Rais wa Gambia Yahya Jammeh ametangaza taifa hilo lenye Waislamu wengi kuwa jamhuri ya Kiislamu

Rais wa Gambia Yahya Jammeh ametangaza taifa hilo lenye Waislamu wengi kuwa jamhuri ya Kiislamu

Rais wa Gambia Yahya Jammeh ametangaza taifa hilo lenye Waislamu wengi kuwa jamhuri ya Kiislamu

Yahya-Jammeh_2468947b.jpg Bw Jammeh ameimbia runinga ya taifa kwamba tangazo lake linaambatana na sifa na maadili ya kidini ya Gambia. hii ni kutokana na kuwa na waislamu wengi ambapo asilimia 90 ya raia wa Gambia ni Waislamu.

Amesema kuwa raia na wageni wa dini nyingine hawatalazimishwa kuvalia mavazi ya Kiislamu, na wataruhusiwa kuendelea na dini zao bila kusumbuliwa.

President-of-the-Republic-of-The-Gambia-Yahya-Jammeh-and-QFs-Deputy-Director-of-Communication-Mr-Rashed-Al-Qurese-300x198.jpg Koloni hiyo ya zamani ya Uingereza hutegemea sana utalii. Uhusiano kati ya taifa hilo na nchi za Magharibi umekuwa ukidorora siku za karibuni. Kwa mfano muungano wa Ulaya ulikatiza kwa muda pesa za msaada kwa Gambia mwaka jana kutokana na rekodi mbaya ya haki za kibinadamu.Jammeh_21.jpg
Bw Jammeh ameongoza taifa hilo ndogo la Afrika Magharibi kwa miaka 21.
Mataifa mengine yanayojitambulisha kama jamhuri za Kiislamu ni Iran na Pakistan, na barani Afrika kuna Mauritania.
Bw Jammeh aliondoa Gambia kutoka kwa Jumuiya ya Madola 2013 akitaja muungano humo kuwa wa ukoloni mamboleo.

Usisahau kushare posti hii!! Share Facebook, Twitter bila kusahau Whatsapp!!

Toa maoni yako kuhusu, Rais wa Gambia Yahya Jammeh ametangaza taifa hilo lenye Waislamu wengi kuwa jamhuri ya Kiislamu. hapa..

Add a New Comment
or Sign in as Wikidot user
(will not be published)
- +

Kwa sasa endelea kusoma posti hizi zifuatazo;