YESU%20MFALME%20WA%20HURUMA.gif

Blog kwa Wakatoliki

Mpangilio wa kurasa Kwa Wakatoliki ndani ya AckySHINE

|| HOME || MAKALA || TAFAKARI || SALA || MAFUNDISHO || MIUJIZA || WATAKATIFU || NYIMBO || PICHA ||

.

๐Ÿ‘‰ MASOMO YA MISA, MACHI 27, 2016 SIKUKUU YA PASAKAโœ…

SOMO 1

Mdo. 10:34, 37- 43

Petro akafumbua kinywa chake, akasema, Jambo lile ninyi mmelijua, lilionea katika Uyahudi wote likianzia Galilaya, baada ya ubatizo aliohubiri Yohane; habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu; naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu aikuwa pamoja naye. Nasi tu mashahidi wa mambo yote yaliyotendeka katika nchi ya Wayahudi na katika Yerusalemu; ambaye walimwua wakamtundika mtini. Huyo Mungu alimfufua siku ya tatu, akamjalia kudhihirika, si kwa watu wote, bali kwa mashahidi waliokuwa wamekwisha kuchaguliwa na Mungu, ndiyo sisi, tuliokula na kunywa naye baada ya ufufuka kwake kutoka kwa wafu. akatuagiza tuwahubiri watu na kushuhudia ya kuwa huyu ndiye aliyeamriwa na Mungu awe mhukumu wa wahai na wafu. Huyo manabii wote humshuhudia, ya kwamba kwa jina lake kila amwaminiye atapata ondoleo la dhambi.

Neno la Bwanaโ€ฆ Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 118:1-2, 16-17, 22-23.

K. Siku hii ndiyo aliyoifanya Bwana,
Tutashangilia na kuifurahia.

Aleluya.
Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema
kwa maana fadhili zake ni za milele.
Israeli na aseme sasa,
Ya kwamba fadhili zake ni za milele. (K)

Mkono wa kuume wa Bwana umetukuzwa;
Mkono wa kuume wa Bwana hutenda makuu.
Sitakufa bali nitaishi,
Nami nitayasimulia matendo ya Bwana. (K)

Jiwe walilolikataa waashi
Limekuwa jiwe kuu la Pembeni.
Neno hili limetoka kwa Bwana,
Nalo ni ajabu machoni petu (K)

SOMO 2

Kol. 3:1-4

Mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu, Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu

Neno la Bwanaโ€ฆ Tumshukuru Mungu.

INJILI

Yn. 20:1-9.

Hata siku ya kwanza ya juma Mariamu Magdalena alikwenda kaburini alfajiri, kungali giza bado; akaliona lile jiwe limeondolewa kaburini. Basi akaenda mbio, akafika kwa Simoni Petro na kwa yule mwanafunzi mwingine ambaye Yesu alimpenda, akawaambia, wamemwondoa Bwana kaburuni, wala hatujui walipomweka. Basi Petro akatoka, na yule mwanafunzi mwingine , wakashika njia kwenda kaburini wakaenda mbio wote wawili; na yule mwanafunzi wengine akaenda mbio upesi kuliko Petro, akawa wa kwanza wa kufika kaburini. Akainama na kuchungulia, akaviona vitambaa vya sanda vimelala; lakini hakuingia. Basi akaja Simoni Petro akimfuata, akaingia ndani ya kaburi; akavitazama vitambaa vilivyolala; ile leso iliyokuwako kichwani pake; haikulala pamoja na vitambaa, bali imezogwazogwa mbali mahali pa peke yake. Basi ndipo alipoingia naye yule mwanafunzi mwingine aliyekuwa wa kwanza wa kufika kaburini, akaona na kuamini. kwa maana hawajalifahamu bado andiko, ya kwamba imempasa kufufuka

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo

๐Ÿ™‰Usisahau kushare posti hii Kuhusu ๐Ÿ‘‰MASOMO YA MISA, MACHI 27, 2016 SIKUKUU YA PASAKA, Shareโœ” Facebook, Twitter bila kusahau WhatsApp n.k..๐Ÿ’ฏโœ…
[WIMBO๐ŸŽถ]๐Ÿ‘‰๐ŸŽผPenye pendo๐ŸŽน
[WIMBO๐ŸŽถ]๐Ÿ‘‰๐ŸŽผFamilia Takatifu๐ŸŽน

๐Ÿ“š Endelea kusoma kuhusu;-๐Ÿ‘‡

Huruma ya Mungu ni ya Milele na Upendo wake ni Wa DAIMA!

Mungu ni mwenye Huruma, Rehema na Neema. Anataka watu wote waokolewe na Wala sio Hakimu na Mtoa Adhabu. Soma zaidi...

Mimi naitumainia Huruma ya Mungu
Wewe je?

Ifahamu Huruma ya Mungu hapa>>>

Karibu uonje Huruma ya Mungu Baba yetu iliyo tunda la Upendo wake Mkuu Kwetu. Utasitasita mpaka lini? Wakati wa Kubadili Maisha ni sasa

Soma zaidi kuhusu Huruma ya Mungu Hapa na jinsi ya kuipokea na kuitumainia>>>

.

Kichekesho%20Kipya Usikose ๐Ÿ“•Kitabu cha Mbinu za Kilimo Bora Cha Mboga๐ŸŒฟ๐Ÿ… Kina kurasa 100 na utaalamu wa mazao zaidi ya 10
๐Ÿ‘‰Bofya hapa KuchukuaKizuri

.

Kichekesho%20Kipya Usikose ๐Ÿ“•Kitabu cha Vichekesho Vikuu Vikali 300+โœ” Kina kurasa 270 zenye picha๐Ÿ“ท na vichekesh๐Ÿ˜‚ zaidi ya 300๐Ÿ’จ
๐Ÿ‘‰Bofya hapa KuchukuaKizuri

.

.

.

.

.

.