Tushiriki mafumbo hayo mara ngapi?

Tushiriki mafumbo hayo mara ngapi?


Tushiriki mafumbo hayo kadiri ya umbile la kila mojawapo. Kuna “ubatizo mmoja” (Ef 4:5) kwa sababu ni kuzaliwa upya “kwa maji na kwa Roho” (Yoh 3:5), jambo lisiloweza kurudiwa. Vilevile katika kipaimara na daraja, karama inayopatikana kwa kuwekewa mikono na mwandamizi wa Mitume haifutiki, inadai kuchochewa tu. “Nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu” (1Tim 1:6). Kumbe tunahitaji ekaristi mara nyingi, kwa sababu ni chakula cha roho. “Bwana, sikuzote utupe chakula hiki” (Yoh 6:34). “Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo” (1Kor 11:26).


Soma mpangilio wa mafundisho yote kulingana na topiki hapa>>Mafundisho mengine ya Kikatoliki


Ishara-ndogo-ya-Msalaba.png
HURUMA-YA-MUNGU.png
YESU-ANAKUPENDA.png