Mambo 5 ya muhimu kuzingatia kuhusu mahali unapotaka kuweka mizinga ya nyuki

By, Melkisedeck Shine.

Ukitaka kujua kuwa eneo unalotaka kuweka mizinga ya nyuki ni sahihi unatakiwa kuzingatia yafuatayo:

1. Haishauriwi kuweka mzinga shambani au karibu na shamba. Unatakiwa uweke umbali wa mita 150-200 kutoka kwenye mazao au nyumbani. Hii ni Kulingana na hali ya kujilinda ya nyuki wa Afrika

2. Mzinga ni lazima uwekwe sehemu ambayo haitasababisha upotevu wa nyuki wanaporudi kutoka nje ya mzinga. Mfano wasiingie kwenye kundi lisilokuwa lao.

3. Mizinga inatakiwa isiwekwe mbalimbali sana ili kuepusha usumbufu wa kutembea mbali kwa mfugaji wakati anapokagua.

Sifa ya eneo la kuweka mizinga
β€’ Iwe Kimya na mbali ya jumuia kama vile hospitali, shule, na viwanja vya michezo vile vile isiwe karibu na maeneo ya biashara au viwanda.
β€’ Karibu na maji masafi-kandokando ya mto, mabwawa ya samaki, mabeseni ya maji au sehemu ya matone.
β€’ Sehemu ya kuweka mizinga Iwe ni karibu na chakula cha nyukimimea inayochanua, miparachichi, nazi, euculptus, migunga n.k
β€’ Iwe sehemu ambayo ni kavu na isiwe sehemu ya tindiga kwani unyevu unyevu husababisha ugonjwa wa ukungu (magonjwa ya fangasi yaani fungal disease) na pia huzuia utengenezaji mzuri wa asali.
β€’ Mahali pa mizinga pawe mbali na watu waharibifu na iliyojificha kuepuka waharibifu.
β€’ Sehemu ya kuweka mizinga ni lazima iwe inafikika kirahisi kwa kipindi chote cha mwaka ili iwe rahisi kuhamisha nyuki pale inapohitajika.
β€’ Panatakiwa pawe kivuli cha kutosha hasa wakati wa mchana jua linapokuwa kali, na kusiwe na upepo mkali.

4. Mizinga ya nyuki Iwe mbali na mashamba, ambapo dawa za kuulia wadudu zinatumika.

5. Vichaka au wigo unaotenganisha mizinga na kuzuia wavamizi ni muhimu ili kupunguza ukali wa nyuki.

USIKOSE HIIπŸ‘‰ TIBA KWA KUTUMIA MAJI

[fumbo kwako] πŸ‘‰Imekuaje hawa watoto wakapungua?

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Mambo 5 ya muhimu kuzingatia kuhusu mahali unapotaka kuweka mizinga ya nyuki;

a.gif Mambo muhimu ya kuzingatia kwenye ufugaji wa nyuki wa asali

Unapohitaji unahitaji kufuga nyuki ni lazima uwe na uelewa wa mzunguko wa maisha ya nyuki. Unapoanza ni lazima uulize mtaalamu wa nyuki, wafugaji wenzako ambao wana uzoefu wa kutosha, au kujiunga katika kikundi cha ufugaji ili apate ufahamu zaidi juu ya ufugaji wa nyuki… endelea kusoma

a.gif Mambo makubwa yanayosababisha kulazimika kulima au kutifua udongo

Kutifua udongo ni jambo la muhimu sana ili kuufanya udongo kuwa bora… endelea kusoma

a.gif Aina kuu ya mizinga bora ya nyuki kwa ajili ya kupata asali nyingi

Hii ni aina ya mizinga inayotumika sana na wengi. Gharama yake ni ndogo kiasi kulinganisha na mingine. Ni aina nzuri sana kwa mtu anaeanza ufugaji wa nyuki kwa kuwa ni wa gharama nafuu. Mfugaji wa nyuki anaweza kutengeneza mzinga Yya aina hii mwenyewe kama ana utaalamu wa useremala… endelea kusoma

KADI-SHUKRANI-MZAZI.JPG

a.gif Jinsi ya kufanya nyuki waingie kwenye mzinga mpya

Ukitaka kuwavutia na kuingiza nyiki kwenye mzinga unatakiwa kufanya yafuatayo;.. endelea kusoma

a.gif Mbinu za kuzuia magonjwa kwa kuku

Mbinu hizo ni hizi zifuatazo;.. endelea kusoma

a.gif Kampeni ya usafi Binafsi

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.
Lengo la kampeni Hii ni kuhamasisha watu kudumisha usafi wao binafsi kwa afya zao na kwa maendeleo yao.
Kampeni hii inaamini kuwa usafi wa mtu binafsi unamkinga na matatizo yatokanayo na uchafu kijamii na kiafya kwa mfano maradhi ambayo yanaweza kumzuia kuendelea na kazi zake za kawaida na kukua kimaendeleo kama mtu binafsi… endelea kusoma

a.gif Kampeni ya Kudumisha Amani na Upendo

Kampeni hii ilianzishwa Rasmi Mwaka 2014 na Melkisedeck Leon Shine.
Lengo la kampeni Hii ni kudumisha Amani na Upendo bila kuangalia tofauti zetu.
Kampeni hii inaamini kuwa katika upendo kuna amani.
Kampeni hii inafundisha kwamba upendo wa kweli ni wa kuwafanyia wengine vile ungependa kufanyiwa nao. Kila mtu amfanyie mwenzake vile anavyopenda afanyiwe… endelea kusoma

FURSA.PNG

Fursa Ya Kazi Na Ajira Yenye Malipo Mazuri

Au soma zaidi hapa

.

Marafiki-wa-enzi.GIF
UJUMBE-KUOMNBA-KUKUTANA-NA-NDUGU.JPG

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.