Maswali na majibu kuhusu Misa Takatifu ya Kanisa Katoliki
πβ Ishara ndogo ya Msalaba juu ya panda la uso, mdomo, na kifua kabla ya Injili ina maana gani?
Maana yake ni kama Ahadi kuwa, Niko tayari kulifahamu Neno la Mungu kwa akili yangu, Nitalitangaza kishujaa kwa Midomo yangu, Nitalipenda na kulishika kwa Moyo wangu wote.
πβ Je ni dhambi kukosa Misa Jumapili?
NDIYO. Ni dhambi kubwa kukosa Misa kwa Makusudi siku ya Jumapili/Dominika na Sikukuu zilizoamriwa.
πβ Sakramenti ya Ekaristi ni nini?
Sakramenti ya Ekaristi ni Sakramenti ya Mwili na Damu ya Yesu Kristo, aliye kweli katika Maumbo ya Mkate na Divai. (Yoh 6:1-17, Mt 26:26-28)
πβ Ni wakati gani katika Misa Mkate na Divai vinageuka Mwili na Damu yake Kristo?
Ni katikati ya Misa padri asemapo maneno Matakatifu aliyosema Yesu mwenyewe: "HUU NDIO MWILI WANGU; HII NDIO DAMU YANGU" (Lk 14:22-26).
πβ Je Sakramenti ya Ekaristi hujulikana kwa majina yapi?
Majina haya;
1. Ekaristi Takatifu
2. Karamu ya Bwana
3. Misa Takatifu
4. Sakramenti Takatifu ya Altare
5. Komunyo Takatifu
6. Sadaka Takatifu
7. Kumega Mkate
πβ Baada ya Mitume kufa ni nani wanafanya Sakramenti ya Ekaristi
Badaa ya Mitume kufa Maaskofu na Mapadri wanaendelea kuadhimisha Sakramenti ya Ekaristi Takatifu
πβ Ni lini Yesu Kristo aliwapa Maaskofu na Mapadri Uwezo wa kugeuza mkate na divai kuwa Mwili na Damu yake?
Yesu Kristo aliwapa Maaskofu na Mapadri Uwezo wa kugeuza mkate na divai kuwa Mwili na Damu yake alipowafanya Mitume kuwa Mapadri katika karamu ya mwisho aliposema "FANYENI HIVI KWA UKUMBUSHO WANGU" (Lk 22:14-20)
πβ Misa ni nini?
Misa ni sadaka safi ya Wakristo kwa Mungu, ndiyo sadaka ya Agano Jipya ambayo Kristo kwa njia ya Padri anamtolea Mungu Baba mwili na damu yake katika umbo la mkate na divai kama alivyojitolea mwenyewe juu ya msalaba.
πβ Sadaka ya Msalaba ni nini?
Sadaka ya Msalaba ni tendo la mateso na kifo cha Bwana wetu Yesu Kristojuu ya Msalaba pale Kalvari
πβ Ni kwa nini Sadaka ya Misa Takatifu ni Sadaka ile ile ya Msalaba?
Sadaka ya Misa Takatifu ni ile ile ya Msalaba kwa sababu ni sadaka moja tu, kuhani na kafara ni yule yule. Tofauti ni namna tu yankuitoa hiyo sadaka. (1Kor 11:26, Ebr 9:14,25-28)
Pale msalabani damu ilimwagika lakini katika Ekaristi damu haimwagiki tena
πβ Misa Takatifu hutolewa kwa nani?
Misa Takatifu hutolewa kwa Mungu Baba Mwenyezi (Ebr 5:1-10, Law 9:7).
πβ Yesu aliweka sadaka ya Misa Takatifu kwa makusudi gani?
Yesu aliweka sadaka ya Misa Takatifu ili;
1. Amtolee Baba sadaka bora siku zote
2. Atujalie mastahili yake Msalabani
3. Azilishe roho kwa neema za sadaka hiyo. (Ebr 5:1-10, 7:27).
πβ Sadaka ya Misa Takatifu yatolewa kwa nia gani?
Sadaka ya Misa Takatifu yatolewa kwa nia ya kumwabudu Mungu, kumshukuru, kujipatanisha nae na kumwomba. (Ebr 9:14)
πβ Misa Takatifu hutolewa kwa ajili ya nani?
Misa Takatifu hutolewa kwa ajili ya kanisa nzima yaani kwa ajili ya watu wote wazima na wafu. (Ebr 9:14. Rum 1:9)
πβ Kutolea Misa kwa Marehemu maana yake ni nini?
Kutolea Misa kwa Marehemu ni kutolea Misa kwa ajili ya roho zilizoko toharani ili ziweze kuingia mbinguni
πβ Misa Takatifu ina sehemu kuu ngapi?
Misa Takatifu ina sehemu kuu mbili
1. Litrujia ya Neno
2. Liturujia ya Ekaristi
πβ Litrujia ya Ekaristi ina sehemu kuu ngapi?
Litrujia ya Ekaristi ina sehemu kuu tatu
1. Matayarisho ya vipaji
2. Sala ya Ekaristi
3. Ibada ya Komunyo
πβ Ni vitu gani vya msingi na vya lazima katika kuadhimisha Ekaristi Takatifu?
Vitu vya lazima katika kuadhimisha Ekaristi Takatifu ni
1. Mkate wa Ngano
2. Divai ya mzabibu
πβ Kabla ya Kupokea Ekaristi Takatifu Tunasali sala gani?
Tunasali "Ee Bwana sistahili uingie kwangu lakini sema neno tu na roho yangu itapona"
πβ Katika Ekaristi Takatifu Tunampokea nani?
Katika Ekaristi Takatifu Tunampokea Yesu Kristo Katika Maumbo ya Mkate na Divai na tunaungana naye (Yoh 6:57)
πβ Mkristo awe katika hali gani kabla ya kupokea Ekaristi Takatifu?
