YESU%20MFALME%20WA%20HURUMA.gif

Blog kwa Wakatoliki

Mpangilio wa kurasa Kwa Wakatoliki ndani ya AckySHINE

|| HOME || MAKALA || TAFAKARI || SALA || MAFUNDISHO || MIUJIZA || WATAKATIFU || NYIMBO || PICHA ||

.

👉 Maelezo kuhusu Ekaristi Takatifu

Melkisedeck

Msomaji wangu mpendwa, asante kwa kuendelea kupenda kutembelea blog hii. Baada ya kukuandalia makala kuhusu;

Leo nimekutayarishia makala kuhusu Maelezo kuhusu Ekaristi Takatifu.

Maelezo kuhusu Ekaristi Takatifu

⛪1. Ekaristi ni nini?
Ekaristi ni Sakramenti ya Mwili na Damu ya Yesu Kristo, katika
maumbo ya mkate na divai. Sakramenti hii
iliwekwa na Yesu Mwenyewe kwenye karamu ya mwisho, siku ya Alhamisi jioni kabla ya mateso
yake. (Yoh 6:1-71; Mt 26:26-28).

2. Maana ya jina Ekaristia
Tendo la shukrani na baraka.
Jina Ekaristi limetokana na neno la Kigiriki,
εύχαριστείν, maana yake ni “tendo la shukrani”,
“ kutoa shukrani*”, (Lk 22:19; 1Cor 11:24).
Ni tendo ambalo Yesu analifanya kwa Mungu.
Anamshukuru Mungu kwa kukamilisha kazi ya ukombozi. Tendo la baraka – εύλογείν

Kulingana na utamaduni wa Wayahudi baraka ilkua ikitolewa wakati wa mlo ikitukuza kazi za up mbaki za Mungu (Mt 26:26; Mk 14:22).

3. Injili zinazoongelea kuwekwa kwa Ekaristi

Injili tatu zinatueleza jinsi Yesu Kristo alivyoweka
Ekaristi Takatifu:
Mt 26:26-28.
Mk 14: 22-24
Lk 22:19-20

Mwinjili Yohane anaeleza Yesu Kristo mkate wa
uzima. Sura ya sita.

4. 1Kor 11:23-25
Mtume Paulo anatueleza jambo hilo katika Waraka wa kwanza kwa Wakorintho. 1Kor
11:23-25.
5. Tunajifunza kutoka kwa Yesu mambo
yafuatayo Lk 22:1. Saa ya Yesu (Lk 22:14). Hapa hamaanishi
saa ya kula, hapana. Bali saa ile ile ya kutimiliza tendo la wokovu. Yohane anapenda kusema saa ya kumtukuza Mungu, saa ya kupita kutoka ulimwengu huu kwenda kwa Baba. Sisi tunaweza kusema, tuna saa maalum ya kuingia katika ulimwengu wa
roho.Saa ya kukutana na Mungu, kutoka
ulimwengu huu kwenda kwa Mungu. (Sala au kifo).

2. Shukrani na masifu kwa Baba (Lk 22:17).

3. Kugawana sisi kwa sisi kikombe cha kwanza (Lk 22:17).

4. Kumbukumbu ya sadaka yake ya wokovu (Lk 22:19).

5. Uwepo wake (Lk 22:19).

6. Damu yake imemwagika kwa ajili yetu, kikombe cha pili (Lk 22:20).

Ekaristi ni Baraka kuu:
Yesu anabariki –kazi ya wokovu inabarikiwa na Yesu Mwenyewe. Hata vitu tunavyovitumia kila siku ni lazima kuviombea
baraka. Kabla ya mageuzo mkate na divai vinaombewa baraka (Mt 26:26).

Yesu anajitoa mwenyewe kwa watu –Yesu anajitoa kwa kila mshiriki (Mt 26:26).

5. *Matunda ya Ekaristi katika maisha ya mkristo.**

1. Muungano na Kristo:
Ekaristi inatuunganisha na Kristo kwa muungano wa ndani kabisa (Yoh 6:56).

2. Uzima wa milele : Ekaristi ni chanzo cha
uzima, maisha yetu yote yanapata uzima kwa kushiriki Mwili na damu ya Kristo, (Yoh 6:57).

3. Umoja: Ekaristi inaleta umoja wa kweli.
Tunafanywa kuwa mwili mmoja (1Kor 10:16-17).

4. Huondoa dhambi: Inatuondolea kwa
kuzifuta dhambi ndogo au inatutenga na dhambi ndogo (Mt 26:28; Yoh 1:29). Sakramenti ya
kitubio ndio hasa huondoa dhambi za mauti
(1Yoh 1:7; Yoh 20:22-23).

5. Dawa ya kutuponya kutoka katika umauti:
Ekaristi ni dawa ya kutokufa (Yoh 6:57-58).

6. Kufufuliwa siku ya mwisho: (Yoh 6:54).

6.Nguvu ya Ekaristi
–Kuponywa kwa
kuondolewa dhambi zetu.
Nguvu za Mungu zimo katika Ekaristi. Kabla ya kupokea Ekaristi tunasali Ee Bwana siesta hili uingie kwangu lakini sema neno tu na roho yangu
itapona. Bila shaka litakuwa kosa kubwa kwetu sisi kufikiri kwamba uponyaji unahusu masuala ya
mwili tu. Si kila uponyaji ni uponyaji wa mwili.

