Je, siku ya Ijumaa kuu Wakatoliki wanaabudu Msalaba?

By, Melkisedeck Shine.

Kitu cha msingi ni kusikiliza maneno ya Padre au shemasi anapowaalika watu kuja kuanza kuabudu.Padre au shemasi husema,

“Huu ndio mti wa msalaba, ambao wokovu wa dunia
umetundikwa juu yake, njooni tuuabudu”.

Ukifuatilia kwa makini kiswahili sanifu na bahati njema wewe mwalimu japo sijui wa somo lipi, utagundua kuwa, Padre hufanya mambo haya yafuatayo katika mwaliko huo:
1. Hutuonesha mti wa msalaba.
2. Hutuambia kuwa juu ya mti huo,wokovu umetundikwa
3. Kisha hutualika tukauabudu.

Ningekuwa naongea nawe,ningekuuliza hivi hutualika tukauabudu mti wa msalaba au wokovu ambao umetundikwa juu ya huo mti au tukauabudu mti na msalaba au tukauabudu nini? Hebu fikiri kisha uone kama mawazo yako ni sawa na nitakachokisema hapa chini kabla hujaangalizia!

Wakatoliki hualikwa kufanya nini?

Kwa mwaliko huo,wakatoliki hualikwa kwenda kuuabudu WOKOVU ulio juu ya msalaba.WOKOVU NI NINI? WOKOVU ni jina lililoandikwa kwa kiswahili.Jina wokovu kibiblia na kwa lugha asili ya Biblia ni sawa na jina YESHUA kwa kiebrania au YOSHUA. Mwanangu,wewe unamfahamu Yoshua katika Biblia kuwa alichukua jukumu la kuwaingiza Waisrael katika nchi ya ahadi baada ya Musa kufa kwani huyu ndiye aliyekuwa msaidizi wa Musa.Yoshua aliwachukua watu hawa wakiwa ng`ambo ya mto Yordan wakisubilia tu kuiingia nchi ya ahadi.Kumbe kwa Waisrael Yoshua ni mtu wa muhimu sana kwao kwani baada ya Musa kuwatoka,wanamtumainia Yoshua na kumwona kuwa ni Mwokozi wao kwa kitendo cha kuwafikisha salama katika nchi ya ahadi ambayo kwa miaka karibu 40 wamesafiri kuifikia.Tendo la Yoshua la kuyapiga maji ya mto yakagawanyika na kuacha nchi kavu nao wakavuka bila shida,ndilo wanaloliona kuwa la kuwaletea ukombozi kama alivyofanya Musa pale alipoyapiga maji ya bahari ya Sham yakaacha njia wakapita kwa usalama kutoka Misri.

Kristo ndiyo WOKOVU wetu tunayepaswa kumwabudu kwani alipokuja aliamua kuanzia kazi yake ya kutuletea wokovu katika mto Yordan pale ambapo Yoshua kahitimishia kazi yake.Yoshua aliwavusha watu toka ng`ambo ya mto kuwaingiza katika nchi ya ahadi ambayo ni Kanaan ya duniani na Yesu anapokuja,kama mwokozi,anataka awatoe watu wake kutoka katika nchi ya ahadi ya kidunia,kuwapeleka katika nchi ya ahadi ya mbinguni.Kumbe Yesu ni mwokozi wetu anayetutoa kutoka katika dunia kwenda mbinguni wakati Yoshua anaitwa mwokozi kwa kuwa aliwatoa Misri akawaleta Kanaan nchi ya ahadi.Yesu na Yoshua kwa mantiki hii ni hilo jina WOKOVU kama nomino wakati kazi waliyotenda ni ya kutuokoa na kikitamkwa kama kitendo,Yesu au Yoshua,anaitwa Mwokozi.

Labda nikupeleke kidogo darasani juu ya mambo ya viambishi katika lugha ya kiswahili kwani hapa ndipo wengi wanaposhindwa kueleza kile tunachokiabudu ile Ijumaa Kuu.
Padre au Shemasi husema ,

Huu ndiyo MTI wa msalaba ambao WOKOVU wa dunia Umetundikwa juu yake, njooni tuUabudu.

