Mafundisho ya Dini

πŸ‘‰Je, Amri ya Saba ya Mungu inafundisha nini?

Amri ya saba ya Mungu inafundisha kuitambua mali ya mtu na kuiheshimu.

πŸ‘‰Mali ya mtu ni ipi?

Mali ya mtu ni ile aliyoipata kwa njia halali yaani kwa haki.

πŸ‘‰Lengo la mali ya binafsi ni lipi?

Kutosheleza mahitaji yake mtu binafsi, ya familia, ya wenye shida na ya kanisa.

πŸ‘‰Mtu awatendeje wanyama?

Mtu anatakiwa kuwatendea wanyama kwa wema kama viumbe wa Mungu

πŸ‘‰Amri ya saba ya Mungu inakataza nini?

Inakataza

1. Wizi

2. Kulangua

3. Kutapeli

4. Kughushi

5. Kufuja mali

6. Kutoa au kupokea rushwa

7. Ufisadi

8. Kuharibu mali ya mtu au jamii

πŸ‘‰Anayejipatia mali kwa njia isiyo ya halali yampasa kufanya nini?

Anayejipatia mali kwa njia isiyo ya halali yampasa kurudisha gharama yake kwa mwenye mali

πŸ‘‰Anayeharibu mali ya mwingine lazima afanye nini?

Anayeharibu mali ya mwingine lazima alipe hasara aliyosababisha. (Lk 19:8)

πŸ‘‰Je yatupasa kufanya kazi?

Ndiyo, kwa sababu:

1. Kazi inampa mwanadamu heshima

2. Kufanya kazi ni wajibu wa haki. (Mwa 1:28)

πŸ‘‰Je ni lazima kuwasaidia masikini na fukara?

Ndiyo, Kuwatendea Masikini mema ni kumtendea Yesu mwenyewe. (Mt 25:40)

USIKOSE HIIπŸ‘‰ Vyanzo vya sala za Kikristo

.

.

Makala

Mafundisho

.

.

.

images-18.jpeg

Kama Una mashaka na Imani na mafundisho ya Kanisa Katoliki soma hapa>>

Website hii inaletwa kwako na Melkisedeck Leon Shine.

Naomba utafakari kuhusu; Sifa za Sala yeyote. Mungu akubariki sana. Tuombeane…!