Ni halali kujitungia ibada kwa sababu gani?

Ni halali kujitungia ibada kwa sababu gani?


Ni halali kujitungia ibada kwa sababu sala ni hasa maongezi ya Mungu na mtu. Adamu na Eva “walisikia sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga” (Mwa 3:8). Yeye hachoki kumvuta kila mmojawetu kwake na kumtia hamu ya kumhimidi na kumuabudu, kumuomba kwa ajili yake na ya wengine, kumshukuru na kumsifu. “Ee Bwana, uisikie sala yangu, uzisikilize dua zangu, kwa uaminifu wako unijibu kwa haki yako” (Zab 143:1). Hata tukisali pamoja, uhusiano wa kila mmojawetu na Mungu ni wa pekee. Tusiposali kwa moyo, ibada ni ya bure. “Watu hawa hunikaribia na kuniheshimu kwa vinywa vyao, bali mioyo yao wamefarakana nami” (Isa 29:13).


Soma mpangilio wa mafundisho yote kulingana na topiki hapa>>Mafundisho mengine ya Kikatoliki


YESU-ANAKUPENDA.png
HURUMA-YA-MUNGU.png
Ishara-ndogo-ya-Msalaba.png