tags

Fadhila inayoondoa uvivu ni ipi?

Fadhila inayoondoa uvivu ni utendaji


Mambo yanayomzuia mtu kuishi maisha mema ni yapi?

Mambo hayo ni;

1. Dhambi

2. Vilema

3. Vishawishi


Vilema ni nini?

Vilema ni mazoea ya kutenda mambo mabaya na kuacha kutenda mambo mema. (Gal 5:19-21)


Vichwa au Mizizi ya dhambi ni ipi?

1. Majivuno

2. Uchoyo

3. Wivu

4. Hasira

5. Tamaa mbaya

6. Ulafi

7. Uvivu au uzembe


Majivuno ni nini?

Majivuno ni kujiona mkubwa nafsini mwako au mbele za watu.


Ni fadhila gani inayoondoa majivuno?

Fadhila inayoondoa majivuno ni fadhila ya Unyenyekevu


Ubahili ni nini?

Ubahili ni kupenda mno mali za dunia na kumsahau Mungu


Ni fadhila gani inayoondoa ubahili?

Fadhila inayoondoa ubahili ni ukarimu


Uchafu ni nini?

Uchafu ni kufanya mawazo, tamaa, maneno au matendo kwa kuvunja amri ya sita au ya tisa ya Mungu


Ni fadhila ipi inayoondoa uchafu?

Fadhila inayoondoa uchafu ni fadhila ya Usafi wa Moyo


Wivu ni nini?

Wivu ni kuwaonea watu uchungu kwa heri walizonazo au kufurahia misiba yao


Ni fadhila ipi yenye kuondoa wivu?

Fadhila inayoondoa wivu ni fadhila ya wema


Ulafi ni nini?

Ulafi ni kupenda kula au kunywa bila kiasi


Ni fadhila gani inayoondoa ulafi?

Fadhila inayoondoa ulafi ni kadiri na kiasi


Hasira ni nini?

Hasira ni kukasirika bure kuonea na kulipiza kisasi


Ni fadhila ipi yenye kuondoa hasira?

Fadhila inayoondoa hasira ni fadhila ya upole


Uvivu ni nini?

Uvivu ni uregevu wa moyo unaotufanya tukose juhudi


YESU-ANAKUPENDA.png
JesusShroudAnimated.gif