Biblia inasema nini kuhusu mume mwema

By, Melkisedeck Shine.

afya-mapishi-na-lishe.png

Biblia inasema nini kuhusu mume mwema

1. Awe mwenye kumcha Mungu

Mume mwema ni yule anayeheshimu nafasi ya Mungu katika maisha yake, anayemcha Mungu na kuepukana na uovu wa kila aina. Anatambua kwamba Mungu ndiye anayepaswa kuongoza maisha yake na si vinginevyo.

Kumbukumbu 6:5 Nawe mpende BWANA Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.

2. Mwenye kumpenda mke wake kama nafsi yake

Kumpenda mke wake zaidi ya kitu chochote iwe ni wazazi, kazi, biashara, watoto n.k. Mume mwema siku zote huthamini nafasi ya mke katika maisha yake na mara zote mke wake ni namba moja kwake.

Mwanzo 2:24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.

Efeso 5: 25,28 Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda kanisa, akajitoa kwa ajili yake,..vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.

3. Mwenye uwezo wa kuiongoza familia yake

Inashangaza kuona baadhi ya waume hawawezi kusimama kama viongozi katika nyumba zao. Wanasahau kama Mungu kawaweka kama viongozi wa familia na mke ni msaidizi wake. Utakuta wengine wanaaacha jukumu hilo kwa mkewe kwa kupenda au kwa kutokupenda na wengine wanajikuta wamewafanya wazazi wao au ndugu zao wengine kusimama kama viongozi wa familia.Biblia inaweka wazi kuwa mume ni kichwa cha ndoa, ni lazima kila mume atambue hilo na ahakikishe anasimama kwenye nafasi yake kwa uaminifu bila kujali hali yake, wadhifa, kipato, huduma au chochote kile.

Efeso 5:23 Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe; kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.

4. Mwenye Kuihudumia Familia Yake

Mume mwema lazima ahakikishe anafanya kazi na kuipatia familia yake mahitaji ya kila siku. Haijalishi mkewe anafanya kazi au la, yeye kama mume anajukumu la kuihudumia familia yake na hii ni sehemu ya uongozi wake. Hapa pia inajumuisha na kuilinda familia yake juu ya hatari zote na kuhakikisha wana furaha na amani ya kudumu. Ili mke na watoto waweze kuwa na amani ni lazima wahakikishiwe usalama wao kimwili, kiroho na kiuchumi.

1Timotheo 5:8 Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.

5. Mwenye kuwafundisha watoto njia inayopasa

Mume kama kiongozi wa familia anajukumu la kuwafundisha watoto njia inayofaa akisaidiana na mke wake. Waume wengi wanafikiri kazi ya kuwafundisha watoto ni ya mama wao ni kutoa tu adhabu pale wanapoona mtoto amekosea lakini hawajishughulishi katika kuwafundisha. Mume mwema lazima alitambue jukumu lake la kuwafundisha watoto neno la Mungu na misingi ya maisha ya mkristo.

Kumbu kumbu 6: 6-7 Na maneno haya ninayokuamuru leo,yatakuwa katika moyo wako; nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena, uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.

Efeso 6:4 Nanyi wakina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya BWANA.

6. Mwenye kumheshimu mke wake

Imezoeleka kuwa mke ndiye anayepaswa kimheshimu mume, lakini biblia inawataka pia waume kuwahepa heshima wake zao na kuishi nao kwa akili. Haipaswi mume kufanya maamuzi yoyote yanayohusu familia bila kumshirikisha mke wake, yawe madogo kama lini mgeni fulani aje hadi makubwa kama ujenzi au kuanzisha biashara. Mke ni sehemu ya mume hivyo ni lazima mume ampe heshima yake na kuthamini mawazo yake na mchango wake hata kama mke hafanyi kazi ya kuingiza kipato. Kumbuka mke anabeba jina la mume wake na ni sehemu ya mume wake, inahuzunisha kuona waume wengine wakiwadharau wake zao mbele ya ndugu zao au marafiki. Haipasi kabisa kumgombeza au kumsema vibaya mke wako mbele za watu, iwe ni ndugu, watoto au mwingine yeyote.

1Petro 3:7 Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.


Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Biblia inasema nini kuhusu mume mwema;

a.gif SIFA ZA MUME MWEMA

1. Ametulia si macho juu juu kama nzi kila akionacho hata kichafu chaliwa.
2. Anajiheshimu, anamuheshimu mkewe, ndugu wa pande zote, watu wengine pamoja na majirani pia.
3. Mwenye huruma na mapenzi ya kweli kwa mke na familia kwa ujumla.
4. Mtunzaji wa familia na si bahili au mfujaji wa mali.
5. Mcha mungu, au mwenye utu… endelea kusoma

a.gif Sifa za mke mwema

Mithali 14:1“Kila mwanamke aliye na Hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu hibomoa kwa mikono yake mwenyewe”
Kuna mithali isemayo “MAJUTO MJUKUU”, ni kawaida kwa wanandoa kuangalia na kulaumiana juu ya matatizo yanayojitokeza, badala ya kutafakari chanzo cha matatizo. Matatizo mengi ya ndoa yanatokana na wanandoa kutokuwa na elimu ya ndoa na kutofuata ushauri wa Mungu aliyeanzisha Ndoa… endelea kusoma

a.gif SMS boomba za mapenzi

Najiuliza kila leo hivi ni mimi tu kimeo katika dunia hii ya leo maana kila leo nayempata huishia kunipa ahadi kila leo, mpenzi kila siku waniaidi mara nitakupa leo mara kabla ya machweo, hivi ni lini utanipa jibu la uhakika nakunipa mapenzi ya uhakika nipate farijika? Nakupenda mpenzi… endelea kusoma

a.gif SMS tamu za kimahaba

Furaha ni kawaida yangu, kununa si busara kwangu, kuishi nawewe vizuri ni sehemu ya Maisha yangu, kukusalimia ni hulka ya Moyo wangu, Uhali gani mpenzi?.. endelea kusoma

a.gif Mambo 10 ambayo wanawake wamewazidi wanaume

1. Wana Nguo Nyingi KulikoWanaume.
2. Wanafahamu Nani Ni Baba HalisiWa Watoto Wao… endelea kusoma

a.gif Ushauri kwa vijana wenye miaka 22 nakuendelea

Ikiwa wewe ni kijana na Una umri wa kuanzia miaka 22 na Kuendelea
Soma hapa ujifunze maisha ya hekima na namna bora ya kuishi na kufanikiwa ungali kijana.. endelea kusoma

a.gif Marafiki zangu wa Facebook ujumbe wangu huu

RAFIKI ZANGU WA FACEBOOK, LEO NATAKA TUKUMBUSHANE NENO DOGO TU, LAKINI NI LA MUHIMU SANA:
Fuatana nami;.. endelea kusoma

a.gif MAKUNDI MANNE YA WATU DUNIANI

Habari tazama leo ni siku nyingine Mungu katenda miujiza kwako wakati wengine wamekufa usiku wewe umeamka tena, hebu sema asante kwa hilo, tunaendele na mada zetu na leo tutaangalia makundi manne ya watu katika dunia… endelea kusoma

afya-mapishi-na-lishe.png

.

familia-mapenzi-na-mahusiano.png
UJUMBE-KUOMNBA-KUKUTANA-NA-NDUGU.JPG
elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.