Maana ya Kuabudu kwa Mkatoliki

Kuabudu sio kupiga magoti
Ingekuwa ni kupiga magoti basi wanafunzi wanaopewa adhabu ya kupiga magoti mashuleni wangekuwa wanamwabudu mwalimu wao.

Wala siokusujudu.
Maana hata wanajeshi wanamsujudia raisi na wakuu wao.ingekuwa kuabudu ni kusujudia basi hata wanajeshi basi wanaabudu wanadamu.

Wala sio kubusu.
Maana wengi tungekuwa tumeabudu vingi. Tumebusu picha za wapendwa wetu na tumewabusu wengi pia. Tumebusu zawadi tunazopewa.
Kama kuabudu ni kubusu hakika tungekuwa tumekubuhu.

Sasa kuabudu Nini ni?

Kuabudu hakupo katika mwili Bali kupo katika Roho na kweli.
(Walio kanisani wengi ila waabuduo wachache)

Kuabudu kunabebwa na kusudi.
Kubusu msalaba sio kuabudu.
(Kutegemea na kusudi lako hapo.)

Mara nyingi huwa tunasali.
( Ee kristo uliyembinguni.
Nikiutazama msalaba huu nakumbuka kifo chako msalabani kwaajili ya dhambi zangu)

Kwahiyo kuubusu hapo ni kubusu kumbukumbu tu. Kama picha na sio kuabudu kwani hakuna asiyejua kuwa kristo Yupo juu Mbinguni. Na hakuna asiyejua kuwa. Msalaba sio kristo.

Ile ni kumbukumbu)

Watu wengi wanapotosha hili.

Kuabudu sio kubusu.

Ila nyinyi mnaweza kuutazama mwili ila Mungu anatazama mioyo yetu.
Tunaelewa maana ya kuabudu .
Ukitaka kujua zaidi kuwa kuabudu sio matendo ya juu bila kusudi. (Kusudi la mtu sio rahisi kulijua)

Umesoma habari ya Shadrach, Meshack na Abernego,

Walipokataa kusujudia sanamu ya mfalme nebukadneza.
Baada ya msimamo mkali.
Mfalme aliamua kuwaomba basi wafanye tu kusujudia kuonesha watu kuwa wameabudu ( kumbuka ni kuonesha watu Mungu asingeona kuwa wameabudu kwakuwa anaangalia moyo na sio mwili Kama wanadamu) wakafanya kujadiliana wao kwa wao na kuona kuwa Kama watafanya hivyo wataokoa uhai wao Ila watawapotosha watu kwa kuwa walikuwa viongozi. (HUU NI UDHIBITISHO KUWA KUABUDU SIO MATENDO YA JUU)

KABLA YA KUENEZA SHUTUMA. JITAHIDI UWE MTU HURU KUJIFUNZA, MAANA ITIKADI INAWEZA KUMFANYA MTU KUTOJIFUNZA JIPYA LOLOTE. NA KUSHIKA JAMBO LISILO LA KWELI.
MUNGU AKUBARIKI NATUMAINI UMEJIFUNZA,. ( Share kwa watu wajifunze haswa tukielekea kipindi muhimu kabisa Cha kwaresma tuanze kukuza Imani zetu )
[2/24, 12:08] Nic: Kuabudu Nini ni?
Kuabudu ni Jambo zito sana kuliko mtu anavyodhani.
Kuabudu sio kuimba.
Ninakuabudu🔊🎶🎵

Kuabudu
Kupo mbali kuliko hayo maneno Tena ukizingatia
Mungu wetu yupo juu.
Na Ni Mungu asiyeonekana

(Mwili hauwezi kuabudu peke yake bila Roho kamwe)
KATIKA KUABUDU MUNGU HUTAZAMA ROHO AMBAYO HUWA IMEBEBA KWELI YALE MWILI UNAYATOA.

