Mtakatifu Petro Mtume

By, Melkisedeck Shine.


Mtakatifu Petro Mtume

Petro alikuwa Myahudi wa karne ya 1, mfuasi wa Yesu Kristo, tena kati ya wandani wake.

Baada ya Yesu, ndiye mtu anayejulikana zaidi katika Injili zote nne.

Katika orodha zote nne za mitume 12 wa Yesu zinazopatikana katika Biblia ya Kikristo anashika nafasi ya kwanza (tofauti na wenzake wengi ambao wanabadilishana nafasi, na kinyume cha Yuda Iskarioti, msaliti anayepewa daima nafasi ya mwisho); isitoshe Math 10:2 inasisitiza: "Wa kwanza Simoni aliyeitwa Petro".

Wakristo wengi, hasa Wakatoliki na Waorthodoksi, wanamheshimu kama mtakatifu tena kama papa wa kwanza wa Roma hadi kifodini chake kati ya 64 na 67, wakati wa dhuluma ya Dola la Roma dhidi ya Ukristo iliyoanzishwa na Kaisari Nero.

Maana ya jina la Mtume Petro

Mwana wa Yona au Yohana, jina lake asili kwa Kiebrania ni שמעון Šim‘ôn, Shim'on, kutoka kitenzi shama "kusikiliza").

Kadiri ya Injili ya Mathayo (16:18) na Injili ya Yohane (1:42) ni Yesu Kristo aliyembadilishia jina akamuita Kefa (kwa Kiaramu "mwamba", jina ambalo lilitafsiriwa kwa Kigiriki Petros na kwa Kilatini Petrus). Mtume Paulo alimtaja kama Kephas (1Kor 1:12; 3:22; 9:5; 15:5; Gal 1:18; 2:9,11,14) na mara moja kama Petro (Gal 2:7-8).

Maisha Mtume Petro ya awali

Mzaliwa wa Bethsaida, kaskazini kwa Galilaya alihamia Kapernaumu pamoja na ndugu yake Andrea kwa ajili ya uvuvi. Kijiji hicho kikawa baadaye makao makuu ya utume wa Yesu katika maeneo ya kaskazini ya Palestina. Hasa Yesu alitumia nyumba na boti la Petro.

Mtu wa ndoa, Petro hakusomea ualimu wa Torati, lakini alimfuata Yohane Mbatizaji. Akiwa kwake, karibu na mto Yordani, aliletwa na Andrea kwa Yesu (Yoh 1:41-42).

Maisha yake Baada ya kukutana na Yesu

Aliitwa na Yesu kumfuata wakiwa huko ziwani (Math 4:19-20; Lk 5:11) akiahidiwa atakuwa "mvuvi wa watu", halafu akafanywa mtume wake wa kwanza.

Pamoja na Mtume Yakobo Mkubwa na Mtume Yohane wana wa Zebedayo alishirikishwa matukio kadhaa ya pekee kama mwandani wa Yesu, hasa aliposhuhudiwa na Mungu mlimani huku ameng'aa kiajabu.

Akiwa na silika ya uchangamfu, alikuwa msemaji mkuu kati ya mitume wa Yesu, hasa walipoulizwa naye wanamuona kuwa nani, akajibu: "Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai" (Math 16:16). Ndipo alipojibiwa na Yesu: "Heri wewe Simoni Bar-Yona, kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni. Nami nakuambia: Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lolote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni, na lolote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni" (Math 16:17-19).

Ungamo la namna hiyo linaripotiwa na Yoh 6:68: "Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele. Nasi tumesadiki, tena tumejua, ya kuwa wewe ndiwe Mtakatifu wa Mungu".

Mara nyingine majibu yake yalimvutia lawama ya Yesu, hata akaitwa "Shetani" kwa sababu ya kumshawishi aende mbali na matakwa ya Mungu ili afuate mbinu za kibinadamu (Mk 8:33).

Kwa kuwa Yesu alitakiwa kutumikia akawafundisha wafuasi wake kutumikia, aliagizwa kuandaa pamoja na Yohane karamu ya mwisho ya Yesu na mitume wake kwenye Pasaka, ambapo ilimbidi akubali kuoshwa naye miguu (Yoh 13:8-9).

