Mafundisho ya Dini

๐Ÿ‘‰Nani ameumba vitu vyote?

Mungu ameumba vitu vyote

๐Ÿ‘‰Mungu ni Muumba vyote maana yake ni nini?

Mungu ni Muumba vyote Maana yake amefanya vitu vyote kwa kutaka tu pasipo kutumia chochote. (2Wamakabayo 7:28, Yoh 1:3)

๐Ÿ‘‰Kwanza Mungu aliumba nini?

Kwanza Mungu aliumba Malaika (Kol 1:16)

๐Ÿ‘‰Kisha kuumba Malaika Mungu aliumba nini?

Kisha kuumba Malaika Mungu aliumba Mbingu na dunia, na viumbe vingine vingi vyenye kuonekana mimea na watu. (Mwanzo 1;31)

๐Ÿ‘‰Kwa nini Mungu aliumba ulimwengu?

Mungu aliumba ulimwengu ili adhihirishe utukufu wake na kutushirikisha wema, ukweli na uzuri wake

๐Ÿ‘‰Mungu aliumbaje ulimwengu?

Mungu aliumba ulimwengu kwa uwezo wake kwa kusema na bila kutumia kitu chochote. (Mwa 1:1)

๐Ÿ‘‰Mungu alisema nini alipotaka kumuumba mtu?

Mungu alipotaka kumwumba mtu alisema; "Tumfanye mtu kwa mfano wetu na kwa sura yetu" (Mwa 1:26-27)

๐Ÿ‘‰Tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu maana yake ni nini?

Tumeumbwa kwa mfano na sura ya Mungu maana yake tuna roho zenye akili na utashi yaani uwezo wa kutofautisha mema namabaya, na zitakazoishi milele.

๐Ÿ‘‰Watu wa kwanza kuumbwa na Mungu ni akina nani?

Watu wa kwanza kuumbwa na Mungu ni Adamu na Hawa (Eva). (Mwa 1:27)

๐Ÿ‘‰Mungu alimwumbaje Adamu?

Mungu aliufanya mwili wa Adamu kwa udongo, akaupulizia roho yenye uhai. (Mwa 2:7)

๐Ÿ‘‰Mungu alimwumbaje Eva (Hawa)?

Mungu alimwumba Eva kwa mfupa wa ubavu kutoka kwa Adamu, akamtia roho. (Mwa 2:21-24)

๐Ÿ‘‰Kwa nini Mungu alituumba? Kwa nini Mungu aliumba mtu?

Mungu ametuumba tumjue, tumpende, tumtumikie tulipo wazima hapa duniani, hata mwisho tukisha kufa tuende kwake Mbinguni katika katika makao ya raha milele. (Mwa 2:7; Mt. 19:17; Yoh 14:1-3 na Yoh 17:24)

๐Ÿ‘‰Asili ya uhai wote ni nani?

Asili ya uhai wote ni Mwenyezi Mungu. โ€œHapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchiโ€ (Mwa 1:1).

๐Ÿ‘‰Mungu aliumbaje vyote?

Mungu aliumba vyote kwa kutaka tu, bila ya kutumia chochote. โ€œNakusihi, mwanangu, inua macho yako utazame mbingu na nchi, ukaone vitu vyote vilivyomo; fahamu kwamba Mungu hakuviumba kwa vitu vilivyokuwapo. Na ndivyo alivyofanya wanadamu piaโ€ (2Mak 7:28). Umuambie: โ€œNajua ya kuwa waweza kufanya mambo yote, na ya kuwa makusudi yako hayawezi kuzuilikaโ€ (Ayu 42:2).

๐Ÿ‘‰Kwa nini Mungu aliumba vyote?

Mungu aliumba vyote bila ya kulazimika, kusudi tu adhihirishe na kushirikisha utukufu wake. โ€œMbingu zauhubiri utukufu wa Mungu, na anga laitangaza kazi ya mikono yakeโ€ (Zab 19:1). โ€œKwa kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Aminaโ€ (Rom 11:36).

๐Ÿ‘‰Je, Mungu anazidi kushughulikia viumbe vyake?

Ndiyo, Mungu anazidi kushughulikia viumbe vyake, akividumisha na kuviongoza vyote vifikie lengo alilovipangia. โ€œNdani yake yeye tunaishi, tunakwenda na kuwa na uhai wetuโ€ (Mdo. 17:28). Tunamtegemea pande zote: angetuacha kidogo tungetoweka mara. Yesu alipolaumiwa kwa kuponya watu siku ya pumziko, alijitetea kwamba, โ€œBaba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kaziโ€ (Yoh. 5:17). โ€œYeye hujishughulisha sana kwa mambo yenuโ€ (1Pet. 5:7).

