Canibalism Kwa Kuku Au Tatizo La Kudonoana

Mpendwa Msomaji, baada ya kukuandalia makala inayopendwa kuhusu; Namna ya kukabiliana na Magonjwa ya kuku, sasa nimekuandalia makala hii kuhusu;

Canibalism Kwa Kuku Au Tatizo La Kudonoana.

Canibalism Kwa Kuku Au Tatizo La Kudonoana

By, Melkisedeck Shine.

CANNIBALISM KWA KUKU NI NINI?

"Cannibalism,"

Kudonoana kwa kuku ni tatizo linalo wa sumbua wengi, ni moja ya athari ya lishe duni. Ni kisema lishe duni na maanisha chakula wanacho kula kukosa vurutubisho muhimu vya madini au kuku kutokula chakula cha kutosha.

#Hizi ni moja ya sababu zinazo pelekea kuku kudonoana.

1.Kuku kukaa wengi kwenye eneo dogo

2. Tabia yao

3.Ubaguzi wa rangi

Hii Mara nyingi hutokea kwa kuku weusi ukiwachanganya na kuku mweupe au rangi ingine tofauti, kuku weusi Mara nyingi huwa ni wakali sana Kwahiyo ukiona kuku bandani kwako kadonolewa chunguza kwa makini chanzo ninini! Kama ni ubaguzi wa rangi unaweza watenga hao weusi.

4. Kuku kutokupata chakula cha kutosha

5.Upungufu wa madini ( protini)

6. Kukosa kitu walicho kizoea au kuboreka

Kwa mfano kuku ukiwazoesha kuwa changanyia Damu kwenye chakula , siku utakapo punguza kipimo au kuacha kabisa kuwa changanyia damu ambayo umewazoesha kuwa changanyia lazima watadonoana.

Kuku ukiwa zoesha kuwa fungia mchicha hasa wale kuanzia mwezi mmoja hadi wa miezi 4 siku utakapo acha kuwafungia mchicha inaweza sababisha wakadonoana.

Kuku hupenda kuparuaparua na kuzunguka zunguka. Wakikosa nafasi na vitu vya kudonoa donoa huanza kudonoana wenyewe kwa wenyewe.

7. Mwanga mkali

8. Msongo

Banda lenye joto sana na lisilo pitisha hewa vizuri huwapatia msongo/stress kuku, na kuku huweza kuanza kudonoana.

9. Uhaba wa vyombo bandani๐Ÿ‘‡

Hii hutokana na kuwa na kuku wengi halafu vyombo vichache vya chakula , Kwahiyo wakati wa kula lazima watagombania na kudonoana

Kuku wa umri tofauti kuwekwa kwenye banda moja

#Tiba Kinga

#Tiba___ Tumia Protini (Amino Acid) stahiki kulingana na tatizo.

Mfano: (methionine , lysine nk)

#Kinga

_Changanya Proteni kiwango kizuri kwenye chakula cha kuku,chakula cha kuku kijumuishe virutubisho vyenye asili ya wanyama ambavyo ni chanzo kizuri cha Proteni

_Hakikisha kuku wako wanakaa kwenye eneo la kutosha . hii inategemea aina ya kuku na umri wake.

Usisahau kushare makala hii uliyoisoma kuhusu; Canibalism Kwa Kuku Au Tatizo La Kudonoana. Share Facebook, Twitter bila kusahau WhatsApp.

Makala hii kuhusu, Canibalism Kwa Kuku Au Tatizo La Kudonoana, imeonekana kupendwa na wasomaji wengi. Makala nyingine zinazopendwa ni kama hizi zifuatazo;

โ€ข Mambo makubwa yanayosababisha kulazimika kulima au kutifua udongo, endelea kusoma...

โ€ข Jinsi ya kumlisha n'gombe anayekamuliwa atoe maziwa mengi, endelea kusoma...

โ€ข Matumizi ya mihogo kama dawa ya kuzuia wadudu kwenye mimea, endelea kusoma...

โ€ข Mambo Ya Kuzingatia Kuongeza Utagaji Wa Kuku, endelea kusoma...

โ€ข Matumizi ya mihogo kama dawa ya kuzuia wadudu kwenye mimea, endelea kusoma...

โ€ข Jinsi ya kutumia mashonanguo kama dawa ya kuzuia wadudu kwenye mimea, endelea kusoma...

โ€ข Jinsi ya kuandaa mbangimwitu kama Dawa ya magonjwa na ya kuulia wadudu shambani, endelea kusoma...

โ€ข Faida ya kupanda maharagwe katikati ya kabichi, endelea kusoma...

โ€ข Jinsi wigo wa mimea kwenye shamba unavyoweza kukinga mazao yako na wadudu waharibifu, endelea kusoma...

โ€ข Mambo manne muhimu ya kuzingatia kukabiliana na wadudu shambani, endelea kusoma...

Unaweza kusoma makala mpya nzuri kila unapotembelea website hii wakati wowote. Baada ya kusoma makala hii kuhusu; Canibalism Kwa Kuku Au Tatizo La Kudonoana, sasa endelea kusoma makala hizi nyingine nzuri nilizokuandalia;

FURSA..! Kuna nafasi za kazi 100.

Au soma zaidi hapa

.

NIMEKUMISI-MPENZI086H.JPG
UJUMBE-MSAMAHA-35JHF32.JPG