Maana ya siku ya Jumatano ya Majivu

Tumsifu Yesu Kristu…

Karibu tena katika Website yako uipendayo ya Wakatoliki yenye mambo mengi kuhusu Imani na Mafundisho ya Kikatoliki. Kama una wasiwasi kuhusu Imani ya Kanisa Katoliki nimekuandalia makala maalumu ya kukufunulia Ukweli hapa>>.

Mpendwa Msomaji, baada ya kukuandikia makala nzuri inayopendwa kuhusu; Kujitambua Mbele ya Mungu, kwa sasa nimekuandalia makala hii kuhusu;

Maana ya siku ya Jumatano ya Majivu.

Unaweza pia kupokea makala zote mpya zinazopostiwa hapa kwenye email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo.

Endelea kuelimika na kubarikiwa kila siku unapotembelea tovuti hii.

Maana ya siku ya Jumatano ya Majivu

By, Melkisedeck Shine.

Utangulizi

Wakati umetimia na ufalme wa Mungu umekaribia, tubuni na kuiamini Injili, (Mk 1:15), haya ndiyo maneno ya kwanza ya Yesu ambayo kadri ya Mwinjili Marko yanafungua kazi ya hadhara ya Yesu, kwa maana hiyo kazi ya Yesu inaanza kwa kuwaandaa watu katika toba ili hatimaye, wapate kuukaribia au kuingia katika ufalme wa Mungu.

Na wakati ndiyo sasa. Wakati ni sasa, Yesu anatuhubiria na Kwaresima imewadia, na ndiyo maana siku ya Jumatano ya majivu, kwa kuitikia mwito wa maneno ya Yesu kanisa linatualika kuingia katika kipindi cha Kwaresma, ambacho ni kipindi cha kujikusanya, kujitayarisha, kijitengeneza na kujikarabati hasa kwa toba, kufunga, kusali na kujitoa sadaka zaidi mambo yanayorutubishwa kwa tafakari ya kina ya Neno la Mungu.

Nini maana ya Jumatano ya majivu?

Jumatano ya majivu ni mwanzo wa kipindi cha kwaresima katika kanisa, Ni mwanzo wa siku arobaini za kutafakari kwa undani fumbo kuu la upendo wa Mungu linalofunuliwa kwa kujitoa kwake na kufa msalabani, kifo cha aibu cha Msalaba ili kuichukua aibu yetu au dhambi zetu.

Kwaresma ni nini?

Kwaresma ni kipindi cha siku 40 cha kujiandaa kuadhimisha Sherehe kuu ya PASAKA yaani kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Tunajiandaa kwa Kufunga Kusali, Kutubu, na Matendo mema.
Mama kanisa anatupatia kipindi hiki ili tuweze kutafakari njia na mienendo yetu na kubadilika kama haimpendezi Mungu

Tunapofunga tunatakiwa kuzuia vilema vyetu na kuviacha kabisa, tunaomba kujaliwa moyo wa toba, tunainua mioyo yetu na tunaomba Mungu atujalie nguvu na tuzo. Haitoshi tu kukiri makosa yetu bali tunahimizwa kuungama na kutubu hayo makosa na kuwa tayari kuanza upya. Kipindi cha Kwaresima huanza tangu Jumatano ya majivu. Mwanzoni mwa kazi yake ya kuhubiri Habari njema Yesu anaanza kwa kusema tubuni na kuiamini Injili – Mk 1,15. Maneno haya haya tunayasikia/tumeyasikia kila tunapopakwa majivu. Mwaliko huu wa Yesu unatuingiza katika kipindi cha toba – tubuni na kuiamini Injili. Huu ni mwaliko wa uzima. Ni mwaliko ili tuongoke, tuanze maisha mapya, maisha ya sala, kufunga na kutoa sadaka.

Kwa nini ikaitwa Jumatano ya majivu?

Jina linatokana na desturi ya kumpaka mtu majivu kichwani pamoja na kumtamkia maneno ya kumhimiza afanye toba inavyotakiwa na kipindi hicho cha liturujia kinachoandaa Pasaka.

Kwa kawaida siku ya Jumatano ya majivu unaanza mfungo unaofuata kielelezo cha Yesu kufunga chakula siku arubaini jangwani baada ya kubatizwa na Yohane Mbatizaji na kabla ya kuanza utume wake mwenyewe.

Nini maana ya majivu tunayopaka?

