Mafundisho ya Dini

๐Ÿ‘‰Je, ufunuo wa Mungu unaendelea hata leo?

Hapana, ufunuo wa Mungu hauendelei, kwa sababu alikwisha kuukamilisha kwa kumtuma duniani Neno wake wa milele. โ€œKwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo. Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunuaโ€ (Yoh 1:17-18). Baada yake hauwezekani ufunuo mpya. Hatutakiwi kumuamini yeyote akidai eti, ametumwa kukamilisha kazi ya Yesu; kwa kuwa mwenyewe alisema, โ€œMbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamweโ€ (Math 24:35). โ€œIjapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe! Kama tulivyotangulia kusema, na sasa nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe!โ€ (Gal 1:8-9).

๐Ÿ‘‰Ufunuo wa Mungu unatufikiaje miaka elfu mbili baada ya Kristo?

Ufunuo wa Mungu unatufikia kupitia Kanisa lake, lililokabidhiwa Mapokeo ya Mitume na linaloongozwa na Roho Mtakatifu hadi ukweli wote. Yesu aliahidi kwamba, โ€œYeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yakeโ€ (Yoh 16:13). โ€œMaana Roho huchunguza yote hata mafumbo ya Munguโ€ (1Kor 2:10).

๐Ÿ‘‰Je, ufunuo wa Mungu unaweza kufafanuliwa rasmi na kila mtu?

Hapana, ufunuo wa Mungu unaweza kufafanuliwa rasmi na umoja wa Maaskofu tu, kwa kuwa ndio waandamizi wa Mitume 12 wa Yesu. โ€œAu je, neno la Mungu lilitoka kwenu? Au kuwafikia ninyi peke yenu?โ€ (1Kor 14:36). โ€œHakuna unabii katika Maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamuโ€ (2Pet 1:20-21). Tunahitaji unyenyekevu wa Mwafrika ambaye shemasi Filipo alimsikia โ€œanasoma chuo cha nabii Isaya; akanena, โ€˜Je, yamekuelea haya unayosoma?โ€™ Akasema, โ€Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiongoza?โ€™ Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja nayeโ€ (Mdo 8:30-31).

๐Ÿ‘‰Tupokeeje ufunuo wa Mungu?

Tupokee ufunuo wa Mungu kwa kusadiki mafundisho ya Kanisa lake, ili tuzidi kumjua na kuambatana naye bila ya kudanganyika. Yesu aliwaambia Mitume wake, โ€œAwasikilizaye ninyi anisikiliza mimi, naye awakataaye ninyi anikataa mimi; naye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenitumaโ€ (Lk 10:16). โ€œSisi nasi twamsukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa, mlipopata lile neno la ujumbe la Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kwelikweli, litendalo kazi pia ndani yenu ninyi mnaoaminiโ€ (1Thes 2:13).

.

.

Makala

Mafundisho

.

.

.

IMG_20181021_135203.jpg

Kama Una mashaka na Imani na mafundisho ya Kanisa Katoliki soma hapa>>

Website hii inaletwa kwako na Melkisedeck Leon Shine.

Naomba utafakari kuhusu; Neno "Nimekusamehe". Mungu akubariki sana. Tuombeane…!