Kanisa linamuadhimishaje Mungu tena?

Kanisa linamuadhimishaje Mungu tena?


Kanisa linamuadhimisha Mungu tena kwa visakramenti ambavyo kwa mamlaka ya Kristo linawatia watu neema zake katika nafasi yoyote ya maisha. Kati yake muhimu zaidi ni baraka na mazinguo, ambavyo vipo tangu zamani, hata nje ya taifa la Israeli. Melkisedek alisema, “Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi. Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako” (Mwa 14:19-20). Farao aliomba, “Mkanibariki mimi pia” (Kut 12:32). Balaam alisifiwa, “Najua ya kuwa yeye umbarikiye hubarikiwa, na yeye umlaaniye hulaaniwa” (Hes 22:6). “Ikawa, ile roho mbaya kutoka kwa Mungu ilipomjilia Sauli, ndipo Daudi akakishika kinubi, akakipiga kwa mkono wake, naye Sauli akaburudishwa, na ile roho mbaya ikamwacha” (1Sam 16:23). “Na mimi nikitoa pepo kwa Beelzebuli, je, wana wenu huwatoa kwa nani?” (Math 12:27).


Soma mpangilio wa mafundisho yote kulingana na topiki hapa>>Mafundisho mengine ya Kikatoliki


YESU-ANAKUPENDA.png
HURUMA-YA-MUNGU.png
Ishara-ndogo-ya-Msalaba.png