Mtume Paulo katika Waraka wa kwanza kwa Wathesalonike sura ya 5:23 kuwa sisi wanadamu tu mwili, roho na nafsi . Hivyo tunaweza kuponywa nafsi zetu na roho zetu. Hata kama uponyaji haujanja katika mwili.

Lakini mara nyingi ukitokea uponyaji wa ndani basi matokeo
yake utayaona hata kimwili. (anima sana in
corpore sano) (Roho yenye afya katika mwili
wenye afya)

1. Ekaristi Takatifu inayalinda maisha ya
kimanga ya roho tuliyoyapokea wakati wa Ubatizo
, kwa kupata anayekomunika nguvu za kimungu za kupambana na vishawishi, na
kudhoofisha nguvu za tamaa. Inaimarisha uhuru wa mapenzi ya nafsi zetu wa kuhimili
mashambulizi ya shetani.

2. Ekaristi Takatifu inaongeza maisha ya
neema ambayo tayari tunayo. Hufanya hivyo kwa kuhuisha fadhila na vipaji vya Roho Mtakatifu
tulivyonavyo.

3. Ekaristi Takatifu inayatibu magonjwa ya kiroho ya nafsi kwa kuziondoa dhambi ndogo na kumkinga mtu na adhabu ndogo ndogo za kidunia
zitokanazo na dhambi. Ondoleo la dhambi ndogo na mateso ya muda yasababishwayo na dhambi hizi hufanyika mara moja kwa sababu ya upendo
kamili kwa Mungu ambao huamshwa kwa
kuipokea Ekaristi. Ondoleo la dhambi hizi
hutegemea kiasi cha upendo unaoelekezwa
kwenye Ekaristi (Lk 7:47).

4. Ekaristi Takatifu inatupa furaha ya kiroho tunapomtumikia Kristo, tunapotetea njia yake,
tunapotekeleza majukumu yetu ya maisha, na kufanya sadaka zetu zinazotukabili zile ni katika kuiga maisha ya Mwokozi wetu.

🙏Tumsifu Yesu Kristu

💞Ave Maria 💕

Melkisedeck

Nitumie Maoni yako Kuhusu Maelezo kuhusu Ekaristi Takatifu hapa

Jina
Dini/dhehebu
Mfano Mwislamu, Katoliki, Lutherani, Mlokole n.k
Email
Itatumika kukujibu
Maoni yako


🙉Usisahau kushare posti hii Kuhusu 👉Maelezo kuhusu Ekaristi Takatifu, Share✔ Facebook, Twitter bila kusahau WhatsApp n.k..💯✅

📚 Endelea kusoma kuhusu;-👇

Huruma ya Mungu ni ya Milele na Upendo wake ni Wa DAIMA!

Mungu ni mwenye Huruma, Rehema na Neema. Anataka watu wote waokolewe na Wala sio Hakimu na Mtoa Adhabu. Soma zaidi...

Mimi naitumainia Huruma ya Mungu
Wewe je?

Ifahamu Huruma ya Mungu hapa>>>

Karibu uonje Huruma ya Mungu Baba yetu iliyo tunda la Upendo wake Mkuu Kwetu. Utasitasita mpaka lini? Wakati wa Kubadili Maisha ni sasa

Soma zaidi kuhusu Huruma ya Mungu Hapa na jinsi ya kuipokea na kuitumainia>>>

.

.

.

Melkisedeck

Tumsifu Yesu Kristu…

Jina langu ni Melkisedeck L. Shine. Mimi ni Mkristu Mkatoliki
Karibu Katika Blog yangu ya Kikatoliki mahali pa kusoma makala mbalimbali za Kikatoliki, sala, Tafakari, Picha za Katoliki pamoja na nyimbo za Kikatoliki

Blog ya AckySHINE Kwa Wakatoliki ni Blog pekee ya Kiswahili ya Kikatoliki kwa posti nyingi, isiyochosha kusoma, yenye posti nyingi nzuri mpya kila saa unapotembelea. Unahakikishiwa kupata kitu kipya utakachopenda kila unapotembelea blog hii, Utapata makala za Kikatoliki, sala, Tafakari, Picha za Katoliki, nyimbo za Kikatoliki n.k. Kwa sasa kuna posti Mpya 1179 za Kikatoliki kwa ajili yako, nimekutayarishia kila kitu kazi yako ni kuperuzi na kutembelea Blog hii mara kwa mara.

Chagua unachotaka hapa…

|| MAKALA || TAFAKARI || SALA || MAFUNDISHO || MIUJIZA || WATAKATIFU || NYIMBO || PICHA ||

Usisite kuniandikia maoni,mapendekezo au maswali hapa

Jina
Dini/dhehebu
Mfano Mwislamu, Katoliki, Lutherani, Mlokole n.k
Email
Itatumika kukujibu
Maoni yako

Karibu tena na Mungu Akubariki

Nakutakia pasaka njema

ABOUT ME | MY PERSONAL BLOG

.