Mafundisho ya Dini

πŸ‘‰Katika Amri ya Tano ya Mungu tumeamriwa nini?

Tumeamriwa tutunze uhai wetu na wa watu wengine tangu mwanzo hadi mwisho. (Mwa 4:10-11)

πŸ‘‰Kwa nini ni lazima kutunza uhai wetu na wa wenzetu?

Kwa sababu uhai wa watu wote umetoka kwa Mungu

πŸ‘‰Haki gani ya Binadamu ni ya msingi kupita zote?

Haki ya binadamu iliyo ya msingi kupita zote ni uhai wake ambao ni lazima uheshimiwe na kulindwa tangu siku ya kutungwa mimba

πŸ‘‰Nani anatenda dhambi dhidi ya amri ya tano ya Mungu? Mambo yanayovunja Amri ya Tano ya Mungu

Anayetemda dhambi dhidi ya amri ya tano ya Mungu ni yule;-

1. Anayemuua mtu au anayejiua mwenyewe

2. Anayemdhuru mwingine kwa namna yoyote ile

3. Anayeua Mimba na kuharibu nguvu za uzazi

4. Anayesaidia kuua, kumdhuru mtu au anayesaidia kutoa/kuharibu mimba

5. Anayeharibu mazingira yaliyomuhimu kwa uhai

6. Anayetetea au kuendeleza mifumo ya ya dhuluma, uhasama na vita.

.

.

Mafundisho

.

.

.

IMG_20181021_134724.jpg

Kama Una mashaka na Imani na mafundisho ya Kanisa Katoliki soma hapa>>

Website hii inaletwa kwako na Melkisedeck Leon Shine.

Naomba utafakari kuhusu; Umuhimu wa kumsogelea Mungu. Mungu akubariki sana. Tuombeane…!