MAFUNDISHO YA KANISA KATOLIKI KUHUSU NEEMA

πŸ‘‰β” Je, tunaweza kuhakikisha neema ya utakaso?

Hapana, hatuwezi kuhakikisha neema ya utakaso kwa kuwa ni tukio ambalo linapita maumbile na kufanyika rohoni, hivyo halifikiwi na hisi zetu. Pengine Mungu anatokeza dalili fulani za badiliko hilo kama vile furaha ya ndani au karama ya nje, lakini hizo hazihitajiki wala hazitoshi kuthibitishia mtu amepata neema hiyo. β€œWengi wataniambia siku ile: Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri: Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu” (Math 7:22-23). β€œNijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu” (1Kor 13:1-3).


πŸ‘‰β” Neema ni nini?

Neema ni kipaji cha roho kinachopita nguvu za viumbe vyote; ndicho kipaji tupewacho na Roho Mtakatifu ili tupate uzima wa milele. (Lk 1:30, Rum 5:2)


πŸ‘‰β” Kuna aina ngapi za neema?

Kuna aina mbili za neema

1. Neema ya utakaso

2. Neema ya msaada


πŸ‘‰β” Neema ya Utakaso ni nini?

Neema ya Utakaso ni uzima wa Kimungu unaomiminwa na Roho Mtakatifu mioyoni mwetu. (Yoh 1:16, Yoh 3:3-5)


πŸ‘‰β” Neema ya Utakaso yapatikanaje?

Neema ya Utakaso yapatikana kwa;

1. Kwanza kwa Sakramenti ya Ubatizo

2. Sakramenti ya Kitubio

3. Kwa majuto kamili (majuto ya mapendo)

4. Yaongezwa kwa kupokea Sakramenti nyingine

5. Kwa Sala

6. Kwa Ibada Takatifu

7. Kwa matendo mema


πŸ‘‰β” Neema ya Utakaso yapoteaje?

Neema ya Utakaso yapotea kwa kutenda dhambi kubwa (dhambi ya mauti)


πŸ‘‰β” Kuna Faida ya kuwa na Neema ya Utakaso?

Faida ya kuwa na Neema ya Utakaso ni;-

1. Kupendwa na Mungu hapa duniani

2. Na kupokelewa kwake mbinguni baada ya kufa


πŸ‘‰β” Neema ya Msaada ni nini?

Neema ya Msaada ni msaada tupatao kwa Roho Mtakatifu kutuongezea nguvu Rohoni tutende mambo mema na tuepuke Mabaya


πŸ‘‰β” Neema ya Msaada yapatikanaje?

Neema ya Msaada yapatikana kwa kupokea Sakramenti, kusali, na kutenda mambo ya Ibada (Yoh 15:5, 1Tim 2:4)


MAFUNDISHO YA KANISA KATOLIKI KUHUSU REHEMA

πŸ‘‰β” Rehema ni nini?

Rehema ni msamaha au ondoleo la adhabu ya dhambi tulizostahili sababu ya dhambi zilizokwisha ondolewa


πŸ‘‰β” Rehema hutolewa na nani?

Rehema hutolewa na Kanisa Katoliki kwa kutugawia mastahili ya Yesu Kristo, Bikira Maria na Ya Watakatifu


πŸ‘‰β” Kuna Rehema za namna ngapi?

Rehema za namna mbili

1. Rehema kamili

2. Rehema pungufu (Rehema isiyo kamili)


πŸ‘‰β” Rehema kamili ni nini?

Rehema kamili ni msamaha wa kufutiwa adhabu zote za muda za dhambi


πŸ‘‰β” Rehema isiyo kamili (pungufu) ni nini?

Rehema isiyo kamili (pungufu) ni msamaha wa kupunguziwa adhabu ya dhambi


πŸ‘‰β” Adhabu za dhambi huondolewa kwa namna gani? Jinsi ya kupata rehema

Adhabu za dhambi huondolewa kwa;

1. Kufanya malipizi au majuto kamili

2. Kuvumilia taabu na mateso katika maisha

3. Kuvishinda vishawishi na majaribu

4. Kusali sala mbalimbali

5. Kuomba Misa kwa ajili hiyo.

6. Kusoma neno la Mungu na kulitafakari na kulinganisha na maisha yetu ya kila siku

7. Utakaso wa Toharani kama adhabu hizi hazikuondolewa duniani


πŸ‘‰β” Kipimo cha Rehema ni nini?

Kipimo cha Rehema hutegemea uzito wa majuto na mapendo mtu aliyonayo kwa Mungu Muumba wake. (1Kor 9:11)


πŸ‘‰β” Mtu akitaka kupata Rehema za Kanisa Katoliki yampasa nini?

Mtu akitaka kupata Rehema za Kanisa Katoliki yampasa;

1. Kujua na kufuata utaratibu unaotolewa na Kanisa Katoliki wa kupata Rehema

2. Awe katika hali ya neema ya Utakaso

3. Kufanya matendo yote yanayotakiwa kwa kupata rehema hiyo, kwa mfano;

a). Hija au Kuhiji katika mwaka wa Jubilei katika Kanisa lililo teuliwa na Askofu
b). Kufanya mafungo - Kama vyama vya kitume
c). Kuzuru makaburi (Kutembelea) yaliyobarikiwa
d). Katika hatari ya kufa padri hutoa rehema pamoja na Sakramenti ya wagonjwa
e). Kusali kwa nia za Baba Mtakatifu

Chagua aina ya mada ya maswali unayotaka kusoma hapa..

NI-VIZUR-KUMSIFU-MARIA-AU.JPG

πŸ™‰πŸ™‰πŸ™‰Usisahau kushare makala hii kuhusu Maswali na majibu kuhusu Neema na Rehema.πŸ‘ Share facebook, twitter n.k bila kusahau WhatsApp!πŸ’―βœ”


images-20.jpeg

Ujumbe wangu kwako kwa sasa

Sala ni Hazina. Kusali ni muhimu sana. Sala unayosali leo inaweza kukusaidia hata miaka kumi ijayo au ikasaidia watoto wa watoto wako. Mungu ni mwenye fadhila na anakumbuka yote. Mwombe Mungu akulinde ukiwa mzima ili uwapo hatarini akukumbuke hata kabla hujamwomba.

Mungu Akubariki Daima… Tuombeane!

πŸ“š Endelea kusoma kuhusu;-πŸ‘‡

JE-MARIA-NI-MAMA-YETU-PIA.JPG
IMG_20180108_172800.jpg

Kama Una mashaka na Imani na mafundisho ya Kanisa Katoliki soma hapa>>

Website hii inaletwa kwako na Melkisedeck Leon Shine,