Usiyoyajua kuhusu shambulio la kigaidi la Septemba 11, 2001 huko Marekani

By, Melkisedeck Shine.

uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png

Usiyoyajua kuhusu shambulio la kigaidi la Septemba 11, 2001 huko Marekani

Kila ifikapo Septemba 11 ya kila mwaka Marekani hukumbuka shambulizi baya la kigaidi kuwahi kutokea la kulipuliwa kwa majengo pacha ya Shirika la Biashara la Kimataifa (WTO) mjini New York mwaka 2001.

Jumanne iliyopita Septemba 11, mwaka huu Marekani iliadhimisha kumbukumbu ya miaka 17 ya shambulizi ambalo kundi la kigaidi la Al-Qaida chini ya kiongozi wake Osama bin Laden lilikiri kulifanya.
Idara ya Polisi ya New York imelichukulia tukio hili kwa uzito mara mbili ya ule wa taifa zima kwa kuwa yenyewe pia ilipoteza maofisa wake wanaokadiriwa kufikia 23 katika shambulizi hilo. Kwa sababu hiyo, idara zote za polisi kutoka maeneo yote ya Marekani na Canada waliungana kufanya matembezi karibuni na eneo la Manhattan ambapo shambulizi hilo lilitokea.
Tukio hili lilichukua uhai wa raia zaidi ya 2,977 mjini New York, makao makuu ya jeshi la Marekani maarufu kama Pentagon na eneo la wazi mjini Pennsylvania. Shambulizi hili na madhara yake limeibadili sera ya Marekani kuhusu ulinzi kwa miaka 17 sasa na kulifanya taifa hilo kuwa makini zaidi juu ya ugaidi.
Hata hivyo, bado imekuwa vigumu kuwasahaulisha wananchi wa Marekani tukio hilo baya. Yapo mambo ambayo kama si umeyasahau basi huyafahamu kuhusu Septemba 11. Haya ni baadhi ya mambo hayo.
Haijulikani namna watekaji wa ndege walivyoingia katika vyumba vya marubani. Baada ya shambulizi hili iliundwa kamati ambayo ilikuja na ripoti iliyochapishwa mwaka 2004, ripoti hiyo ilieleza kwamba hakuna hata mmoja anayefahamu ni kwa namna gani watekaji waliingia kwenye ndege mpaka kwenye vyumba vya marubani wa ndege nne ambazo zilitumika katika shambulizi hilo.
Hata hivyo, ripoti hiyo inaeleza kuwa “huenda mmoja wa marubani au ofisa wa ndege alibanwa na kutoa ufunguo wa ndege au alilazimishwa kufungua mlango katika ndege ya abiria iliyoitwa American Airlines 11.”
Baada ya watekaji kuingia katika chumba cha rubani waliielekeza katika majengo-pacha ya makao makuu ya WTO, New York na kuligonga lile la upande wa kaskazini saa 8:46 asubuhi. Abiria wote 81, watekaji watano na wahudumu tisa na marubani wawili waliokuwemo katika ndege hiyo iliyokuwa inatoka Boston kwenda Los Angeles walifariki dunia pamoja na watu waliokuwepo katika jengo hilo ambao idadi yao haikufahamika.
Abiria waliwataarifu jamaa na familia zao kuhusu kutekwa kwao, inadaiwa kwamba abiria wote waliokuwamo katika ndege zote nne zilizotekwa, yaani American Airlines 11, United Airlines 175, American Airlines 77 na United Airlines 93 walizipiga simu ama simu zao au nyingine zilizokuwapo katika ndege kuwataarifu juu ya uwepo wa watekaji hao.
Hata hivyo, walishindwa kuwa na msaada kwani waligundua kwamba mfumo wa taarifa ulikwisha kuzimwa.
Ndege iliyoitwa American Airlines 77 iliondoka katika uwanja wa Dulles mjini Washington ilitekwa karibu na Indianapolis kisha ikarudishwa Washington na kuangushwa Pentagon. Mke wa mwanasheria wa Serikali, Jenerali Ted Olson, Barbara Olson alikuwa miongoni mwa abiria waliokuwepo katika ndege hiyo, alimpigia simu mumewe kumweleza kuwa wametekwa. Hata hivyo, American 77 ilianguka Pentagon saa 9:37 asubuhi na kuua watu 69 waliokuwemo ndani ya ndege.
Mawasiliano yaliyopatikana katika visanduku vya mawasiliano yaliunganishwa baadaye na kugundua namna ambavyo ndege ilitekwa.
Idadi ndogo ya abiria waliokuwamo ilirahisisha watekaji wasigundulike, ripoti zinaeleza kuwa maofisa waliochunguza kisa hicho wanasema kuwa idadi ndogo ya abiria kuliko ile iliyotakiwa kubebwa na ndege hizo ilichangia watekaji kupenya kirahisi na kupata nafasi ndani ya ndege bila kugundulika. Kwa mfano, American 11 iliyoondoka Boston kwenda Los Angeles ilikuwa na abiria 81 kati ya 158 iliyotakiwa kubeba.
Pia, United 175 iliyoondoka Boston kwenda Los Angeles ilikuwa na abiria 56 pekee kati ya 168, hiyo ni sawa na asilimia 33 ambayo ni chini ya asilimia 49 ya uzito iliyotakiwa kubeba. American 77 ilikuwa inaelekea Los Angeles kutoka Washington ilikuwa na abiria 58 kati ya abiria 176 iliyotakiwa kubeba.
United 93 iliyotoka New York kwenda San Francisco ilikuwa na abiria 37 ambao ni sawa na asilimia 20 ya uwezo wake ikiwa ni chini ya asilimia 52 ya uzito iliyotakiwa kubeba. Idadi hii inadaiwa kuwapa watekaji nafasi ya kuketi bila kugundulika kwa kuwa kama ndege zingekuwa na abiria wote basi wangeonekana kwani wangekosa mahala pa kuketi.
Kupungua idadi ya watekaji kulisababisha United 93 isilete madhara makubwa, inadaiwa kwamba watekelezaji wa shambulizi hili walipanga kwamba kila ndege iwe na watekaji watano, lakini Mohamed al Kahtani alizuiliwa na maofisa uhamiaji wa uwanja wa Florida Orlando baada ya kuhisiwa, ” inasema ripoti ya Septemba 11.