1. Awe na Neema ya Utakaso yaani asiwe na dhambi ya mauti
2. Awe na Imani, Ibada na Kumtamani Yesu
3. Afunge chakula Muda wa saa Moja na Kileo zaidi ya masaa matatu
4. Awe safi kimwili
5. Awe na adabu na heshima
πβ Komunyo Takatifu Hutuletea neema gani?
1. Hulinda na kuongeza neema ya Utakaso iliyo uzima wa roho zetu
2. Hutuondolea dhambi ndogo na kupunguza hatari ya kutenda dhambio kubwa
3. Hututia bidii na nguvu ya kutenda mema kwa kutuongezea Imani, Matumaini na Mapendo
4. Huleta Umoja katika Kanisa, sio sisi na Kristo tuu bali sisi kwa sisi.
πβ Mkristo akipokea Ekaristi Takatifu akiwa na dhambi rohoni anatenda dhambi gani?
Mkristo akipokea Ekaristi Takatifu akiwa na dhambi anatenda dhambi kubwa yaani kufuru Sakramenti. (1 Kor 11;29)
πβ Je, Kanisa linahimiza waamini wapokee Ekaristi wakati gani?
Kanisa linahimiza waamini wapokee Komunyo Takatifu kila siku wanaposhiriki Misa
πβ Nani Mhudumu wa adhimisho la Ekaristi Takatifu?
Mhudumu wa adhimisho la Ekaristi Takatifu ni Askofu na Padre
πβ Je, Mkristo akipokea kipande cha Hostia amempokea Yesu Mzima?
Ndiyo, Amempokea Yesu Mzima kabisa, Hata akipewa zaidi ya hostia moja amempokea Yesu Mzima
πβ Sakramenti ya Ekaristi Takatifu Huifadhiwa wapi?
Sakramenti ya Ekaristi Takatifu Huifadhiwa kwenye Tabernakulo
πβ Tabernakulo ni nini?
Tabernakulo ni mahali Patakatifu anapokaa Yesu wa Ekaristi siku zote
πβ Sakramenti ya Ekaristi Takatifu hukaa Tabernakulo kwa sababu gani
Sakramenti ya Ekaristi Takatifu hukaa Tabernakulo kwa ajili ya watu wote hasa wagonjwa
πβ Ishara wazi ya Sakramenti ya Ekaristi Takatifu ni nini?
Ishara wazi ya Sakramenti ya Ekaristi Takatifu ni maumbo ya mkate na divai, na maneneo ya mageuzo ya Yesu mwenyewe Padri akiyatamka.
πβ Baada ya kumpokea Yesu wa Ekaristi tufanye nini?
Baada ya kumpokea Yesu wa Ekaristi: Tumwabudu,tumshukuru, tumwombe kwani yeye ni Mwenyezi. (Mt 2:11, Lk 17:11)
Chagua aina ya mada ya maswali unayotaka kusoma hapa..
amri_kumi
amri_ya_kumi
amri_ya_kwanza
amri_ya_nane
amri_ya_nne
amri_ya_pili
amri_ya_saba
amri_ya_sita
amri_ya_tano
amri_ya_tatu
amri_ya_tisa
amri_za_kanisa
asili
biblia
bikira_maria
daraja
dhambi
dhamira
ekaristi
fumbo
habari_njema
hukumu
huruma
ibada
ishara
ishara_ya_msalaba
kanisa
karama
katekesi
katoliki
kifo
kipaimara
kitubio
kuabudu
liturujia
maana
madhehebu
malaika
mapokeo
marehemu
misa
mitume
mpako_wa_wagonjwa
mtu
mungu
ndoa
neema
rehema
roho_mtakatifu
sakramenti
sala
sanamu
toharani
ubatizo
ufufuko
ufufuo
ufunuo
umwilisho
utatu_mtakatifu
utawa
uumbaji
uzima_wa_milele
vilema
visakramenti
vishawishi
wafu
watakatifu
yesu
πππUsisahau kushare makala hii kuhusu Maswali na majibu kuhusu Misa Takatifu ya Kanisa Katoliki.π Share facebook, twitter n.k bila kusahau WhatsApp!π―β
Ujumbe wangu kwako kwa sasa
Kama mtu anasali kila siku katika maisha yake hakuna kitu kitakachokuwa kigumu. Sala ni njia ya kujipatia neema za kuendesha maisha yetu. Usiache kusali kila siku hata kama upo katika hali gani.
Mungu Akubariki sana… Tuombeane!
π Endelea kusoma kuhusu;-π
Chagua aina ya mafundisho unayotaka kusoma hapa..
amri_kumi
amri_ya_kumi
amri_ya_kwanza
amri_ya_nane
amri_ya_nne
amri_ya_pili
amri_ya_saba
amri_ya_sita
amri_ya_tano
amri_ya_tatu
amri_ya_tisa
amri_za_kanisa
asili
biblia
bikira_maria
daraja
dhambi
dhamira
ekaristi
fumbo
habari_njema
hukumu
huruma
ibada
ishara
ishara_ya_msalaba
kanisa
karama
katekesi
katoliki
kifo
kipaimara
kitubio
kuabudu
liturujia
maana
madhehebu
malaika
mapokeo
marehemu
misa
mitume
mpako_wa_wagonjwa
mtu
mungu
ndoa
neema
rehema
roho_mtakatifu
sakramenti
sala
sanamu
toharani
ubatizo
ufufuko
ufufuo
ufunuo
umwilisho
utatu_mtakatifu
utawa
uumbaji
uzima_wa_milele
vilema
visakramenti
vishawishi
wafu
watakatifu
yesu
Post preview:
Close preview