Mambo Ya Kuzingatia Kuongeza Utagaji Wa Kuku

By, Melkisedeck Shine.

Inafahamika kuku kutaga mayai mengi hutokana na aina ya mbegu ya kuku, ila jua kwamba hata aina ya mbegu ya kuku yenye sifa ya kutaga mayai mengi kama haitapewa matunzo mazuri  basi sifa yake ya utagaji itapotea.
Kwa kawaida Tetea anatumia muda wa masaa 24 - 27 (siku moja) kutengeneza yai. Hakuna njia ya kupunguza muda huu (yaani atengeneze mayai miwili katika siku moja). Hiyo ndio asili yake. Njia Nzuri ya kumfanya kuku atage muda mrefu ni kumfanya awe na furaha na afya.
Njia za kuwafanya kuku wawe na furaha na afya:

1. Wape chakula bora chenye virutubisho vya kutosha. Usichakachue chakula chao hawatataga.

2. Viota vyao viwe safi. Safisha viota vyao mara kwa mara ili watage sehemu safi.

3. Wawe na sehemu ya wazi ya kuzunguka zunguka na kuparua parua.

4. Wawekee calcium ya kutosha kwenye chakula chao ili mayai wanayotaga yawe na gamba gumu.

5. Wachunguze mara kwa mara
kama wana dalili za kuumwa, na endapo dalili zipo watibu mara moja.

6. Wapatie maji safi kila siku. Pia safisha vyombo vyao kwa sabuni kila siku.

7. Hakikisha banda lao ni safi muda wote ili kusiwe na wadudu kama viroboto, chawa na papasi. Wadudu hawa huwasumbua kuku na kuwafanya wapunguze kutaga.

8. Hakikisha kuku hawapati msongo/stress, mfano kusiwe na wanyama wa kuwatisha wanaopita au kuingia bandani kwao.

9. Chagua aina ya kuku wanaotaga mayai mengi.

10. Umri wa kuku. Kuku wenye umri wa miezi 6 - 18 wanataga sana. Wakiwa na miezi 19 - 24 wananyonyoka manyoya (Annual Molt), hivyo hupunguza kutaga, na wakianza kutaga tena, wanataga mayai makubwa na machache kuliko mwanzo.

11. Wasihamishwe hamishwe banda. Kuku hutaga vizuri zaidi wakiwa kwenye mazingira waliyoyazoea.

12. Walishe mboga za majani za kutosha.
Kumbuka: Kuku wenye furaha na afya ndio watakaotaga sana kwenye maisha yao.
Note: Wakati mwingine inadhaniwa kwamba Jogoo anaweza kumsaidia Tetea kutaga mayai mengi. Jogoo hawezi kuongeza utagwaji wa mayai, lakini anahitajika kuyarutubisha mayai (kuyafanya yawe na mbegu). Kama kuku wako anataga mayai machache, kuongeza Jogoo hakutamfanya Tetea atage mayai mengi.MPENZI-MLO-MWEMA-34NG.JPG

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Mambo Ya Kuzingatia Kuongeza Utagaji Wa Kuku;

a.gif Matumizi ya mihogo kama dawa ya kuzuia wadudu kwenye mimea

Muhogo Inazuia Minyoo na vidukari… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kutumia mashonanguo kama dawa ya kuzuia wadudu kwenye mimea

MASHONANGUO.jpg

Mashonanguo kwa kiingereza ni Blackjack au kwa kisayansi yanajulikana kama (Bidens
pilosa)
Mashona nguo yanazuia wadudukama vile Vidukari, Siafu, bungo, katapila, chenene (crickets), nyenyere, siafu na inzi weupe… endelea kusoma

a.gif Canibalism Kwa Kuku Au Tatizo La Kudonoana

"Cannibalism,"
Kudonoana kwa kuku ni tatizo linalo wa sumbua wengi, ni moja ya athari ya lishe duni. Ni kisema lishe duni na maanisha chakula wanacho kula kukosa vurutubisho muhimu vya madini au kuku kutokula chakula cha kutosha… endelea kusoma

[Kitendawili Kwako] 👉Kimwiinamishacho mfalme

[Fumbo Kwako] 👉Je, glass ina Maji kiasi gani?

SALAMU-JIONI98HBS.JPG

a.gif Mambo 8 ya kuzingatia kabla ya kuleta mifugo (kuku, ng'ombe,mbuzi n.k) wapya bandani

Mambo hayo ni haya yafuatayo;
1. Hakikisha unaondoa matandazo yote ndani ya nyumba,
2. Ondoa vyombo vya kulishia na kunyweshea… endelea kusoma

a.gif Jinsi vitunguu swaumu vinavyosaidia kuzuia wadudu shambani

Vitungu saumu vina manufaa sana katika kukabiliana na aina mbalimbali za wadudu waharibifu na baadhi ya magonjwa kutokana na kuwa na harufu kali inayosaidia kuwafukuza wadudu kama vidukari, bungo na hata panya… endelea kusoma

a.gif Kampeni ya Kudumisha Umoja Wa Imani na Amani kwa watu wote

Kampeni hii ilianzishwa Rasmi Tarehe 15/05/2012 na Melkisedeck Leon Shine.
Lengo la kampeni Hii ni kudumisha Amani na Umoja bila kuangalia tofauti za imani zetu za kidini… endelea kusoma

a.gif Mambo makubwa yanayosababisha kulazimika kulima au kutifua udongo

Kutifua udongo ni jambo la muhimu sana ili kuufanya udongo kuwa bora… endelea kusoma

[Picha Nzuri] 👉Huyu ndiyo fundi wa admini

[Msemo wa Leo] 👉Kutokuwa na kitu

[Jarida la Bure] 👉Kijitabu cha Picha Kali

FURSA.PNG

Fursa Ya Kazi Na Ajira Yenye Malipo Mazuri

Au soma zaidi hapa

.

MPENZI-MLO-MWEMA-34NG.JPG
NIMEKUMISI-MPENZI086H.JPG

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.