Ndege zote tatu zilikuwa na watekaji watano huku United 93 ikiwa na watekaji wanne pekee na kushindwa kuwadhibiti abiria na marubani. Kutokana na hilo, United 93 haikulenga kama ilivyokusudiwa.”
Kwa sababu hiyo baadhi ya abiria walijaribu kuelekea kwenye chumba cha marubani kumdhibiti, aliamua kuiangusha ndege katika eneo la wazi huko Shakville ikiwa ni dakika 20 tu baada ya ndege hiyo kupaa.
Makamu wa Rais, Cheney aliamuru United 93 itunguliwe. Kabla ya abiria kupambana na watekaji na ndege hiyo kuanguka, makamu wa Rais, Dick Cheney alitoa amri ya ndege hiyo kutunguliwa kabla haijafika Washington, inaeleza ripoti ya Septemba 11. Hata hivyo, ripoti inaongeza kuwa waliopewa kazi ya kuitungua walikuwa na uwezekano mdogo wa kufanya hivyo kwa muda muafaka. Mamlaka za jeshi zilisema kuwa kama si abiria kusababisha United 93 kuanguka, wangehakikisha haifiki Washington, jambo ambalo baadaye walikiri kuwa haukuwa uamuzi sahihi.
Baada ya balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania kulipuliwa Agosti 7, 1998, Rais Bill Clinton aliamuru jeshi la Marekani kumuua Osama kabla ya Septemba 11 ambapo shirika la kijasusi la CIA pamoja na mashirika mengine yaliandaa mipango kadhaa ya kumkamata Osama mwaka 1998, ilisema ripoti hiyo.
Hata hivyo, mipango hiyo ilikufa na kufufuka mara kadhaa kwa kuwa walitegemea zaidi msaada kutoka kwa viongozi wa jadi wa Afghanistan.
Mshauri wa masuala ya ulinzi wa Marekani, Sandy Berger alijaribu kuibua mjadala kwamba ingekuaje kama ungekosekana ushahidi wa kumtia hatiani Osama katika mahakama ya Marekani kabla ya kufanyika kwa mashambulizi ya makombora dhidi ya Osama katika makazi yake huko Afghanistan na kuuawa mwaka 2011.
CIA walimuonya Rais Clinton mara kadhaa kuhusu utwekaji wa ndege tangu mwaka 1998. Desemba 4, mwaka 1998 ilitolewa taarifa kwa Rais kuwa Osama ameandaa mpango wa kuteka nyara ndege za Marekani na mashambulizi ili kushinikiza kuachiwa kwa Yousef na magaidi wengine. Inaeleza ripoti ya Septemba 11.
Shambulizi lilihusishwa na Saudi Arabia, ripoti ya Septemba ilieleza kuna baadhi ya kurasa zaidi ya 28 ambazo hazijawekwa wazi zinafichua kwamba kulikuwa na viashiria uhusika au kuwapo mkono wa Saudi Arabia katika shambulizi hilo. Kurasa hizo zinaonyesha kwamba kulikuwa na ufadhili kutoka kwa mwana wa mfalme wa Saudia, Bandar aliyekuwa balozi nchini Marekani. Taarifa kutoka gazeti la USA Today zilieleza kuwa “Kuna uwezekano wa ufadhili wa kifedha kutoka kwa familia ya kifalme ya Saudia kwa raia wake wanaoishi Marekani wakiwemo watekaji wawili miongoni mwa waliohusika huko San Diego. Taarifa pia zinaonyesha kuwa kulikuwa na ufadhili kwa misikiti ya Waislamu wenye msimamo mkali mjini California.” Hata hivyo kurasa hizo hazijawekwa wazi kwa sababu haikuthibitishwa kuwa taarifa hizo zinahusika moja kwa moja na shambulizi la Septemba 11. Taarifa zinaeleza kuwa watekaji 19 waliohusika na shambulizi hilo walitoka Saudi Arabia.
Kulikuwa na mipango mingine hapo awali ya kushambulia ndege za abiria. Ripoti ya Septemba 11 inaeleza kwamba kulikuwa na misururu ya mipango ya mashambulizi dhidi ya ndege za abiria za Marekani kabla ya Septemba 11, 2001. Mtuhumiwa namba moja wa mipango hiyo, Ramzi Yousef anatajwa kupanga ulipuaji wa makao makuu ya WTO mwaka 1993 na mashambulizi ya ndege 12 za Marekani ukanda wa Pacific mwaka 1995. Yousef alifanya kazi hiyo na mjomba wake aliyeitwa Khalid Sheikh Mohammed ambaye naye alihusika kwa kiasi kikubwa katika shambulizi la Septemba 11. Yousef alikamatwa Februari 7, 1995 huko Islamabad, Pakistan. Alipanga shambulizi lingine Manila, Ufilipino ambalo halikufanikiwa.
Shambulizi la Septemba 11 dhidi ya majengo ya WTO, Mjini New York halikuwa la kwanza. Itakumbukwa mchana wa tarehe Februari 26, mwaka 1993 bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari dogo lilipuka katika maegesho ya magari ya ardhini katika moja ya majengo hayo. Ripoti ya Septemba 11 inaeleza kuwa watu sita waliuawa katika mlipuko huo na wengine zaidi ya 1,000 kujeruhiwa. Ripoti zinasema kwamba Ramzi Yousef ambaye ni muumini wa dhehebu la Sunni ndiye aliyepanga shambulizi hili la kigaidi na alilenga kuua watu 250,000.
Ni miaka takribani 15 imepita tangu kutokea kwa shambulizi la New York. Tukio hili lilifufua upya vita vikali dhidi ya ugaidi ambapo kila nchi duniani kwa sasa inapambana kuhakikisha hakuna kitisho dhidi ya ugaidi.
Baraza la Umoja wa Mataifa linapambana na makundi haya ambayo yanazidi kukua kila siku. Makundi kama Islamic State, Boko Haram, Al-Shabaab na mengine ni miongoni mwa makundi yanayosumbua usalama wa raia katika nchi mbalimbali. Ni wajibu wa kila nchi kuimarisha idara zake za usalama kuhakikisha ya Septemba 11 au zaidi hayajirudii.


elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

Endelea kusoma makala hizi zifuatazo;

a.gif Mambo Ya Kuzingatia Kuongeza Utagaji Wa Kuku

Inafahamika kuku kutaga mayai mengi hutokana na aina ya mbegu ya kuku, ila jua kwamba hata aina ya mbegu ya kuku yenye sifa ya kutaga mayai mengi kama haitapewa matunzo mazuri  basi sifa yake ya utagaji itapotea.
Kwa kawaida Tetea anatumia muda wa masaa 24 - 27 (siku moja) kutengeneza yai. Hakuna njia ya kupunguza muda huu (yaani atengeneze mayai miwili katika siku moja). Hiyo ndio asili yake. Njia Nzuri ya kumfanya kuku atage muda mrefu ni kumfanya awe na furaha na afya.
Njia za kuwafanya kuku wawe na furaha na afya:.. soma zaidi

a.gif Mambo ya Msingi kuyajua Ili uishi na watu vizuri

Nimezipenda hizi nasaha. Naamini na nyinyi wenzangu hamtakosa japo machache ya kujifunza:-
1. Epuka hasira za ovyo na kila mtu, kuwa msikivu kabla ya kukimbilia maamuzi (elewa kuwa ukiwa na hasira huwezi kupata suluhu ya jambo)
2. Usiwatendee wengine ubaya ukadhani kuwa utakuwa salama (ubaya hulipwa kwa ubaya, ipo siku ubaya wako kwa wengine utakurejea kama sio kuwarejea watu wa kizazi chako).. soma zaidi

a.gif Ushauri wa ukweli Ili Uwe mwanaume wa Ukweli

1. Ukija kijiweni au pub au kwenye nyama choma acha zile stori za sijui umesoma wapi hadi wapi, sijui una madigirii mangapi. Piga stori nyingine, mbona ziko nyingi tu. Kujielezea sana shule yako ni ushamba fulani hivi, dizaini kama hujiamini so lazima ujivishe nyota. Unaboa… soma zaidi

[Kitendawili Kwako] 👉Fimbo yangu nzuri iliotea kwenye miiba

uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png

a.gif Kwa nini watu wasio na ualbino wanaogopa kuoa Albino kwa imani kuwa watawazalia watoto Albino?

