Jinsi ya kumlisha n'gombe anayekamuliwa atoe maziwa mengi

By, Melkisedeck Shine.

Ng’ombe wa maziwa wanahitaji virutubisho zaidi ili kuweza kuzalisha maziwa kwa wingi hasa katika kipindi cha miezi 3-4 ya mwanzo baada ya kuzaa, wakati ambao uzalishaji wa maziwa unakuwa juu.

Malisho ya ng'ombe wa maziwa ni lazima yawe na uwiano sahihi wa viungo. Mifugo inahitaji chakula kitakachowapa nguvu, protini, madini, na vitamin ili kujenga miili yao, kuzalisha maziwa, na kuzaliana.

Kulisha ng’ombe wa maziwa kwa kutumia aina yoyote ya malisho haitoshi kukuhakikishia ng’ombe anakuwa na afya nzuri na kutoa maziwa ya kutosha. Kama ilivyo kwa mifugo mingine kama kuku na hata binadamu, ng’ombe anahitaji
mlo bora yaani kamili.

Vyakula vinavyohitajika kwa ng'ombe wa maziwa

Malisho ya kijani (Majani)

Huu ni mlo mkuu kwa ng'ombe wa maziwa. Mlo ni muhimu na wenye virutubisho. Lakini malisho bora ya kijani ni yale yanayoweza kumpatia ng’ombe wa maziwa virutubisho muhimu vinavyohitajika.

Malisho ya kijani yanatakiwa yawe ya kijani kibichi na machanga, hii ina maana kuwa, majani ya malisho ni lazima yakatwe na kuhifadhiwa yakiwa bado machanga na kabla ya kuchanua. Hii ina maana kuwa mimea ambayo imepoteza rangi yake halisi ya kijani inaweza tu kuwasaidia mifugo kuishi lakini haina virutubisho muhimu vya kuwapa mifugo nguvu, madini, protini na haiwezi kusaidia katika uzalishaji wa maziwa.

Malisho yenye viwango vya chini vya virutubisho yanatakiwa yaongezewe kwa chakula cha ziada chenye virutubisho vya kutosha kitakachoziba pengo la virutubisho vilivyokosekana.

Vyakula vya kutia nguvu

Kwa kawaida aina zote za majani ni chanzo kizuri cha vyakula vya kutia nguvu kwa mifugo, kama tuu tu yatalishwa yakiwa bado machanga.

Mfano wa Majani yaliyo maarufu kwa malisho ni matete, ukoka, majani ya tembo, seteria na Guatemala. Majani ya mahindi au mtama ni chakula kizuri sana kwa kuwapa nguvu mifugo.

Vyakula vingine vinaweza kutokana na aina zote za nafaka, punje za ngano, au molasesi.

Vyakula hivi vya kutia nguvu vinatakiwa vilishwe kwa kiasi kidogo.

Vyakula vya Protini

Mimea michanga ina kiasi kikubwa cha protini kuliko mimea iliyokomaa. Mahindi machanga pamoja na majani ya viazi vitamu ni mahususi kwa protini.

Mikunde ina protini nyingi zaidi kuliko nyasi. Mfano, mabaki ya majani ya maharage, njegere, desmodium na lusina. Majani yanayotokana na mimea kama lusina, calliandra au sesbania ina kiwango kikubwa cha protini pia.

Aina nyingine ya vyakula vyenye protini ni mashudu ya pamba, mashudu yaalizeti na soya.

Ng’ombe wa maziwa wasilishwe kwa kutumia aina zote za jamii ya mikunde kwa zaidi ya asilimia 30 ya uwiano wa mchanganyiko wa malisho ili kuepuka matatizo ya kiafya.

Madini

Ng'ombe wa maziwa wanahitaji madini ya ziada. Madini Ni lazima yapatikane muda wote, mfano kama jiwe la chumvi au kama chumvi ya unga ya kuweka kwenye (chakula) pumba.

Wanyama wanaokuwa, wenye mimba, na ng’ombe anaenyonyesha wanahitaji kiasi kikubwa cha madini, mfano calcium na phosphorous kwa kuwa madini mengi yanatoka kwenye maziwa.

Madini yanaweza kupatikana katika Mimea ya jamii ya mikunde na mengineyo isipokuwa nyasi. Mimea hii inatoa kiasi kikubwa cha calcium na madini mengineyo.

Chakula cha ziada (mf. Pumba)

Ng'ombe wa maziwa anapewa cha kula cha ziada mfano pumba. Pumba inahitajika kwa ng'ombe lakini kwa kiasi kidogo. Pumba aina ya Dairy meal ina kiwango kikubwa sana cha madini. Lakini ina madhara kwa mifugo endapo wanyama watalishwa kwa kiwango kikubwa.

Malisho yanayotokana na majani au nyasi kavu ni lazima yabakie kuwa chakula kikuu kwa mifugo. Haishauriwi kulisha zaidi ya kilo 6 za pumba kwa siku kwa ng’ombe mwenye kilo 450.

