YESU%20MFALME%20WA%20HURUMA.gif

Blog Kwa Wakatoliki

HOME | MAKALA | TAFAKARI | SALA | MAFUNDISHO | MIUJIZA | WATAKATIFU | NYIMBO | PICHA | MAKTABA/LIBRARY | BIKIRA MARIA | KUHUSU SANAMU | KUHUSU KANISA

Kama Una mashaka na Imani na mafundisho ya Kanisa Katoliki soma hapa>>

By Melkisedeck Leon Shine

.

πŸ‘‰β” Je, sisi wanyonge tunaweza kushiriki uzima wa milele wa Mungu?πŸ‘‡

Ndiyo, sisi wanyonge tunaweza kushiriki uzima wa milele wa Mungu: hapa duniani katika mwanga hafifu wa imani, na kisha kufa katika uangavu wa utukufu usiofifia kamwe. Kwa kuwa lengo la Baba ni kwamba tuungane na Yesu Mwanae kwa uwezo wa Roho Mtakatifu ili tuwe na utukufu wake. β€œNa uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma” (Yoh 17:3). β€œKwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa” (2Pet 1:3-4). Sisi tuliobatizwa tunaitwa β€œwana wa Mungu; na ndivyo tulivyo!” (1Yoh. 3:1). Kwa sababu tumesadiki kwamba β€œMungu ni upendo” (1Yoh 4:8) na kwamba β€œhakuna lisilowezekana kwa Bwana” (Lk 1:37). β€œNa kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, β€˜Aba!’ yaani, β€˜Baba!’ Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu” (Gal 4:6-7).

βͺSwali lililopita: Tutakapofariki dunia itatutokea nini?
⏩Swali linalofuata: Aliyezungumzia moto wa milele ni nani?
⏬⏬ Endelea kusoma maswali haya yafuatayo ili kuelewa zaidi swali hili kuhusu πŸ‘‰Je, sisi wanyonge tunaweza kushiriki uzima wa milele wa Mungu?πŸ‘‡
MELKISEDECK-SUA.jpg

Ujumbe wangu kwako kwa sasa

Mawazo ya Mungu ni makuu. Mungu anatuwazia mema daima. Hata unapopitia shida na matatizo katika maisha nia ya Mungu inabaki kuwa njema ya Kukuonyesha ukuu wake na kukuwezesha kumjua yeye. Pengine usingejua matendo ya Mungu bila kupitia shida na changamoto katika maisha. Mungu hapendi upate shida bali anaruhusu hayo ili upate faida ya kumjua na kujua uwezo wake. Hata Yesu ilibidi apitie mateso na kifo ili uwezo wa Mungu udhihirike baada ya kufufuliwa. Amini kuwa kuna mema mbele yako baada ya mateso haya ya sasa.

Mungu Akubariki Daima… Tuombeane!