Salamu za mwaka mpya

By, Melkisedeck Shine.

familia-mapenzi-na-mahusiano.png

Salamu za mwaka mpya

Wanandoa wapya waliooana muda si mrefu,
waliishi maisha ya kimasikini sana.Siku moja
mume akamuita mke wake akamwambia''mke
wangu naondoka naenda safari ya mbali,kwenda
kutafuta mali ili tuje tuishi maisha ya furaha na
raha ila sijui nikiondoka nitakaa huko miaka
mingapi.Nakuomba mke wangu uwe mwaminifu
usinisaliti na mimi pia huko niendako nitakuwa
mwaminifu sitakusaliti''.

Mke alikubali na mume
akaondoka akaanza kutembea.Alitembea kwa siku
nyingi sana hatimaye akafika kwa mkulima
mmoja aliyekuwa anatafuta mtu wa kumsaidia
kufanya kazi katika shamba lake.Yule kijana
akaomba kazi akapata ila akamwambia yule
mkulima''nitafanya kazi ila mshahara wangu
utakuwa unanitunzia mpaka siku nikitaka
kuondoka nitakuambia unipe hizo pesa zangu
zote nilizofanya kazi kwako.Yule mkulima
akakubali ombi la yule kijana.Kijana akafanya ile
kazi kwa miaka ishirini,na siku moja akamwambia
boss wake kwamba ataondoka hivyo ampe pesa
zake zote.Yule mkulima akasema sawa ila
nitakupa mambo mawili uchague moja.Mkulima
akasema 1.nikupe pesa zako zote uondoke au
2.nikupe ushauri wa aina tatu afu nisikupe pesa
zako zote ulizofanya kazi kwangu kwa kipindi
chote cha miaka ishirini.Lakini sitaki unipe jibu
sasa hivi katafakari afu kesho utanipa jibu
umechagua kipi.Yule Jamaa akakaa
akatafakari,kesho yake akaja na jibu.Boss
akauliza unataka kipi?Yule jamaa akasema nipe
huo ushauri wa aina tatu.Boss akarudia tena
''nikikupa huo ushauri ujue sitakupa pesa zako
ulizofanya kazi kwangu.Yule jamaa akasema
sawa ww nipe huo ushauri.Yule Boss mkulima
akasema
i.usifanye mambo kimkato na usipende njia za
mkato.
ii.usipende kudadisidadisi na kushangashangaa
mambo yasiyokuhusu mana kuna mambo
mengine ni mabaya ukiyadadisi na kuyashangaa
sana yatakupelekea kifo.
iii.usifanye maamuzi wakati unahasira au
unauchungu.
Baada ya hayo yule Boss akamwambia haya
kijana wangu unaweza kuondoka,shika hii mikate
mitatu hii miwili utakula wewe mwenyewe ukiwa
njiani kurudi nyumbani na huu mmoja utakula na
mke wako siku ukifika nyumbani.Jamaa
akachukua ile mikate akaanza safari.Mara
akakutana na mzee mmoja akamwambia''kijana
umepitia hii njia?hii njia ni ndefu sana unaweza
kumaliza mwezi hujafika hivyo pitia hii njia ya
mkato utafika haraka.Jamaa akakubali akaanza
kutembea kupitia ile njia ya mkato,mara
akakumbuka ushauri wa kwanza
aliopewa.Akaamua kurudi tena kwenye njia ya
awali ile ndefu Baadae akaja kugundua ile njia ya
mkato ilikuwa na waasi waliokuwa wanaua yeyote
na kumteka akipitia hiyo njia.Akatembea kwa
muda mrefu akachoka
akaona nyumba ya wageni akalipia pesa akaoga
afu akalala.Usiku akasikia makelele sana
akaamka ili akaangalie kuna nini,wakati anataka
kufungua mlango akakumbuka ushauri wa
pili,jamaa akarudi akalala zake.Asubuhi mwenye
gest akamuuliza vipi hukusikia makelele usiku?
Jamaa akasema alisikia ila sikutaka kufatilia sana
yasiyonihusu.Mwenye nyumba akasema wewe ni
mtu wa pekee kutoka salama mana hapa huwa
kuna mtu anatoka usiku anapiga kelele na yeyote
anayetoka nje kushangaa na kutaka kujua nini
kinaendelea huwa anauawa na yule mtu na
kuzikwa kwenye uwanja ule.Jamaa akaendelea na
safari na baada ya safari ya siku nyingi usiku na
mchana akafika nyumbani kwake kwake usiku na
mke wake alikuwa amelala.Alipochungulia kwenye
ufa akaona kuna mtu mwingine wa kiume amelala
pembeni.Jamaa alipatwa na hasira na ghadhabu
akataka aingie awaue mke wake pamoja na yule
mwanaume mwingine aliyekuwepo ndani afu yeye
arudi akafanye kazi kwa boss wake.Lakini kabla
hajafanya hivyo akakumbuka ushauri wa tatu
akaamua kwanza.Akagonga mlango mke wake
akafungua,mke alifurahi sana akamkumbatia
mume wake.Lakini mke alimsukuma yule
mwanamke na kumwambia''kwanini
umenisaliti?''mke akasema sijakusaliti mume
wangu toka uondoke.Jamaa akasema vipi na yule
mwanaume ndani ni nani?.Mke akasema huyo ni
mtoto wako ulipoondoka nilikuja kugundua kuwa
nina ujauzito ndio nikamzaa huyu mtoto.Wote
walifurahi sana na baadae mke akaandaa chai
ndipo mume akauchukua ule mkate wa tatu
aliopewa na boss.Baada ya sara aliumega mara
akakuta kitita cha pesa nyingi sana,zilizidi hata
zile alizostahili kulipwa baada ya kufanya kazi
miaka ishirini.MUNGU WETU YUKO KAMA HUYU
BOSS,WAKATI MWINGINE ANAPOTAKA KUJITOA
SADAKA,ANATAKA ATUPE VITU ZAIDI YA VILE
TUNAVYOJITOA,ANATAKA TUWE NA HEKIMA ZA
KIMUNGU PAMOJA NA BARAKA ZA
MWILINI.MUNGU ANATUWAZIA MEMA SIKU
ZOTE. ……mwaka ni mpya hata ningekuwa na milion nikawapeni mfurahie siku ya leo isingetosha lakini kwa hekima kubwa nafikiri malengo mema ya mbele ili sote tufurahie bila kuchoka….By primo