Yesu alipokamatwa, alijaribu kumtetea kwa upanga, halafu akamfuata kwa mbali pamoja na Yohane mpaka ndani ya ua wa nyumba ya kuhani mkuu. Ndipo woga ulipomfanya amkane Yesu mara tatu kwa kiapo kama alivyotabiriwa naye.

Hata hivyo, Yesu alikuwa amemuahidia atamuombea aongoke akaimarishe wenzake: "Simoni, Simoni, tazama, Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano; lakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike; nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako" (Lk 22:31-32).

Basi, alipotazamwa na Yesu akajuta kwa machozi mengi.

Maisha ya Petro Baada ya kufufuka kwa Yesu

Baada ya kifo cha Yesu, akawa wa kwanza kuingia kaburi lake tupu tena wa kwanza kati ya mitume kutokewa na Yesu mfufuka, naye katika tokeo lingine katika ziwa Galilaya akamthibitisha katika uongozi wa kundi lake lote, kondoo na wanakondoo. Alifanya hivyo baada ya Petro kukiri mara tatu (Yoh 21:17): "Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda".

Kadiri ya Matendo ya Mitume, kabla ya ujio wa Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste ya mwaka huo (30 au 33 B.K.) aliongoza wafuasi wetu kuziba pengo la Yuda, mtume msaliti, kwa kumweka Mathia mahali pake.

Halafu akawa mhubiri shujaa akachukua maamuzi muhimu sana kwa uenezi wa Kanisa, kama vile kumbatiza akida Korneli na Wapagani wengine bila ya kudai watahiriwe kwanza.

Jambo hilo lilimvutia lawama kubwa, lakini zikaja kwisha hasa kwa mtaguso wa Yerusalemu (mwaka 49).

Petro alikuwa maarufu kwa miujiza pia, kiasi cha kuponya wengi kwa kivuli chake.

Herode Agripa I alipomuua Yakobo na kumfunga Petro ili kumuua pia, alitolewa gerezani kimuujiza akahama Yerusalemu (mwaka 44).

Katika Waraka kwa Wagalatia Paulo aliandika jinsi alivyomlaumu Petro wakiwa Antiokia.

Pia alimtaja katika Waraka wa kwanza kwa Wakorintho kama mtu mwenye wafuasi kati yao. Hivyo inaonekana alihubiri huko.

Waraka wa kwanza wa Petro unasema aliuandika akiwa Babuloni, jina la fumbo lililotumiwa na Wakristo kudokezea Roma. Kwa kuwa uliandikwa kwa Wakristo wachanga wa nyanda za juu za nchi inayoitwa leo Uturuki, inaonekana alikuwa amewahubiria kwanza.

Kifo cha Mtume Petro

Yoh 21:18 inaeleza kifumbo kifodini ambacho Petro alimtukuza Mungu mjini Roma, katika eneo la Vatikano, inasemekana kwa kusulubiwa kichwa chini, miguu juu. Ndipo linapoheshimiwa kaburi lake chini ya altare kuu ya kanisa kubwa kuliko yote duniani.

Kifo hicho kinashuhudiwa hasa na waandishi mbalimbali wa karne za kwanza, kama vile Papa Klementi I kati ya miaka 95 na 97, Ignasi wa Antiokia, Dionisi wa Korintho, Irenei wa Lyons, Klementi wa Aleksandria, Tertuliani, Jeromu n.k.

Vitabu vya Mtume Petro

Mbali ya Barua ya kwanza, ambayo aliiandika mwenyewe kwa msaada wa Sila na kukubaliwa mapema kama kitabu kitakatifu, vitabu vingine viliandikwa kwa jina la Petro kuanzia mwisho wa karne ya 1.

