Shine.

Kulikuwa na mfalme mmoja aliyekuwa na mbwa kumi wakali sana. Alipenda kuwatumia mbwa hawa pindi akitaka kumuadhibu mtumwa aliyekosea.

Mbwa hawa waliwatesa watumwa kwa kuwararua na meno yao makali! Wakati mwingine watumwa waliokutana na adhabu hii walipoteza uhai.

Siku mtumwa aliyemtumikia mfalme kwa miaka kumi alitoa wazo baya ambalo halikumpendeza mfalme, ikaamriwa akamatwe na kutupwa katika banda la mbwa.

Mtumwa alinung'unika na kusema :"nimekutumikia kwa miaka 10, na leo wanitenda hivi? Naomba unipe walau siku 10 kabla hujanitupa baniani! " Mfalme akakubali.

Katika siku izo 10, mtumwa alimfuata mlinzi wa banda la mbwa na kumuomba ampe nafasi kuwahudumia mbwa wale. Mlinzi alistaajabu ila akakubali. Mara moja mtumwa akaanza kazi ya kuwapa mbwa chakula, kuwaogesha na kila aina ya faraja ambazo wanyama huhitaji.

Siku 10 zikaisha, mfalme akaamuru mtumwa atupwe bandani kutumikia adhabu yake.

Hilo likafanyika kwa haraka, lakini cha kushangaza mbwa walianza kulamba miguu ya mtumwa na si kumrarua kama ilivyotegemewa. Mfalme akastaajabu, akasema:"Nini kimewasibu mbwa wangu? ",.

Mtumwa akajibu :" nimewahudumia mbwa hawa kwa siku 10 tu ila hawajasahau fadhila zangu.

Ila nimekutumikia miaka 10 lakini umesahau yote kwa sababu ya kosa moja tu! " Kufikia hapo mfalme akatambua kosa lake na akaamuru mtumwa aachiwe huru.

FUNZO: Katika maisha kuna watu husahau mambo mema waliyotendewa pindi wakikosewa.

Kamwe usiruhusu historia nzuri kufutika sababu ya jambo moja usilolipenda! Tembea katika msamaha!

Usisahau kushare makala hii uliyoisoma kuhusu; HADITHI YA MFALME ALIYEKUWA NA MBWA WAKALI KUMI. Share Facebook, Twitter bila kusahau WhatsApp.

Makala hii kuhusu, HADITHI YA MFALME ALIYEKUWA NA MBWA WAKALI KUMI, imeonekana kupendwa na wasomaji wengi. Makala nyingine zinazopendwa ni kama hizi zifuatazo;

• Kama una miaka 24 hadi 29 huu ni ujumbe wako, Soma hii tafadhali, endelea kusoma...

• Soma Kisha Jifunze, endelea kusoma...

• Ujumbe kwa wadada, endelea kusoma...

• Neno la kutia Moyo, endelea kusoma...

• KUHUSU WANAWAKE, endelea kusoma...

• USIPITE BILA KUSOMA HII, endelea kusoma...

• KAMA ULIZALIWA BAADA YA MWAKA 90 HAYA AMAMBO YALIKUPITA, endelea kusoma...

• Kuangalia picha za ngono, endelea kusoma...

• Haya ndio maisha ya ndoa, endelea kusoma...

• Nguvu ya umoja na ushirikiano, endelea kusoma...

Unaweza kusoma makala mpya nzuri kila unapotembelea website hii wakati wowote. Baada ya kusoma makala hii kuhusu; HADITHI YA MFALME ALIYEKUWA NA MBWA WAKALI KUMI, sasa endelea kusoma makala hizi nyingine nzuri nilizokuandalia;

Usipitwe na Nafasi za kazi kwa leo

<<Bofya HAPA kujua zaidi>>

.

tafuta-rafiki.gif
SALAMU-MPENZI-MCHANA-33097HG34MX.JPG