Endelea kusoma makala hizi zifuatazo;

a.gif Salamu za kuaga mwaka na kukaribisha mwaka mpya

KWAHERI MWAKA JANA. UMENIFUNZA MENGI… soma zaidi

a.gif Salamu za kiinjilisti kwa wadada

~Yaanike matiti yako kwenye mitandao wee, yabane vizuri na vaa vinguo vya ajabu ili yaonekane…
~Jaa kiburi wanavyokusifia wanaume wazinzi kuwa wewe ni mzuri na umependeza…
~Vaa visiketi vyako vya kubana na kuacha vimapaja vyako nje wanaume wasio na huruma wakusifie kisha wakulaghai na kuzini na wewe…
~Zitoe mimba hizo wanazokupa endelea na huo mchezo mpaka pale utakapoona kuua sio maagizo ya Mungu na wakati huo umeshaua kizazi… soma zaidi

a.gif Ujumbe kwa Mke Mtarajiwa

Mke wangu mtarajiwa, najua uko sehemu
salamanukivuta muda na jamaa mwingine kabla
hatujaoana. Lakini kabla sijakuweka ndani Ninayo
machache ya kukueleza….. soma zaidi

a.gif Mambo ya kufanya ili kupona majeraha mapema

Hakuna mtu anayependa kupata majeraha au kuchelewa kupona majeraha. Kwa kuwa uhai na uzima wetu haupo mikononi mwetu, ni vyema tukafahamu kuwa kuna wakati tunaweza kuumia… soma zaidi

a.gif Jinsi ya kutibu chunusi kwa Siki ya tufaa

Siki ya tufaa (Apple cider vinegar) ni moja kati ya dawa zinazojulikana katika kutibu chunusi ahsante kwa uwezo wake wa kurudishia tindikali katika ngozi. Bakteria wabaya, mafuta na uchafu mwingine wowote utaondoka juu ya ngozi yako bila kupenda ukitumia dawa hii… soma zaidi

a.gif Faida ya kunywa maji yenye limao au ndimu kila siku

Watalam mbalimbali wa afya wanasema ya kwamba kwa kila siku ni vyema unywe maji ya ndimu ili uweze kujitibu magonjwa yafuatayo;.. soma zaidi

a.gif Mapishi ya chipsi

Viazi (potato) 1/2 kilo
Mafuta ya kukaangia (veg oil)
Chumvi.. soma zaidi

a.gif Mapishi ya Ugali na dagaa

Dagaa (dried anchovies packet 1)
Unga wa ugali (corn meal flour 1/4 kilo) (unaweza kutumia unga wa choice uipendayo)
Nyanya ya kopo (tin tomato 1/2)
Kitunguu maji (onion 1)
Limao (lemon 1/4)
Pilipili mbuzi nzima bila kukata (scotch bonnet pepper1, do not chop)
Chumvi (salt 1/4 ya kijiko cha chai)
Mafuta (vegetable oil)
Hoho (green pepper).. soma zaidi

elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

.

afya-mapishi-na-lishe.png
MLO-MWEMA-KWA-NDUGU-UJUMBE.JPG
picha-kali.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.