Mafundisho ya Dini

πŸ‘‰Dhamiri adilifu ni nini?

Dhamiri adilifu, iliyo ndani kabisa mwa mtu, ni uamuzi wa akili ambao kwa wakati wake unamuagiza mtu atende mema na kukwepa maovu

πŸ‘‰Katika hukumu zake dhamira ifuate nini?

Katika hukumu zake dhamira ifuate daima Injili, Amri za Mungu na za Kanisa na wajibu zetu.

πŸ‘‰Twajenga na kutunza dhamira zetu namna gani?

Twajenga na kutunza dhamira zetu kwa;-

1. Kufuata sauti ya Roho Mtakatifu

2. Kuzingatia mafundisho ya dini

3. Kuzingatia mila na desturi njema tulizopata katika malezi.

4 Kufuata mifano na tabia njema ya wenzetu na ya Watakatifu

πŸ‘‰Hadhi ya nafsi ya mtu inadai nini kuhusu dhamiri adilifu?

Hadhi ya nafsi ya mtu inadai unyofu wa dhamiri adilifu, yaani upande wa akili na sheria ya Mungu

πŸ‘‰Dhamiri adilifu inaundwa namna gani iwe nyofu na ya kweli?

Dhamiri nyofu inayosema kweli inaundwa kwa

1. Malezi

2. Upokeaji wa neno la Mungu

3. Upokeaji wa Mafundisho ya Kanisa

4. Sala

5. Utafiti wa dhamiri

πŸ‘‰Dhamiri adilifu inatengenezwa na kusaidiwa na nini?

Dhamiri adilifu inatengenezwa na vipaji vya Roho Mtakatifu na kusaidiwa na mashauri ya watu wenye busara.

πŸ‘‰Dhamiri inatakiwa kufuata daima masharti gani?

Dhamira inatakiwa kufuata daima masharti yafuatayo

1. Hairuhusiwi kutenda maovu kusudi yapatikane mema

2. Yoyote muyatakayo mtendewe na watu, ninyi watendeeni vivyo hivyo. (Mt 7:12)

3. Upendo hufuata daima nia na heshima kwa jirani na kwa dhamira yake

.

.

Makala

Mafundisho

.

.

.

IMG_20180125_210005.jpg

Kama Una mashaka na Imani na mafundisho ya Kanisa Katoliki soma hapa>>

Website hii inaletwa kwako na Melkisedeck Leon Shine.

Naomba utafakari kuhusu; Mungu anajibu sala kutokana na nia. Mungu akubariki sana. Tuombeane…!