๐Ÿ‘‰Ikiwa Mungu anatushughulikia, tunapaswa kufanya nini?

Ikiwa Mungu anatushughulikia, tunapaswa kujiachilia mikononi mwake kwa moyo wa kitoto, tukiwajibika bila ya mahangaiko yanayowapata watu wasiomjua. โ€œWaangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je, si bora kupita hao?โ€ (Math 6:26). โ€œNawe una nini usichokipokea?โ€ (1Kor 4:7). โ€œNimrudishie Bwana nini kwa ukarimu wake wote alionitendea?โ€ (Zab 116:12).

๐Ÿ‘‰Tunaanzaje kumjua Mungu?

Tunaanza kumjua Mungu kwa kuzingatia viumbe vyake, hasa dhamiri yetu. โ€œKwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wakeโ€ (Rom 1:20).

๐Ÿ‘‰Viumbe vyenye hiari ni vipi?

Malaika na watu ndio viumbe pekee vyenye hiari ya kuchagua wenyewe wachangie mpango wa Mungu au la. โ€œNazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi, chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako; kumpenda Bwana, Mungu wako, kuitii sauti yake, na kushikamana naye; kwani hiyo ndiyo uzima wakoโ€ (Kumb 30:19-20).

๐Ÿ‘‰Malaika na watu wanaweza kuchagua hata nini?

Malaika na watu wanaweza kuchagua hata wawe wema au wabaya milele. โ€œKulikuwa na vita mbinguni: Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguniโ€ (Ufu 12:7-8). Chaguo letu binadamu linafanyika siku kwa siku kwa kuchukua misimamo mizuri au mipotovu kuhusu dini na maadili. โ€œMwayachunguza Maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia. Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzimaโ€ (Yoh 5:39-40).

๐Ÿ‘‰Je, kati ya viumbe mbalimbali Mungu ameweka mpango wowote?

Ndiyo, kati ya viumbe mbalimbali Mungu ameweka mpango: alitaka malaika wasioonekana wamtumikie kwa kutusaidia sisi watu, na vile vinavyoonekana tuvitumie kwa uadilifu ili kwa njia yetu vimtukuze yeye. โ€œAtakuagizia malaika zake wakulinde katika njia zako zoteโ€ (Zab 91:11). โ€œKwa Hekima yako ulimwumba mwanadamu, ili avitawale viumbe vilivyoumbwa nawe, na kumiliki ulimwengu katika utakatifu na kwa hakiโ€ (Hek 9:2-3).

๐Ÿ‘‰Malaika wakoje?

Malaika ni roho tupu walioumbwa na Mungu ili wamtukuze milele, wamlinde kila mtu na kumtumikia Bwana Yesu katika kutuokoa. โ€œAngalieni, msidharau mmojawapo wadogo hawa, kwa maana nawaambia ya kwamba malaika zao mbinguni sikuzote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguniโ€ (Math 18:10).

๐Ÿ‘‰Sisi binadamu tukoje?

Sisi binadamu ni umoja wa mambo mawili: roho iliyoumbwa na Mungu moja kwa moja, na mwili ulioumbwa naye kwa njia ya wazazi. Maumbile hayo yanatakiwa kukamilika kwa kupokea na kutimiza upendo wa Mungu aliyesema, โ€œโ€™Na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchiโ€™. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumbaโ€ (Mwa 1:26-27).

๐Ÿ‘‰Kwa nini Yesu alishawishiwa/alijaribiwa na Shetani?

Yesu alishawishiwa na Shetani kwa kuwa ni mtu kweli, akamshinda kwa niaba ya watu wote, akituonyesha namna ya kumtii Mungu moja kwa moja, โ€œhata mauti, naam, mauti ya msalabaโ€ (Fil 2:8). โ€œKwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye hakiโ€ (Rom 5:19).

.

.

Makala

Tafakari

Mafundisho

.

.

.

IMG_20180108_172040.jpg

Kama Una mashaka na Imani na mafundisho ya Kanisa Katoliki soma hapa>>

Website hii inaletwa kwako na Melkisedeck Leon Shine.

Naomba utafakari kuhusu; Sala ni ufunguo. Mungu akubariki sana. Tuombeane…!