Majivu ni ishara ya majuto, nayo hufanywa visakramenti kwa kubarikiwa na kanisa. Tunapopakwa majivu katika paji la uso hutusaidia kutafakari na kutukumbusha kuwa wanadamu sisi tu mavumbi na mavumbini tutarudi. Hutukumbusha zaidi kuwa maisha ya hapa duniani tunapita na safari yetu itakamilika pale tutakapoungana na Bwana na mwokozi wetu katika ufalme wako.
Angalia; Isaya 61:3, Ester 4:1-3, Yeremia 6:26, Ezekieli 27:30, Mathayo 11:21 na Luka 10:13

Kwa nini majivu yanapakwa kwenye paji la uso na si vinginevyo?

Ishara yoyote iwekwayo katika paji la uso huonesha umiliki (soma Ufunuo 7:3, Ufunuo 9:4, Ufunuo 14:1, Ezekieli 9:4-6, ). Tunapochorwa ishara ya msalaba katika paji la uso ni ishara kwamba sisi tupo chini yake yeye aliyekufa msalabani kwa ajili yetu.
Hali kadhalika hutukumbusha ishara ya msalaba tuliyochorwa na mafuta matakatifu siku ya ubatizo wetu, hutukumbusha ahadi tuliyoiweka siku hiyo ya ubatizo na kutuita tuishi maisha ya utakatifu

Padri hutamka maneno gani wakati anapaka majivu?

Tunapopakwa majivu Padre husema; Mwanadamu kumbuka u mavumbi na mavumbini utarudi AU Tubuni na kuiamini Injili.

Maneno anayosema padre yana maana gani?

Maneno haya kwa upande mmoja hutukumbusha tunapoelekea, tusisikitike kwamba siku moja tutarudi mavumbini bali tuwe na furaha kwani wakati miili yetu unarudi mavumbini roho zetu zitakwenda kuungana na Mungu Baba mbinguni.
Hivyo maandalizi tunayoalikwa kuyafanaya si maandalizi ya kuelekea mavumbini bali maandalizi ya kuelekeza roho zetu mbinguni. Ndio maana pia twaambiwa tubuni na kuiamini Injili.

Majivu tunayopakwa yanatoka wapi?

Majivu tunayopakwa hutoka katika matawi yaliyotumika katika jumapili ya matawi ya mwaka jana. Majivu haya hubarikiwa na kuwa visakramenti. Hivyo majivu yanapoashiria toba na majuto pia hutukumbusha wema wa Mungu na utayari wake wa kutusamehe.

Kwa nini unatumia matawi ya Jumapili ya Matawi?

Matawi haya yalimkaribisha Yesu Yerusalemu akiwa tayari kufa kwa ajili ya dhambi zetu, yalimpokea mfalme kwa furaha na shangwe kuu. Matawi haya yanapochomwa na sisi kupakwa majivu yetu yanatukumbusha kuwa ni kwa ajili ya dhambi zetu Mungu alimtoa mwanae wa pekee kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu sisi wanaadamu. Hivyo hututafakarisha kuacha dhambi.

Kanisa limekataza nini siku ya Jumatano ya majivu?

Tumekatazwa kula chakula siku ya Jumatano ya Majivu na kula nyama siku ya Ijumaa Kuu katika Amri ya Pili ya Kanisa.

Nani analazima kufunga siku ya Jumatano ya majivu na Kwaresma?

Kila Mkristo aliyetimiza miaka 14 na zaidi anapaswa kufunga kula nyama (Ijumaa kuu) na mwenye miaka zaidi ya 21 kufunga chakula Jumatano ya Majivu

Tunaposema kujinyima wakati wa Kwaresma tunamaana gani?

Kujinyima ni kujikatalia kitu ukipendacho mfano nyama, pombe, sigara, muziki, safari, maongezi n.k.

Mwisho

Wakati wa Kwaresma Waamini wanapaswa kujitakasa zaidi kwa kusali, kufunga, toba na matendo mema

Kipindi cha Kwaresima ni fursa makini ya kumkimbilia Mwenyezi Mungu, kwani kwa njia ya dhambi wamejikuta wakiwa mbali na Uso wa huruma ya Mungu, kiasi hata cha kupoteza imani na matumaini kwa Mwenyezi Mungu. Hii ni changamoto ya kumpenda Mungu na jirani badala ya kukumbatia malimwengu yanayoendelea kuwatumbukiza katika utupu wa maisha ya kiroho. Kwaresima ni kipindi cha waamini kukimbilia na kuambata huruma ya Mungu inayoganga na kuponya dhambi. Ni wakati wa sala, upendo na kufunga.

