.

👉 Waziri mwenye ushawishi mkubwa katika serikali ya Rais Uhuru Kenyatta amejiuzulu👇✔

MELKISEDECK-SUA.jpg

Imehaririwa na; Melkisedeck Leon Shine. Tarehe 29 Jan 2016 14:49. [Legal & Authority]


Waziri mwenye ushawishi mkubwa katika serikali ya Rais Uhuru Kenyatta amejiuzulu

150915090120_anne_waiguru_512x288_waigurutwitter_nocredit.jpg Waziri mwenye ushawishi mkubwa katika serikali ya Rais Uhuru Kenyatta amejiuzulu wadhifa wake baada ya shinikizo kutolewa ajiuzulu kutokana na tuhuma za ufisadi.

Amewaambia wanahabari kwamba amemwandikia Rais Kenyatta akimtaka amuondolee majukumu yake.

Hata hivyo amesisitiza kwamba hana hatia.

“Ninafuata ushauri wa daktari na nimemuomba Rais aniondolee majukumu yangu kama waziri … na akiona inafaa, anipe majukumu ambayo si mazito,” Bi Waiguru amesema.

Bi Anne Waiguru, ambaye amekuwa Waziri wa Mipango na Ugatuzi, ameambia wanahabari Nairobi kwamba ameshauriwa na daktari wake “achukue muda kupumzika”.

🙉🙉🙉Usisahau kushare posti hii kuhusu (Waziri mwenye ushawishi mkubwa katika serikali ya Rais Uhuru Kenyatta amejiuzulu).👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome💯✔


Slide1-mabest-skull.PNG

.

.

Blog nyingine maarufu ndani ya AckySHINE.com

| Vichekesho | Videos | Picha | Ujasiriamali | Mahusiano | Kilimo & Mifugo | Katoliki | Afya & Mapishi | Hadithi | Misemo | SMS