SOMO 1

Mdo 13:14, 43-52

Paulo na Barnaba walitoka Perge, wakapitakati ya nchi, wakafika Antiokia, mjiwa Pisidia, wakaingia katikasinagogi siku ya sabato, wakaketi. Sinagogi ilipofumukana, Wayahudi na waongofu watauwa wengi wakashikamana na Paulo na Barnaba; ambao, wakisemanao, wakawatia moyo kudumu katika neemaya Mungu.

Hata sabatoya pili, watuwengi, karibu mji wote, wakakusanyika walisikie neno la Mungu. Bali Wayahudi walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayakanusha maneno yaliyonenwana Paulo, wakibishana kutukana. Paulo na Barnaba wakanena kwa ushujaa wakasema, Ilikuwalazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza; lakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, na kujiona nafsizenu kuwa hamkustahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia Mataifa. Kwa sababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana.

Nimekuwe kauwe nuru ya Mataifa, Upate kuwa wokovu hata mwishowa dunia.

Mataifa waliposikia hayo wakafurahi, wakalitukuza neno la Bwana, nao waliokuwa wamekusudiwa uzimawamilele wakaamini. Neno la Bwana likaeneakatika nchi ileyote.

Lakini Wayahudi wakawafitinisha wanawake watauwa wenyecheo na wakuu wa mji, wakawataharakisha watu wawaudhi Paulo na Barnaba; wakawatoa katika mipaka yao, wakaenda Ikonio. Na wanafunzi walijaa furaha na Roho Mtakatifu.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 100:1-3,5 (K) 3

(K) Tuwatu wake, nakondoo wa malishoyake.

Mfanyieni Bwana shangwe, duniayote;
Mtumikieni Bwana kwafuraha;
Njonimbelezakekwakuimba. (K)

Juenikwamba Bwana ndiyeMungu;
Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake;
Tuwatu wake, nakondoowamalishoyake. (K)

Kwakuwa Bwana ndiyemwema;
Rehema zake ni za milele;
Na uaminifu wake vizazi na vizazi. (K)

SOMO 2

Ufu. 7:9, 14b-17

Wakati ule, mimi, Yohane, niliona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao.

Mmoja wa wale wazee akiniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-kondoo. Kwa hiyo wako mbele ya kiti cha enzi cha mungu, nao wanamtumikia mchana na usiku katika hekalu lake, na yeye aketiye katika kiti cha enzi atatanda hema yake juu yao. Hawataona njaa tena, wala hawataona kiu tena, wala jua halitawapiga, wala hari iliyo yote. Kwa maana huyo Mwana-kondoo, aliye katikati ya kiti cha enzi, atawachunga, naye atawaongoza kwenye chemchemi za maji yenye uhai, na Mungu atayafuta machozi yote katika macho yao.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

SHANGILIO

Yn. 10:14

Aleluya, aleluya,
Mimi ndimi mchungaji mwema; nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi.
Aleluya.

INJILI

Yn. 10:27-30

Yesu alisema; Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata. Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu. Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu. Mimi na Baba tu umoja.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.

Ishara-ndogo-ya-Msalaba.png