Katika sarufi ya kiswali hasa tunaposema juu ya upatanisho wa kisarufi, bahati mbaya ni kwamba nomino MTI na nomino WOKOVU zote zimechukua viambishi ngeli U, ili kuwa na upatanisho wa kisarufi. Tunasema kwa mfano, mti umaanguka, wokovu umetujia. Katika sentensi hiyo anayotamka padre au shemasi, ina maneno yote mawili, yaani mti na wokovu yenye kiambishi kimoja tu U kinachotuletea shida kuwa kimaresha nini, wokovu au mti. Kiambishi U, hakirejerei mti bali kinarejea wokovu yaani Yesu.
Kwa hiyo tunaposema njooni tuuabudu, hatumaanishi tuuabudu mti la hasha! Bali tuuabudu Wokovu uliotundikwa juu ya mti wa msalaba katika akili zetu. Ndiyo kusema, ibada hii kama mtu hawezi kutoka nje ya pale na kupeleka mawazo yake kwa Yesu, aliye Wokovu wetu , bila shaka anaweza kuwa anaabudu sanamu au mti wa msalaba.

Mpendwa sista, Kristo Bwana wetu ndiye sanamu ya kwanza kabisa ya Mungu. Ndiyo maana Kristo anasema aliyemwona Yesu kamwona Baba Yn 14:8f. Kama Yesu ni sanamu,hata binadamu ni sanamu za Mungu kwa vile tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu.Kama mtu anaziogopa sanamu,ashakumu si matusi,aogope hata kuzaa watoto kwa vile kuzaa mtoto ni kuongeza sanamu duniani kwa kuwa licha ya kufanana na Mungu,zinafanana na mzazi mwenyewe.Kama hatuziabudu,yanini kuziogopa? Kama maandishi ni sanamu lakini hatuyaabudu,kwa nini uogope kusoma herufi? Mungu si mjinga wa kutuhukumu kwa mambo kama hayo yasiyochukua sifa yake.

Pamoja na hayo,tukumbuke kuwa sanamu huanzia kichwani mwa mtu kama nilivyokwishasema.Kama mtu akibuni kichwani kutengeneza gari nzuri sana,hatuwezi kumzuia kwa sababu atakapotengeneza kile alichonacho kichwani kikawa gari,hatakiabudu.La sivyo,hata kupanda gari ili kusafiri tuache kwani tunapanda
Ndani ya sanamu walizotengeneza watu.Ukiwa na picha zako,kwa jinsi zilivyotoka vizuri,ukafurahi na kuzibusu,haina maana kuwa unaziabudu.Au,kwa vile sasa unajua kuwa mtu ni sanamu ya Mungu,je ukienda mahali ukamsalimu mkubwa wako au anayekulea wakati unampa kitu ukampatia huku ukipiga goti, utakuwa unamwabudu?

Hatimaye, Kanisa katika sheria yake no.1159 linafundisha kuwa,sanamu ya Mungu haipo kwani tangu mwanzo Mungu baba hajawahi kuonwa na mtu isipokuwa kupitia kwa mwanae ambaye watu walimwona na waliishi naye wakamfahamu na kumbe kuchonga sanamu ya kufanana naye Isingeliwezekana.Sanamu za Yesu zafanana naye kwa vile watu walimfahamu alivyofanana lakini zimeletwa kwetu kama ukumbusho wa jinsi alivyokuwa si kwa lengo la kuziabudu. Kwa kuziona,hatuna mashaka kuwa alikuwepo kuliko kama tungekuta masimlizi tu.Hivyo hivyo kizazi kijacho kikiambiwa juu ya Nyerere kitaelewa zaidi kikioneshwa picha na sanamu zake lakini hizo picha na sanamu zake hawatasema ndo Nyerere mwenyewe labda kama ni vichaa.

HITIMISHO.

Mungu si mjinga wa kukasirikia kitu kisicho na madhara. Aliwaadhibu wote waliochonga sanamu na kusema hizo zafanana na Mungu lakini sisi hatusemi zinafanana naye bali tunajua kuwa yeye yupo na hizo zipo kama ukumbusho wa sura ya Yesu mwanae ambaye tunamfahamu kupitia waliomwona wakazitengeza. Akili zetu zinapata kutufanya tumtambue Kristo tunapoziona sanamu lakini kwa zenyewe si Kristo wala Mungu wetuFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya Je, siku ya Ijumaa kuu Wakatoliki wanaabudu Msalaba?