Kati yake kimoja kimeingia katika Agano Jipya kama Waraka wa pili wa Petro, wakati vingine vyote vilikataliwa na Kanisa, kama vile Injili ya Petro, Matendo ya Petro, Ufunuo wa Petro.Fwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya Mtakatifu Petro Mtume

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; Mtakatifu Petro Mtume

a.gif Mtakatifu Maria Magdalena

Kadiri ya Injili, baada ya kushuhudia kifo cha Yesu na mazishi yake (Mk 15:40-16:1; Math 27:56-28:1; Yoh 19:25), upendo na juhudi vilimfanya mwanamke huyo awahi kwenye kaburi lake alfajiri ya siku ya Jumapili. Huko alitokewa na malaika na kuambiwa amefufuka… soma zaidi

a.gif Mafundisho (Dogma) ya Kanisa Katoliki kuhusu Bikira Maria

Kuna mafundisho makuu manne kumhusu Bikira Maria ambayo ni lazima kila Mkatoliki ayasadiki kutokana na ufunuo wa Mungu: 1. B. Maria mkingiwa dhambi ya asili 2. B. Maria Mama wa Mungu 3. B. Maria Bikira daima 4. B. Maria kupalizwa mbinguni mwili na roho.. soma zaidi

a.gif Heshima za Liturujia ya Kiroma kwa Maria

Kuna ibada za Mama Bikira Maria zinazoadhimishwa katika liturujia ya Kiroma. Hapa zimepangwa kulingana na heshima zinavyozidiana:.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉SALA YA ASUBUHI

[Wimbo Mzuri PA.gif] Bwana Tunakushukuru

[Tafakari ya Sasa] 👉Sala ni chimbuko la Fadhila

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Ambrosi

[Jarida La Bure] 👉Biblia Takatifu: Agano la Kale

a.gif Kampeni ya usafi na Utunzaji wa mazingira

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.
Lengo la kampeni Hii ni kuhamasisha watu kusafisha na kutunza mazingira yao kwa manufaa yao ya sasa na kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Kampeni hii inaamini kuwa mazingira yakisafishwa na kutunzwa vizuri yanaweza kuwa msaada kijamii, kiuchumi na kiafya kwa kizazi hiki na kizazi kijacho… soma zaidi

a.gif Katika karamu ya Bwana tunakula na kunywa nini?

Katika karamu ya Bwana tunakula na kunywa Mwili wa Damu ya Kristo. Katika sala kuu ya ekaristi padri anaporudia maneno ya Yesu juu ya mkate na divai, Roho Mtakatifu anavigeuza kwa dhati: mkate si tena mkate, wala divai si tena divai, ingawa maumbo yanabaki yaleyale kwa hisi zetu… soma zaidi

a.gif Kwa sababu gani yatupasa kuwa na usafi wa moyo?

Yatupasa kuwa na usafi wa moyo kwa sababu:.. soma zaidi

a.gif Sakramenti ya kwanza daima ni ipi?

Sakramenti ya kwanza daima ni ubatizo, kwa kuwa ndio kupata uzima mpya kwa kushiriki kifo na ufufuko wa Yesu, inavyodokezwa wazi zaidi mtu akizamishwa na kutolewa majini… soma zaidi

a.gif Katika hukumu zake dhamira ifuate nini?

Katika hukumu zake dhamira ifuate daima Injili, Amri za Mungu na za Kanisa na wajibu zetu… soma zaidi

a.gif Yesu alipokufa, ilikuwaje?

Yesu alipokufa, nafsi yake ya Kimungu iliendelea kushikamana na roho na mwili vilivyotengana: kwa hiyo mwili wake uliozikwa haukuweza kuoza kaburini; roho yake ilishukia kuzimu kuwatoa waadilifu waliomtangulia awaingize pamoja naye mbinguni… soma zaidi

a.gif Novena ya Huruma ya Mungu

Utangulizi.. soma zaidi

a.gif Kujikweza Mbele ya Mungu

Rejea Luka 14:7-24 na Luka 18 :9-18.. soma zaidi

a.gif Umwilisho maana yake ni nini?

Umwilisho ni ile hali ya Yesu kama Mungu kujifanya mtu kwa Bikira Maria mzaa. (Yoh 1:14).. soma zaidi

a.gif Tafakari ya Leo ya Katoliki

Tafakari kwa kusoma Makala hizi;.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.