Ualbino ni hali ya
kurithi, hii inamaanisha
kuwa unapata ualbino
kutoka kwa wazazi
wako. Watu wawili
weusi wanaweza kupata
Albino endapo kila
mmoja wao atakuwa
na kinasaba cha ualbino.
Hali hii huwezi kuiona
au kuijua. Unaweza tu
kuitambua baada ya
kujifungua. Takribani
mtu mmoja katika watu
70 ana kinasaba cha
ualbino lakini si rahisi
kujua ni nani anacho.
Endapo Albino ataoa
mwanamke mweusi,
uwezekano wa kuzaa
Albino ni mdogo sana.
Albino wengi waliooa au
kuolewa na watu weusi
wamepata watoto
ambao ni weusi… soma zaidi

a.gif Dalili na matibabu ya tatizo la upungufu wa damu

Upungufu wa damu ni tatizo linalosababishwa na kupoteza damu nyingi, kupungua kwa uzalishaji wa chembe hai za da damu na uharibifu wa chembe za damu kutokana na matatizo na magonjwa mbali mbali seli mundu, ujauzito, hedhi nzito, kurithi, magonjwa sugu na Lishe duni yenye ukosefu wa madini ya folic, chuma na vitamini B12… soma zaidi

a.gif Je, kuna vipimo ambavyo vinaweza kugundua hali ya kuwepo kwa ualbino wakati kichanga kikiwa bado tumboni?

Hakuna kipimo rahisi cha kuwezesha kuonyesha kama mama
mjamzito amebeba kinasaba cha ualbino. Lakini uwezekano upo,
kama wazazi watakuwa wamepata mtoto Albino. Uwezekano wa
kujua kama mimba inayofuatia kichanga kitakuwa na ualbino kwa
kutumia kipimo maalamu kinachovuta maji yaliyo kwenye mji wa
mimba na kupima hayo majimaji kuona kama kuna kinasaba cha
Albino. Hata hivyo, vipimo hivi ni vya gharama kubwa na kwa
kiasi kikubwa kwa sasa vinapatikana, katika hospitali kubwa
maalumu za nchi zilizoendelea (Ulaya, Marekani na kadhalika)… soma zaidi

a.gif Nifanyeje kujiepusha na vishawishi vya mpenzi wangu vinavyoweza kunifanya nisitumie kondomu?

Mara nyingine siyo rahisi kujiepusha na vishawishi vya kujamiiana bila kutumia kondomu kutokana na msukumo wa mpenzi wako. Lakini kumbuka kwamba siyo rahisi kumtambua mwenye magonjwa ya zinaa na mara nyingi huwezi kujua kama mpenzi wako hana ugonjwa wowote wa zinaa au hata virusi vya UKIMWI.
Huwezi kufahamu ni watu wangapi ameshajamiiana nao maishani mwake na mpenzi wako vilevile hawezi kufahamu kama wewe umeshajamiiana na mtu mwingine. Kila unapojamiiana kuna uwezekano wa kuambukizwa magonjwa ya zinaa. Kwa hiyo jadiliana na mpenzi wako na mkubaliane juu ya umuhimu wa kutumia kondomu wakati wa kujamiiana kwa nia ya kuwakinga wote wawili. Kama mpenzi wako anakuambia kwamba hana ugonjwa kama huo, mwambie kwamba hana uhakika wa kufahamu kutokuwa na virusi vya UKIMWI bila kupimwa damu. Na kama mmoja kati yenu hajapimwa, basi uwezekano wa kuwa na virusi upo. Usikubali kushawishiwa kutotumia kondomu, kwa sababu inaweza kuhatarisha maisha yako.
Matumizi ya kondomu inazuia ujauzito ambao wewe bado hauko tayari kuwa nao.. soma zaidi

a.gif Jinsi ya kutunza udongo

Uelewa wa maisha ya mimea husaidia kwa kiasi kikubwa kwa hatua ya kuchukua kuilisha mimea hiyo… soma zaidi

[Msemo wa Leo] 👉Uwezo wa Kutumia ulichonacho

[Jarida la Bure] 👉Kijitabu cha Kilimo Bora cha Bamia

[Hadithi Nzuri] 👉Kisa kilichombadilisha mume tabia

[SMS kwa Umpendaye] 👉SMS kwa mpenzi anayeishi mbali

elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

.

afya-mapishi-na-lishe.png
rafiki.gif
elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.