Huruma ya Mungu inazidi hasira

Mungu ni mwenye huruma na rehema, Huruma kuu ya Mungu inazidi hasira yake. Yeye ni rahisi kusamehe kuliko kuadhibu. Hata Mungu anapoadhibu kwa ajili ya makosa yetu, huruma yake humfanya kughairi adabu, ijapokua tunastahili adhabu lakini kwa huruma yake ametustahilisha Rehema neema na Baraka.

Kila Mungu anapoadhibu baada ya adhabu ni Baraka, hii ni kutokana na upendo wake mkubwa kwetu kutoka Katina kilindi cha huruma yake kuu.

Nakualika kuitumainia Huruma ya Mungu. Hata kama upo katika hali yoyote ile, Iwe ya neema au ya dhambi Mungu bado anakutambua na anatamani uwe nae.

πŸ™‰πŸ™‰πŸ™‰Usisahau kushare makala hii kuhusu Huruma ya Mungu inazidi hasira yake.πŸ‘ Share facebook, twitter n.k bila kusahau WhatsApp!πŸ’―βœ”


IMG_20181021_133435.jpg
Ujumbe wangu kwako kwa sasa

Hakuna sala yeyote itolewayo kwa unyenyekevu wa kweli katika imani, matumaini na mapendo inayopita bure mbele ya Mungu. Mungu hamtupi mwenye unyoofu wa moyo.

Mungu Akubariki sana… Tuombeane!

SASA.gif

πŸ“š Endelea kusoma kuhusu;-πŸ‘‡

Ndugu.gif