Sala ni nini?

Sala ni kuinua mioyo yetu kwa Mungu na kuongea nae. Kuongea maana yake ni kusema na Kusikiliza. Sala sio kuongea tuu, sala ni kuongea na kusikiliza. Mungu anatualika tuongee nae kwa kusema na kusikiliza. Kwenye Biblia tunasoma Hivi;

β€œNiite, nami nitakujibu na kukuambia mambo makubwa yaliyofichika ambayo hujapata kuyajua".(Yeremia 33:3)

Vile tunavyokuwa na juhudi ya kusali kwa kusema mbele ya Mungu ndivyo hivyo hivyo tunatakiwa tuwe na juhudi ya kumsikiliza Mungu kile anachotuambia. Tunaweza kumsikiliza Mungu ndani kabisa ya Mioyo yetu, mara nyingine kwa kupitia dhamira zetu, kupitia watu wengine na kupitia neno lake (Biblia). Tuombe neema ya kutambua sauti yake anaposema nasi ili tuweze kumsikiliza na kutengeneza mahusiano mazuri kati yetu na yeye.

Mungu ni Baba yetu, anatupenda sana na yupo tayari kutusikiliza wakati wote ndio maana Mungu anatualika kwa kutuambia;

"Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu". (Isaya 1:18)

Tudumu katika sala daima kwa sababu njia ya sala ndipo tunaweza kusema yale tunayotaka mbele ya Mungu na kusikia yale anayotaka Mungu.

⏩Swali linalofuata: Kwa nini tunasali?

⏬⏬Endelea kusoma maswali haya yafuatayo ili kuelewa zaidi swali hili kuhusu πŸ‘‰Sala ni nini?πŸ‘‡

β€’ Masifu ni nini?

β€’ Mungu ni nani?

β€’ Mungu ni nini?

β€’ Zaka ni nini?

Usisahau kushare makala hii uliyoisoma kuhusu; Sala ni nini?. Share Facebook, Twitter bila kusahau WhatsApp.

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

Ikiwemo Makala hii ya Sala ni nini?, makala nyingine zinazosomwa sana ni kama ifuatavyo;

β€’ Chagua kunyamaza: Huu ni ushauri kwa Leo, isome hapa

β€’ Matumizi ya Neno 'Ameen', isome hapa

β€’ Usidanganyike Binti yangu, isome hapa

β€’ Mafundisho ya kumfundisha mtu mzima kabla ya ubatizo wa hatari, isome hapa

β€’ Swali la kutisha, isome hapa

β€’ Soma hii stori unaweza ukajifunza kitu, isome hapa

β€’ Tujifunze kitu hapa, isome hapa

β€’ Kuumbwa kwa mtu, Mungu alivyoumba binadamu, isome hapa

β€’ Kuumbwa kwa Dunia, isome hapa

β€’ Mtakatifu Teresa (Teresia) wa Mtoto Yesu (wa Lisieux), isome hapa

Ujumbe wangu kwako kwa sasa wa Kutafakari

"Upendo wa kweli hauambatani na chuki. Huwezi kusema una Upendo wakati kuna watu wengine unawapenda na wengine unawachukia. Ni sawa na kusema kitambaa ni cheupe lakini kina madoa doa, maana yake sio cheupe."

Mungu Akubariki Daima. Tukumbukane katika sala.

Unaweza kusoma makala mpya nzuri kila unapotembelea website hii wakati wowote. Baada ya kusoma makala hii kuhusu; Sala ni nini?, sasa endelea kusoma makala hizi nyingine nzuri nilizokuandalia;

[WIMBOPA.gifπŸ‘‰] Maombezi yako Maria
[WIMBOPA.gifπŸ‘‰] Tumsifu Maria
Mtakatifu-Fransisko-Xaver.jpg

Mtakatifu wa Sasa
Leo tunatafakari na kujifunza kutoka kwa Mtakatifu Fransisko Xavier.
Soma zaidi kuhusu Mtakatifu Fransisko Xavier hapa.

Chagua aina ya mafundisho unayotaka kusoma hapa..

.

.

IMG_20180108_172410.jpg

Kama Una mashaka na Imani na mafundisho ya Kanisa Katoliki soma hapa>>

Website hii inaletwa kwako na Melkisedeck Leon Shine.

Naomba utafakari kuhusu; Sala ni kuongea na Mungu. Mungu akubariki sana. Tuombeane…!