Mafundisho ya Dini

๐Ÿ‘‰Sala ni nini?

Sala ni kuinua mioyo yetu kwa Mungu na kuongea nae

๐Ÿ‘‰Sala ya Taamuli ni nini?

Sala ya taamuli ni sala ya kumtazama tuu Mungu kwa upendo mkubwa moyoni

๐Ÿ‘‰Sala ya fikara ni nini?

Sala ya fikra ni sala asaliyo mtu peke yake au akiwa na wengine kimya kimya akimuwaza Mungu

๐Ÿ‘‰Masifu ni nini?

Masifu ni sala au wimbo unaomsifu na kumtambua Mungu kuwa Mungu

๐Ÿ‘‰Neno "Amina" katika sala lina maana gani?

Neno "Amina" katika sala lina maanisha "Na iwe Hivyo"

๐Ÿ‘‰"Aleluya" katika sala, hasa zaburi ina maana gani?

"Aleluya" katika sala, hasa zaburi ina maanisha "Msifuni Mungu"

๐Ÿ‘‰Hosana maana yake ni nini?

Hosana maana yake ni "Saidia twakuomba" au tafadhali

๐Ÿ‘‰Ishara ya msalaba ni nini?

Ishara ya Msalaba ni tendo la mtu kugusa panda la uso, kifua na mabega kwa kutumia mkono wa kulia na kutamka "Kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina"

๐Ÿ‘‰Ishara ndogo ya Msalaba juu ya panda la uso, mdomo, na kifua kabla ya Injili ina maana gani?

Maana yake ni kama Ahadi kuwa, Niko tayari kulifahamu Neno la Mungu kwa akili yangu, Nitalitangaza kishujaa kwa Midomo yangu, Nitalipenda na kulishika kwa Moyo wangu wote.

๐Ÿ‘‰Mungu ni nani?

Mungu ndiye muumba wa kila kitu katika uwingu na nchi, Mkubwa wa ulimwengu mwenye kuwatuza watu wema na kuwaadhibu watu wabaya. 8Msiwe kama wao, kwa sababu Baba yenu anajua kile mnachohitaji kabla hamjamwomba.โ€™โ€™ 9โ€˜โ€˜Hivi basi, ndivyo iwapasavyo kuomba : โ€œBaba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe.(Mt. 6:8-9). 17Yesu akamwambia, โ€˜โ€˜Usinishike, kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu ukawaambie, โ€˜Ninapaa kwenda kwa Baba yangu ambaye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu ambaye ni Mungu wenu.โ€™ โ€™โ€™ (Yoh 20:17)

๐Ÿ‘‰Mungu ni nini?

Mungu ni Roho kamili na ukamilifu wake hauna mipaka. (Yoh. 4:24, Kut.3:13-15, Zb. 144:3)

๐Ÿ‘‰Nini maana ya neno "Fumbo"?

Fumbo ni ukweli ambao hatuwezi kuelewa kikamilifu, lakini tunasadiki kwa kuwa Mungu hutufumbulia. (Math 11:27)

๐Ÿ‘‰Mmisionari ni nani?

Ni mtu anayepeleka injili mahali ambapo haijafikishwa. (Mk 16:15-20)

๐Ÿ‘‰Jimbo Katoliki ni nini?

Jimbo Katoliki ni Jumuiya ya Wakristo ambao katika I mani na Sakramenti wana ushirika na Askofu aliye halifa wa Mitume.

๐Ÿ‘‰Maklero ni wakina nani?

Maklero ni watu wote wenye daraja Takatifu yaani Maaskofu, Mapadri na Mashemasi.

๐Ÿ‘‰Watawa ni akina nani?

Watawa ni Waamini, Walei au Maklero waliowekwa wakfu kwa Mungu katika Kanisa kwa ajilli ya wokovu wao na wa dunia:-

1. Kwa kufunga rasmi nadhiri za Kitawa mbele ya Kanisa

2. Kwa kuishi masharti ya injili, utii, ufukara na useja mtakatifu.

3. Kwa kufuata mtindo wa maisha uliokubalika na Kanisa

๐Ÿ‘‰Walei ni wakina nani?

Walei ni wote katika Kanisa wasio na Daraja Takatifu

๐Ÿ‘‰Ushirika wa Watakatifu ni nini?

Ushirika wa Watakatifu ni:-

1. Umoja na ushirikiano kati ya Wakristo Duniani, Watakatifu Mbinguni, na marehemu toharani.

2. Ni muungano wa Waamini wote katika Ekaristi Takatifu.

๐Ÿ‘‰Yesu maana yake nini?

Yesu maana yake ni โ€œMungu Mwokoziโ€: alichaguliwa jina hilo kabla hajazaliwa, akitabiriwa kuwa โ€œyeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zaoโ€ (Math 1:21). โ€œHakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwaloโ€ (Mdo 4:12).

๐Ÿ‘‰Kristo maana yake nini?

Kristo maana yake ni โ€œAliyepakwa mafutaโ€ awe kiongozi wa taifa lake walivyotabiri manabii wa kale. Tunahitaji kujua โ€œhabari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvuโ€ (Mdo 10:38).

๐Ÿ‘‰Hekalu ndiyo nini?

Hekalu ndipo tunapomuendea Mungu kwa ibada. Yesu aliheshimu na kutakasa hekalu pekee la taifa lake kama โ€œnyumba ya Babaโ€ yake (Yoh 2:16), lakini alitabiri kuwa litabomolewa moja kwa moja, na kuwa watu watapaswa kuabudu ndani yake aliye hekalu hai. โ€œWayahudi walisema, โ€˜Hekalu hili lilijengwa katika muda wa miaka arobaini na sita, nawe utalisimamisha katika siku tatu?โ€™ Lakini yeye alinena habari za hekalu la mwili wakeโ€ (Yoh 2:20-21). โ€œKatika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Rohoโ€ (Ef 2:22). โ€œHamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyiโ€ (1Kor 3:16-17).

๐Ÿ‘‰Zaka ni nini?

Zaka ni asilimia kumi (10%) ya pato la mtu kwa mwaka ambalo anapaswa kulitoa kwa Kanisa.

๐Ÿ‘‰Sakramenti ya Ekaristi ni nini?

Sakramenti ya Ekaristi ni Sakramenti ya Mwili na Damu ya Yesu Kristo, aliye kweli katika Maumbo ya Mkate na Divai. (Yoh 6:1-17, Mt 26:26-28)

USIKOSE HII๐Ÿ‘‰ Tupokeeje ufunuo wa Mungu?

.

.

Makala

Mafundisho

.

Sala

.

.

IMG_20180109_191617.jpg

Kama Una mashaka na Imani na mafundisho ya Kanisa Katoliki soma hapa>>

Website hii inaletwa kwako na Melkisedeck Leon Shine.

Naomba utafakari kuhusu; Uwe na maono. Mungu akubariki sana. Tuombeane…!