KUABUDU LAZIMA KUNAMTAJA MSHINDI
MKUU KWENYE MAISHA YAKO AMBAYE NI MUNGU.
HUTAZAMA NI KWELI ANAYOSEMA MWANADAMU NDIO YALIYO NDANI YAKE.
(Muumbaji , mkombozi, Alfa na Omega, Muweza, kimbilio lako, msaada wa karibu nk.
Mungu hutazama Roho yako sio Kama mwanadamu atazamaye mwili unayeweza kumdanganya.

Narudia Tena ni wengi sana hawajawahi kumwabudu Mungu.
Imani inayohitajika ili uweze kuuinua Moyo wako na Roho yako kwa Mungu inahitajika kweli kweli iwepo
Ndio maana tunafunga ili kuudhoofisha mwili na kuipa Roho nguvu ili iweze kusikika mbele za Mungu ( isaya 58)

Narudi kueleza
Maana halisi ya kuabudu.
Kuabudu ipo katika Roho na kweli.

Kama hapo mwanzo.
Nilivyoeleza msitishwe
Juu ya kupiga magoti kuinama kubusu.

Hayo yote hayana maana ya kuabudu.
Unaweza kuabudu bila hata kuongea bila hata kutazama.
Hata ukiwa umelala.
Popote I'li mradi
Unaroho tu.

Tuseme basi
Ukiwa kanisani unaabudu altare au mimbari.
Vile vile sanamu tunaziheshimu.
Ila sio Mungu wetu.
Na sio lazima kila mtu akubaliane na wewe
Maana wewe ndio unaujua
Moyo wako na Mungu wako.
Kama unajua Mungu wako alipo na sio sanamu
Unajua na sifa zake na unaamini
Nani anakusumbua.

( MTAZAME MUNGU NA SIO MWANADAMU)

PITIA MAFUNDISHO YA KANISA.
PENDA KUFUATILIA MAISHA YA WATAKATIFU.
UTASHANGAA UKUU WA MUNGU NDANI YA KANISA KATOLIKI

FUATILIA VIDEO ZA MT PIO

PANDRE.
FUATILIA PIA MAISHA YA
PAPA JOHN PAULO WA PILI

UTAAMINI KUWA NEEMA YA MUNGU IPO
TAZAMA MAISHA YAKO
UNAPOSALI KWA IMANI
JE HUJIBIWI.

Mimi siwezi
Maliza kusimulia aliyonitendea live kabisa
Mungu wa Mbinguni

Amini Mungu wako yupo Mbinguni

HAKUNA MKATOLIKI ASIYEJUA MUNGU WAKE NA ANAYEMWABUDU YUPO MBINGUNI.

HAKUNA ASIYEJUA MASANAMU TUNAYAHESHIMU

TENA TUNAZIITA KABISA
SANAMU

MFANO.

NENDA KWENYE SANAMU PALE.

VITUKO
MAKANISA YA WENZETU YANAPICHA.
SASA KAZI YA PICHA NA SANAMU ZINATOFAUTI GANI
SISITUNAZICHUKULIA KAMA PICHA TU.
TUNAZIHESHIMU BASI.
ZINATUKUMBUSHA.
MFANO MSALABA
UNATUKUMBUSHA
KUTESWA KUSULUBIWA
NA KUFUFUKA KWA KRISTO

USIDANGANYIKE
MTAZAME KRISTO
MAANA YEYE HUTAZAMA ROHO
NA SIO MWILI
ANAJUA KUSUDI LAKO
ANAJUA UNALODHAMIRIA
ANAKUJUA
ANAUJUA MOYO WAKO
ANAIJUA ROHO YAKO
MWILI USIKUYUMBISHE
FUNGA SALI
KUWA NA IMANI.
TEMBEA NA KRISTO
SIO WANADAMU.

BAKI IMARA

.

.

.

IMG_20180125_211302.jpg

Kama Una mashaka na Imani na mafundisho ya Kanisa Katoliki soma hapa>>

Website hii inaletwa kwako na Melkisedeck Leon Shine.

Naomba utafakari kuhusu; Mawazo ya Mungu tunapokua na shida na mateso. Mungu akubariki sana. Tuombeane…!