tags

Kishawishi ni nini?

Kishawishi ni tamaa au mvuto mbaya wa kwenda kinyume na Mapenzi ya Mungu ili kuvunja Amri zake na za Kanisa lake.


Kishawishi ni dhambi?

Kishawishi si dhambi ni majaribu tu, ukikubali ndiyo dhambi, ukikataa ni jambo jema. (Mt 18:8-9)


Vishawishi vinatokana na nini?

Vishawishi vinatokana na;

1. Shetani

2. Watu

3. Vitu


Ufanyeje ushinde vishawishi?

Ili kushinda vishawishi:

1. Sali daima hasa mara unaposhawishiwa

2. Epuka nafasi ya dhambi

3. Pokea Sakramenti hasa Kitubio na Ekaristi

4. Soma neno la Mungu.


Mambo yanayomzuia mtu kuishi maisha mema ni yapi?

Mambo hayo ni;

1. Dhambi

2. Vilema

3. Vishawishi


YESU-ANAKUPENDA.png