Mafundisho ya Dini

πŸ‘‰Mambo yanayomzuia mtu kuishi maisha mema ni yapi?

Mambo hayo ni;
1. Dhambi
2. Vilema
3. Vishawishi

πŸ‘‰Vilema ni nini?

Vilema ni mazoea ya kutenda mambo mabaya na kuacha kutenda mambo mema. (Gal 5:19-21)

πŸ‘‰Vichwa au Mizizi ya dhambi ni ipi?

1. Majivuno
2. Uchoyo
3. Wivu
4. Hasira
5. Tamaa mbaya
6. Ulafi
7. Uvivu au uzembe

πŸ‘‰Majivuno ni nini?

Majivuno ni kujiona mkubwa nafsini mwako au mbele za watu.

πŸ‘‰Ni fadhila gani inayoondoa majivuno?

Fadhila inayoondoa majivuno ni fadhila ya Unyenyekevu

πŸ‘‰Ubahili ni nini?

Ubahili ni kupenda mno mali za dunia na kumsahau Mungu

πŸ‘‰Ni fadhila gani inayoondoa ubahili?

Fadhila inayoondoa ubahili ni ukarimu

πŸ‘‰Uchafu ni nini?

Uchafu ni kufanya mawazo, tamaa, maneno au matendo kwa kuvunja amri ya sita au ya tisa ya Mungu

πŸ‘‰Ni fadhila ipi inayoondoa uchafu?

Fadhila inayoondoa uchafu ni fadhila ya Usafi wa Moyo

πŸ‘‰Wivu ni nini?

Wivu ni kuwaonea watu uchungu kwa heri walizonazo au kufurahia misiba yao

πŸ‘‰Ni fadhila ipi yenye kuondoa wivu?

Fadhila inayoondoa wivu ni fadhila ya wema

πŸ‘‰Ulafi ni nini?

Ulafi ni kupenda kula au kunywa bila kiasi

πŸ‘‰Ni fadhila gani inayoondoa ulafi?

Fadhila inayoondoa ulafi ni kadiri na kiasi

πŸ‘‰Hasira ni nini?

Hasira ni kukasirika bure kuonea na kulipiza kisasi

πŸ‘‰Ni fadhila ipi yenye kuondoa hasira?

Fadhila inayoondoa hasira ni fadhila ya upole

πŸ‘‰Uvivu ni nini?

Uvivu ni uregevu wa moyo unaotufanya tukose juhudi

πŸ‘‰Fadhila inayoondoa uvivu ni ipi?

Fadhila inayoondoa uvivu ni utendaji

.

.

Makala

Mafundisho

.

.

.

IMG_20181021_134941.jpg

Kama Una mashaka na Imani na mafundisho ya Kanisa Katoliki soma hapa>>

Website hii inaletwa kwako na Melkisedeck Leon Shine.

Naomba utafakari kuhusu; Jambo la muhimu zaidi Duniani. Mungu akubariki sana. Tuombeane…!