Tafuta

Marafiki zako mliopotezana wanakutafuta Wanakungoja kwa hamu sana uwatafute na wao

👉SOMA ZAIDI HAPA...

👉 Tanzania: Serikali imewaagiza wataaalam wanaosimamia kituo cha kuzalisha umeme cha MTERA kuhakikisha maji hayakauki👇✔

picha-tatu1.jpg Serikali imewaagiza wataaalam wanaosimamia kituo cha kuzalisha umeme cha MTERA kuhakikisha maji katika bwawa hilo hayakauki wakati wote hasa kipindi cha kiangazi ili kuzalisha umeme wakati wote.

Agizo hilo limetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,Mhandisi OMAR CHAMBO wakati wa ziara ya kukagua shughuli zinazoendelea katika kituo hicho.

picha-nane.jpg
Tayari wadau wanaohusika na masuala ya Mazingira, Maji, Maliasili pamoja na Ardhi wameweka mkakati wa kuokoa uharibifu wa mazingira katika vyanzo vya maji yanayoingia katika bwawa hili.

Kituo cha MTERA kina uwezo wa kuzalisha megawati 80 za umeme ambazo zinaingizwa kwenye gridi ya Taifa kilisimamisha uzalishaji wa umeme tangu mwezi Oktoba mwaka huu kutokana na kukauka maji katika bwawa hilo.

🙉🙉🙉Usisahau kushare posti hii kuhusu (Tanzania: Serikali imewaagiza wataaalam wanaosimamia kituo cha kuzalisha umeme cha MTERA kuhakikisha maji hayakauki).👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome💯✔

utotoni.gif

.