YESU%20MFALME%20WA%20HURUMA.gif

Blog kwa Wakatoliki

Mpangilio wa kurasa Kwa Wakatoliki ndani ya AckySHINE

|| HOME || MAKALA || TAFAKARI || SALA || MAFUNDISHO || MIUJIZA || WATAKATIFU || NYIMBO || PICHA ||

.

πŸ‘‰ Zaburi ya Toba, Zaburi ya 51βœ…

πŸ‘Baada ya kusoma kuhusu;πŸ‘‡
images-9.jpeg
πŸ’₯Leo nimekutayarishia makalaπŸ“œ kuhusu Zaburi ya Toba, Zaburi ya 51.πŸ‘‡

πŸ’«Zaburi ya Toba, Zaburi ya 51πŸ‘‡

Imehaririwa na; Melkisedeck Leon Shine. Tarehe 15 Apr 2015 08:56. [Legal & Authority]

zaburi 51

1 Ee Mungu, unirehemu,Sawasawa na fadhili zako.Kiasi cha wingi wa rehema zako,Uyafute makosa yangu.

2 Unioshe kabisa na uovu wangu,Unitakase dhambi zangu.

3 Maana nimejua mimi makosa yanguNa dhambi yangu i mbele yangu daima.

4 Nimekutenda dhambi Wewe peke yako,Na kufanya maovu mbele za macho yako.Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo,Na kuwa safi utoapo hukumu.

5 Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu;Mama yangu alinichukua mimba hatiani.

6 Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni;Nawe utanijulisha hekima kwa siri,

7 Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi,Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji

8 Unifanye kusikia furaha na shangwe,Mifupa uliyoiponda ifurahi.

9 Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu;Uzifute hatia zangu zote.

10 Ee Mungu, uniumbie moyo safi,Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu

11 Usinitenge na uso wako,Wala roho yako mtakatifu usiniondolee.

12 Unirudishie furaha ya wokovu wako;Unitegemeze kwa roho ya wepesi.

13 Nitawafundisha wakosaji njia zako,Na wenye dhambi watarejea kwako.

14 Ee MUNGU, Mungu wa wokovu wangu,Uniponye na damu za watu,Na ulimi wangu utaiimba haki yako.

15 Ee Bwana, uifumbue midomo yangu,Na kinywa changu kitazinena sifa zako.

16 Maana hupendezwi na dhabihu, au ningeitoa,Wewe huridhii sadaka ya kuteketezwa.

17 Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika;Moyo uliovunjika na kupondeka,Ee Mungu, hutaudharau.

18 Uitendee mema Sayuni kwa radhi yako,Uzijenge kuta za Yerusalemu.

19 Ndipo utakapopendezwa na dhabihu za haki,Na sadaka za kuteketezwa, na kafara.Ndipo watakapotoa ng’ombeJuu ya madhabahu yako.

πŸ‘‰ Ishara ya MsalabaπŸ“œ

images-11.jpeg

πŸ“Nini MaoniπŸ’­ yako Kuhusu Zaburi ya Toba, Zaburi ya 51? Niandikie hapaπŸ‘‡

Add a New Comment
or Sign in as Wikidot user
(will not be published)
- +
images-11.jpeg

πŸ“š Endelea kusoma kuhusu;-πŸ‘‡

.

.

images-10.jpeg

"Sala ni kama chakula cha Roho, Bila sala roho inakufa. Tusali daima ili roho zetu ziwe hai siku zote.."

.

.

images-8.jpeg

"Uwe na maono au ndoto ya mambo unayotaka kufanya maishani naye Mungu atakubariki na kujidhihirisha katika ndoto zako."

.

.

IMG_20170703_130916.jpg

"Kwa njia ya sala Binadamu anampa Mungu Utukufu, Mungu anampa Binadamu Wokovu na Neema.,"

.

.

Tumsifu Yesu Kristu….

IMG_20170703_130405.jpg
Melkisedeck Leon Shine

"Mtumainie Mungu kwa maana Mungu hawatupi wale wamtumainiao na kumgoja. Mkono wake upo tayari kwa ajili ya kuwaokoa wale wanaomwelekea."

Jina langu ni Melkisedeck L. Shine. Mwandishi wa Blog hii, Mimi ni Mkristu Mkatoliki

images-7.jpeg

"Mungu anaporuhusu ukaingia katika majaribu na mateso hana nia ya kukutesa bali anataka kukuimarisha. Mungu ni mwema kila wakati."

Usisite kuniandikia maoni,mapendekezo au maswali hapa kuhusu blog hii na kuhusu Imani na Mafundisho ya Kanisa Katoliki

Jina
Dini/dhehebu
Mfano Mwislamu, Katoliki, Lutherani, Mlokole n.k
Email
Itatumika kukujibu
Maoni yako

images-7.jpeg

"Sala ni kama chakula cha Roho, Bila sala roho inakufa. Tusali daima ili roho zetu ziwe hai siku zote.."

ABOUT ME | MY PERSONAL BLOG

.