Usisahau kulike na kushare makala hii uliyoisoma kuhusu; Maana ya siku ya Jumatano ya Majivu. Share Facebook, Twitter bila kusahau WhatsApp.

Ujumbe wangu kwako kwa sasa wa Kutafakari

"Usiache kusali na kutenda mema kwa kuwa huwezi jua ni watu wangapi wanategemea sala na matendo yako mema. Kumbuka Mungu alimwambia Abraham kama akikuta Wacha Mungu wengi hataiharibu Sodoma na Gomora. Vivyo hivyo Inawezekana wapo watu wengi wanaonufaika na Sala na matendo yako, hasa watu wako wa karibu uwapendao. Unapokuwa mtu wa Sala na mcha Mungu unabarikiwa wewe na wale wa karibu yako. KAMWE USIACHE KUMCHA MUNGU NA KUSALI. Ukiwa mregevu ni sawa na unakata Mnyororo wa Baraka za Mungu kwako na wenzako."

Mungu Akubariki Daima. Tukumbukane katika sala.

Endelea kusoma makala hizi;

a.gif Mambo ya kufahamu katika kipindi cha kwaresima
Kwa kipindi cha Kwaresma haya ndiyo mambo muhimu unayopaswa kuyajua… soma zaidi
a.gif Ushauri wangu kwa leo, ni Heri kuchagua kunyamaza
MITHALI 11:12 Asiye na akili humdharau mwenziwe; Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza… soma zaidi
a.gif Soma stori hii, unaweza ukajifunza kitu
SOMA HII STORY UNAWEZA UKAJIFUNZA KITU.
Kijana mmoja alisafiri kwa meli na rafiki zake,
wakiwa katikati ya safari yao meli ilianza
kuzama. Watu wengi pamoja na rafiki wa yule
kijana walikufa maji wakati wanajaribu kujiokoa
kwa kuogelea, lakini yule kijana alifanikiwa.. soma zaidi
a.gif Hadithi: Mkasa wa kusisimua, Jifunze kitu hapa
Watu wawili👬 walikuwa wanakunywa pombe🍺🍻 baa. Wakati wanakunywa wakaanza kubishana🙅🏾‍♂ na baadaye ule ubishi ukawa ugomvi… soma zaidi
a.gif Wakati unapitia magumu usikate tamaa
Kuna Kipindi katika maisha yako unaweza ukapitia mambo Fulani magumu hadi ukaanza kujiuliza,hivi kwa nini yote haya yananitokea?Why Me God?.Na Mimi nimeshawahi kupitia katika hali hii… soma zaidi
a.gif Siri ya kamba nyekundu
Miaka zaidi ya 3000 iliyopita katika mji wa Yeriko alikuwepo mwanamke mmoja kahaba, jina lake Rahabu. Huyu mwanamke aliwaokoa wapelelezi wa Israel waliotumwa kwenda kufanya uchunguzi ktk nchi yao… soma zaidi
a.gif Litania ya Huruma ya Mungu
Litania ya Huruma ya
Mungu.. soma zaidi
a.gif Kwa nini Bikira Maria hakuwa anaombwa akiwa hai? Watu na mitume hawakuwa wanasali kumuomba yeye
Bikira Maria hakuwa anaombwa akiwa hai kwa sababu alikua bado hajatukuzwa na kupewa cheo cha Umalkia wa Mbinguni… soma zaidi
a.gif Kwa nini tarehe ya Pasaka hubadilika
KALENDA za mwanzo ziliutumia mwezi wa
angani kama kipimo cha muda. Ziliitwa
“Lunar calender” au Kalenda-Mwezi. Tarehe 1
ya Mwezi ilikuwa ni siku ulipoandama yaani
Mwezi-Mdogo (Crescent Moon).
Mwezi unapofika siku ya 15 unakuwa
umefikia ukubwa wa juu na huitwa Mwezi-
Mkubwa (Full Moon). Hivyo kwa kalenda ile
tarehe 15 ilikuwa ni siku ya Mwezi-Mkubwa.
Mwaka 45KK, Julius Caesar alitangaza
kalenda mpya ikaitwa “Julian Calender” iwe
na siku 365. Wakati huo ikijulikana kwamba
jua huzunguka kwa siku 365.25. Hivyo pengo
la kalenda na mzunguko likabaki robo siku… soma zaidi
a.gif Mahusiano yanayopelekea Ndoa Takatifu
BY MWL Gasto
Soma had mwisho kuna kitu
KWA NINI UMEINGIA KWENYE MAHUSIANO?
JE ILI UPENDWE>?JE UMEINGIA KWENYE
MAHUSIANO ILI KUJAZA PENGO AMBALO LI
WAZI? UMEINGIA KWENYE MAHUSIANO ILI
UFANANE NA WENGINE WALIO KWENYE
MAHUSIANO? JE UMEINGIA KATIKA MAHUSIANO
ILI KUUMALIZA UPWEKE ULIOKUA NAO?
UMEINGIA ILI UWEZE KUWA NA MTU
UNAYEWEZA KUMUITA MPENZI?
Je ili kumaliza mgandamizo wa kuachika ama
mawazo yeyote?ILI kumkomoa yeyote uliyekuwa
nae kwenye mahusiano?ili
uolewe?au umeanzisha mahusiano kwa sababu muda umeenda?…….
Kama hizi ni sababu za kuingia katika
mahusiano,basi tambua kuwa mahusiano hayo
yatakusumbua sana,na itafika wakati utatoa
maana mbaya ya mahusiano…..na kumbe wewe
ndiye muanzilishi mkuu wa
kuteswa,kuumizwa,kupigwa,kudhalilishwa,kutot
haminika…na wewe ndiye unayetoa ruhusa ya
yote hayo…
Kila mmoja wetu ana uhuru wa kuchagua…usio
na mipaka.Na kila unachokichagua ni
chema…..ni chema kwako….lakini ukumbuke
kila uchaguzi unaoufanya una madhara yake
(yenye faida na yasiyo na faida kwako……….. soma zaidi
a.gif Je Bikira Maria Alizaa Watoto Wengine?
Mapokeo kuhusu Bikira Maria yanaonyesha alikuwa binti pekee wa wazee watakatifu Yohakimu na Ana. Vilevile
Mt. Yosefu, ingawa kisheria alikuwa mume wake, hakutenda naye tendo la ndoa hata moja. Ndiyo maana kwenye
litania yake tunamuita mwenye usafi kamili. Yosefu likufa kabla Yesu hajaanza utume kwa kubatizwa kwenye mto
Yordani. Sisi tunasadiki Maria ni “Bikira daima”… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