Ni lazima wapewe kwa kiwango kidogo sana, ambacho si zaidi ya Kilo 2 kwa mara moja na kichanganywe na majani. Kuongeza kiwango cha pumba kabla na wakati wa kunyonyesha/kukamuliwa, kisizidi kiasi cha kilo 2 kwa wiki ili tumbo la mnyama lizoee.UJUMBE-KUOMNBA-KUKUTANA-NA-NDUGU.JPG

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Jinsi ya kumlisha n'gombe anayekamuliwa atoe maziwa mengi;

a.gif Jinsi vitunguu swaumu vinavyosaidia kuzuia wadudu shambani

Vitungu saumu vina manufaa sana katika kukabiliana na aina mbalimbali za wadudu waharibifu na baadhi ya magonjwa kutokana na kuwa na harufu kali inayosaidia kuwafukuza wadudu kama vidukari, bungo na hata panya… endelea kusoma

a.gif Ugonjwa wa tetanasi au pepopunda unaoathiri sana punda na binadamu

Huu ni ugonjwa hatari sana kwa maisha ya binadamu. Kinyesi cha punda kinabeba vimelea vijulikanavyo kama clostindium tetanii vinavyosababisha ugonjwa wa tetanasi… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kutengeneza mbolea ya mboji kitaalamu na kwa urahisi

Mbolea ya mboji hutokana na mabaki ya majani na miti. Majani na miti yanapooza hugeuka na kutengeneza virutubisho ambavyo husaidia kurutubisha udongo na kupunguza gharama… endelea kusoma

a.gif Namna ya kufanya Ukaguzi wa mara kwa mara wa banda la kuku kuzuia magonjwa

Ukaguzi wa Kila siku
• Hakikisha unasafisha vyombo vya kulishia na kunyweshea pamoja na viota.
• Ondoa kinyesi kwa kuku.
• Waangalie kuku wako kwa makini ili kujua afya na maendeleo yao. Yaani ili kutambua kama kuna mwenye ugonjwa.. endelea kusoma

[Kitendawili Kwako] 👉Nimekwenda lakini sikufikia mwisho wake

[Fumbo Kwako] 👉Je, hawa walizikwa wapi?

[Video Nzuri] 👉Huu ukataji wa ugali ni noma

nn.gif

a.gif Ugonjwa wa tetanasi au pepopunda unaoathiri sana punda na binadamu

Huu ni ugonjwa hatari sana kwa maisha ya binadamu. Kinyesi cha punda kinabeba vimelea vijulikanavyo kama clostindium tetanii vinavyosababisha ugonjwa wa tetanasi… endelea kusoma

a.gif Kampeni ya utunzaji wa wanyama pori

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.
Lengo la kampeni Hii ni kuhamasisha watu kutunza wanyama pori kwa manufaa yao ya sasa na kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Kampeni hii inaamini kuwa wanyama pori wakitunzwa vizuri wanaweza kuwa msaada kijamii, kiuchumi na kimazingira kwa kizazi hiki na kizazi kijacho… endelea kusoma

a.gif Kampeni Ya Wafanye Watabasamu

Let Them Smile Campaign au Kampeni ya Wafanye nao Watabasamu ni kampeni endelevu ya kuhamasisha ushirikiano, umoja na kusaidiana katika jamii kwa watu wa matabaka yote.
Kampeni hii ina lengo la kuamsha na kueneza furaha itokanayo na umoja na mshikamano kwenye jamii kwa njia ya kusaidiana na kushirikiana kimawazo, kwa matendo na kifedha. Ni kweli kwamba furaha ya kweli haiji kwa kujifurahisha mwenyewe bali kwa kufurahishwa… endelea kusoma

a.gif Kampeni ya kutetea watoto yatima

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.
Lengo la kampeni hii ni kuhamasisha watu wote kusaidia kulea na kuwakuza watoto yatima kwa maendeleo bora ya kimwili, kiroho na kijamii kwa manufaa ya watoto wenyewe na kwa manufaa ya watu wote kwa sasa na kwa baadae.
Kampeni hii inaamini kuwa watoto yatima kama walivyo watoto wengine nao ni kama mali ambayo inawekezwa sasa kwa matumizi na maendeleo ya baadae. Japokuwa hawana (wazazi) watu/mtu rasmi wa kuwatunza haimaanishi kuwa hawawezi kuwa watu wa maana baadae… endelea kusoma

[Msemo wa Leo] 👉Kufanya Biashara vizuri

FURSA.PNG

Fursa Ya Kazi Na Ajira Yenye Malipo Mazuri

Au soma zaidi hapa

.

UJUMBE-WA-MSAMAHA-KWA-NDUGU.JPG
UJUMBE-MSAMAHA-35JHF32.JPG

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.