Mambo yanayorudisha kwaya Katoliki nyuma

By, Melkisedeck Shine.

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

Mambo yanayorudisha kwaya Katoliki nyuma

MATATIZO YANAYORUDISHA UIMBAJI WA KWAYA KATOLIKI NYUMA.
1.Kuwaimbia binadamu.Yaani tupo kwa ajili ya kuimba ili tusifiwe na watu.

2.Kuimba bila tafakari.Mara nyingi tunaimba tu bila kuzingatia ujumbe Wa ule wimbo

3.Kuimba bila kusali!Yasemekana Kuimba ni kusali Mara mbili.Waimbaji wengi hukariri wimbo na nyimbo nyingi zimetungwa kwa njia ya sala lakini wanakwaya wengi huimba tu wala hali ya sala haimo ndani yao!

4.Walimu wenye hasira na ubinafsi.Mkufunzi Wa kwaya ni nguzo muhimu kwa maendeleo ya uimbaji.Iwapo choirmaster ni mwenye vurugu, mchochezi na mpenda fitina, bila shaka itakuwa vigumu kwa kwaya kupiga hatua kiuimbaji!

5.Sheria Kali zisizoenda na maadili ya kanisa.Kila jamii INA sheria zake na sheria ni nzuri.lakini tukiwa na sheria zinazowakandamiza wengine, tutapoteza kondoo wengi badala ya kuwaleta kwa Mungu!

6.Utoaji Wa albamu au kurekodi nyimbo kwa nia ya kutafuta pesa au kigezo kwa kwaya.Kwaya nyingi zimeanguka pindi tu wanapotoa albamu ya kwanza!Maana tunakosa kufahamu kuwa sisi ni wainjilisiti na tunawasaidia mapadri wetu kuhubiri injili.

7.Kutotii viongozi Wa kanisa.Wanakwaya wanaokosa kufahamu kuwa wapo chini ya viongozi na kanisa husika Mara nyingi hujipata wakiwa kwa makosa bila kunuia!

8.Kutoishi kwa hali ya sakramenti!Kama kuna jambo kubwa ambalo ibilisi hufurahia, ni yule MTU anayeishi katika maisha ya ndoa isiyo halali mbele za Mungu.Yaani Maana yake unaishi na mke au Mme bila ndoa ya kanisa na huna kizuizi chochote kinachokufanya usipate sakramenti hiyo.

9.Kitubio.Wengi tunapokea sakramenti ya ekaristi katika hali ya dhambi na hatushughuliki kabisaa kwenda kitubio.Hii inachochea zaidi kuwepo kwa dhambi za mazoea katika maisha yetu!

10.Kutosali kila siku.Inakuwa rahisi kwetu sisi kujaribiwa tukiwa hatusali.Kuimba kwako kunawasha hasira za shetani kwa hivo usiposali, bila shaka atarudi kulipiza kisasi.Fwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya Mambo yanayorudisha kwaya Katoliki nyuma

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; Mambo yanayorudisha kwaya Katoliki nyuma

a.gif Maana ndefu ya Ishara ya msalaba

_Ishara ya msalaba ina maana ndefu sana!_.. soma zaidi

a.gif Mafundisho na mapokeo Katika Kanisa Katoliki yanapopatikana kwenye Biblia

JE IMANI AU MAPOKEO YA KANISA KATOLIKI YANAPATIKANA KATIKA BIBLIA?.. soma zaidi

a.gif Neno la hekima la leo

HEKIMA YA LEO.. soma zaidi

[Wimbo Mzuri PA.gif] Maria Bikira

[Tafakari ya Sasa] 👉Upendo wa Mungu

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Juan Diego

[Jarida La Bure] 👉ROZARI YA MAMA BIKIRA MARIA

UJUMBE-WA-MSAMAHA-KWA-NDUGU.JPG

a.gif Uelewa wa namba katika Biblia

Biblia imeandikwa na Mungu kupitia waandishi wanadamu kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu. Hivyo Biblia ni Neno la Mungu. Hivyo mwandishi wa Biblia ni Mungu kupitia wanadamu (God is the primary author of the Bible while human authors are secondary authors). Mungu aliwavuvia (inspiration by the Holy Spirit) waandishi wanadamu ili waweze kuandika kile tu ambacho Yeye (Mungu) alitaka kiandikwe kwa ajili ya wokovu wa wanadamu. Kusema kuwa Biblia imeandikwa na Mungu kupitia wanadamu haina maana ya kuandikwa kwa njia ya imla (dictation), kana kwamba Mungu anataja sentensi au neno na wao wanaandika. Hapana, pamoja na kuwavuvia Roho Mtakatifu, waandishi wanadamu walikuwa huru kutumia vipawa mbalimbali vya uandishi na mazingira yao ili kufikisha ujumbe ambao Mungu amewavuvia. Hivyo walikuwa “active writers of the Bible, and not passive writers.” Walitumia akili (reason), utashi (will), ujengaji picha (imagination) na vipawa vingine. Lakini vipawa hivi vyote vilikuwa chini ya maongozi ya Roho Mtakatifu ili kuwawezesha waandishi wa Biblia kufikisha ujumbe kwa ufasaha bila makosa… soma zaidi

a.gif Askofu ampaje Mkristo Kipaimara?

Kwanza ananyoosha Mikono juu yake akimwombea mapaji saba ya Roho Mtakatifu… soma zaidi

a.gif Hagari na Ishmaeli (Mtoto wa kwanza wa Abrahamu alivyopatikana)

1 Basi Sarai mkewe Abramu hakumzalia mwana, naye alikuwa na mjakazi, Mmisri, jina lake Hajiri… soma zaidi

a.gif Jumamosi ya kwanza ya mwezi

Kila Jumamosi ya Kwanza ya Mwezi tunaadhimisha nini?.. soma zaidi

a.gif "Aleluya" katika sala, hasa zaburi ina maana gani?

"Aleluya" katika sala, hasa zaburi ina maanisha "Msifuni Mungu".. soma zaidi

a.gif Safari ya kupata fadhila ya Unyenyekevu

Leo tunatafakari kuhusu safari ya kupata fadhila ya Unyenyekevu,.. soma zaidi

a.gif Bikira Maria Katika dini ya Kiislamu

Kurani inamtaja mwanamke mmoja tu, tena mara 34: ni Mariamu, mama wa nabii Isa. Akichanganywa na dada wa Haruni na Musa, aliyekuwa na jina hilohilo, anatajwa kama binti Imrani. Pia habari nyingine kadhaa zinapishana na zile za Injili… soma zaidi

a.gif Baba wa Yesu Kristo ni nani?

Baba wa Yesu Kristo ni Mungu Mwenyewe.. soma zaidi

a.gif Mafuta ya mpako wa wagonjwa yanamaanisha nini?

Mafuta ya wagonjwa yanamaanisha lengo la kuwaponya na kuwarudishia nguvu na uzuri… soma zaidi

a.gif Mungu ajua yote maana yake nini?

Mungu ajua yote maana yake ajua ya sasa, ya zamani na ya wakati ujao hata mawazo yetu.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.