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; Je, siku ya Ijumaa kuu Wakatoliki wanaabudu Msalaba?

a.gif NI KWELI WAKATOLIKI WANAABUDU SANAMU ?

Kati ya dhambi ambazo kwa wakatoliki ndiyo wazi kwa watu ni dhambi ya kuabudu sanamu. Dhambi hii imewafanya wakatoliki waonekane au hawasomi Biblia au wanasoma ila hawaelewi au wanasoma na kuelewa lakini wamekuwa wakipuuza maandiko Matakatifu. Ubayana wa dhambi hii kwa wakatoliki ni kile wanachokifanya siku ya Ijumaa Kuu na mambo yanayoonekana katika nyumba za kuabudia kama makanisa ambapo sanamu lukuki zinaonekana, toka zile za vitu vya duniani hadi vile za mbinguni… soma zaidi

a.gif Je Yesu yupo mzima katika Ekaristi Takatifu? Kwa nini tunaabudu Ekaristi Takatifu?

Ndiyo. Ekaristi Takatifu inamuwakilisha Yesu Mwenyewe aliye Mungu na aliyeamua Mwenyewe kuwepo katika Maumbo ya Mkate na Divai.
Ukisoma Yoh 6:51-57 inasema hivi;.. soma zaidi

a.gif Maswali na majibu kuhusu Watakatifu ndani ya Kanisa Katoliki

Soma haya kuhusu watakatifu;.. soma zaidi

[Wimbo Mzuri PA.gif] Jina Maria Jina Tukufu

[Tafakari ya Sasa] 👉Sala sio maneno tuu

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Katarina wa Siena

ufufuo-wa-wafu-upooo.JPG

a.gif Hatimaye Yesu alitumia divai kufanyia nini?

Kama alivyofanya Melkizedeck anayefananishwa na Yesu. “Melkizedeki mfalme wa Salemu alileta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu aliye juu sana” (Mwa 14:18), “amefananishwa na Mwana wa Mungu” (Eb 3:7). Alimtolea Mungu kama sadaka.. soma zaidi

a.gif Mashirika ya Kitawa yapo mangapi?

Mashirika ya Kitawa yapo mengi na yana Karama/Utume mbalimbali, ila yote yanamtukuza Mungu Baba na Kumsujudia Yesu Kristo. (1 Kor 12:4-6).. soma zaidi

a.gif Kwa nini yatupasa kuwaheshimu Watakatifu?

Kwa sababu hao ni washindi, rafiki wa Mungu na waombezi wetu… soma zaidi

a.gif Ujumbe wa leo

*UJUMBE WA LEO*
Ndege anapokuwa hai huwa anakula sana funza, lakini atakapokufa nae huliwa na funza.. Maisha yanabadilika kila wakati, usimdharau wala kumuumiza mtu yeyote katika maisha…Unaweza ukawa imara sana leo lakini kumbuka maisha ni imara kuliko wewe.., Mti mmoja unaweza ukatengeneza mamilioni ya njiti za kiberiti, lakini muda ukifika njiti moja tu ya kiberiti inaweza ikachoma msitu mzima….. soma zaidi

a.gif Roho Mtakatifu anawafanyia Waamini nini?

Roho Mtakatifu anawafanyia Waamini haya.
1. Anawatakasa.. soma zaidi

a.gif Je, wenye daraja wanaweza wakatenda dhambi?

Ndiyo, wenye daraja wanaweza wakatenda dhambi kwa sababu ni binadamu kama sisi sote. Yesu alionja ukosefu wa Mitume hasa wakati wa mateso… soma zaidi

a.gif Misa Takatifu ina sehemu kuu ngapi?

Misa Takatifu ina sehemu kuu mbili.. soma zaidi

a.gif Sakramenti inayohusiana zaidi na ubatizo ni ipi?

Sakramenti inayohusiana zaidi na ubatizo ni kipaimara, kinachoendeleza kazi yake… soma zaidi

a.gif Roho Mtakatifu anatufanyia nini sisi Wakristo?

Roho Mtakatifu anatufanyia haya;.. soma zaidi

a.gif Twawakosea Heshima Baba na Mama kwa kufanya nini?

Twawakosea Heshima Baba na Mama kwa;.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.