Ikiwemo Makala hii ya Maana ya siku ya Jumatano ya Majivu, makala nyingine zinazosomwa sana ni kama ifuatavyo;

• Mungu ni Mkubwa kiasi gani, isome hapa

• Kwa nini Bikira Maria hakuwa anaombwa akiwa hai? Watu na mitume hawakuwa wanasali kumuomba yeye, isome hapa

• Yesu alihalalisha ulaji wa vyakula vyote, Hakuna chakula kinachoweza kumtia mtu unajisi, isome hapa

• Mambo ya kufahamu katika kipindi cha kwaresima, isome hapa

• Ushauri wangu kwa leo, ni Heri kuchagua kunyamaza, isome hapa

• Soma stori hii, unaweza ukajifunza kitu, isome hapa

• Hadithi: Mkasa wa kusisimua, Jifunze kitu hapa, isome hapa

• Wakati unapitia magumu usikate tamaa, isome hapa

• Historia Fupi ya Ibada ya Rozari, isome hapa

• Siri ya kamba nyekundu, isome hapa

Unaweza kusoma makala mpya nzuri kila unapotembelea website hii wakati wowote. Baada ya kusoma makala hii kuhusu; Maana ya siku ya Jumatano ya Majivu, sasa endelea kusoma makala hizi nyingine nzuri nilizokuandalia;

Mtakatifu-Ambrosi.jpg

Mtakatifu wa Sasa
Leo tunatafakari na kujifunza kutoka kwa Mtakatifu Ambrosi.
Soma zaidi kuhusu Mtakatifu Ambrosi hapa.

Chagua aina ya mafundisho unayotaka kusoma hapa..

.

.

.

IMG_20180109_192548.jpg

Kama Una mashaka na Imani na mafundisho ya Kanisa Katoliki soma hapa>>

Website hii inaletwa kwako na Melkisedeck Leon Shine.

Naomba utafakari kuhusu; Upendo na chuki havitangamani. Mungu akubariki sana. Tuombeane…!