Nguvu iliyofichika | Hidden power

By, Melkisedeck Shine.

Mwaka 1836 binti mmoja aliyekuwa na umri wa miaka 18 kutoka familia ya kitajiri huko Lexington, Kentucky alimuomba Mungu aolewe na Rais wa Marekani. Licha ya kwamba utajiri wa familia yao ulitokana na biashara ya utumwa lakini wazazi wake waliamua kuachana na biashara hiyo mwanzoni mwa miaka ya 1800's na kuwa wacha Mungu.

Mary alikuwa muumini wa makanisa ya uamsho kwa wakati huo (Presbyterianism), kama ilivyo makanisa ya kiroho leo. Siku moja akamwabia baba yake, "Mungu ameniambia kuwa mwanaume wa maisha yangu atakuwa Rais wa nchi hii".

Baba yake akastaajabu, lakini hakutaka kumkatisha tamaa. Akamwambia "binti yangu, nchi hii ni kubwa sana, na wasichana wengi wangependa kuolewa na watu mashuhuri na wenye madaraka, lakini si jambo rahisi kuolewa na Rais. Na ukisubiri hali hiyo kutokea unaweza usiolewe kabisa katika maisha yako".

Lakini yule msichana akamtizama baba yake kisha akamjibu "sijali ni wasichana wangapi wanaotamani kuolewa na watu mashuhuri, sijali nchi hii ni kubwa kiasi gani. Ninachojali ni kuwa Mungu ameniambia kuwa siku moja nitakuwa first lady wa nchi hii. Hilo tu"

Maka mmoja baadae (1837) yule binti akachumbiwa na mwanasiasa machachari chipukizi aliyekuwa mwanasheria na mbunge wa Illinois (the rising young lawyer and Democratic Party politician) aitwaye Stephen Douglas. Kwa kuwa Stephen alikuwa mbunge, baba wa yule binti aliamini kuwa huyo ndiye angemuoa mwanae na angekuja kuwa Rais wa Marekani baadae. Kwahiyo ndoto za binti yake zingetimia kupitia Stephen.

Lakini mwaka miaka miwili baadae (1839) uchumba wao ukavunjika.

Mwaka huohuo (1839) katika mji wa Springfield, Illinois, yule binti akakutana na kijana mmoja msomi wa sheria lakini kutoka familia maskini huko Indiana. Kijana huyu alikuwa amekuja Illinois kutafuta kazi. Wazazi wake walikua wakulima maskini. Ardhi yao huko Kentucky ilitaifishwa na hivyo wakahamia Indiana.

Kijana huyu akapendana na yule binti na kuamua kuoana. Mwaka 1840 mwezi December kijana akamvisha pete ya uchumba yule binti. Baba wa binti hakufurahishwa. Akajiuliza iweje mwanae amkatae "mbunge" na akubali kuolewa na "mtoto wa mkulima??". Kwa masikitiko akamuuliza binti yake "unakumbuka ahadi ya Mungu wako kwako?". Binti akajibu "hata sasa bado naamini."

Miaka minne baadae (1843) wakafunga ndoa.

Miaka 17 baadae (1861) yule kijana akachaguliwa kuwa Rais wa 16 wa Marekani. Jina lake aliitwa Abraham Lincoln, na mkewe aliitwa Mary Todd Lincoln.

Mary ndiye aliyekataa kuolewa na Steven Douglas (Mbunge) kwa ajili ya Lincoln (mtoto wa mkulima).

Baba yake Marry akiwa mzee wa zaidi ya miaka 80 alishuhudia mwanae akiwa "First Lady" akamwambia "Mungu wako ni mkuu sana. Aliahidi na ametimiza". Mwaka mmoja baadae (1862) mzee Robert Todd (baba yake Mary) akafariki.

MORAL OF YHE STORY.!
Hadithi hii ni ya kweli kabisa inayomhusu Rais Abraham Lincoln na mkewe Mary Todd Lincoln. Kuna mengi ya kujifunza kwenye kisa hiki, lakini ningependa kukushirikisha machache niliyojifunza mimi.

#Lesson_1: Ukiomba usichoke kusubiri. Mungu akisema atakupa, basi amini atakupa tu. Mungu wetu ni mwaminifu na hutupa kwa wakati wake. Mary aliona maono ya kuwa first lady akiwa na miaka 18, lakini ilimchukua robo karne (miaka 25) hadi maono yake kutimia. Sasa wewe ndugu yangu umemaliza chuo mwaka jana umeomba kazi hata mwaka haujaisha umeshaanza kumlalamikia Mungu. Subiri. Au umeomba mchumba mwaka wa 3 hujapata, unaanza kumlalamikia Mungu eti wenzio wote wameolewa/kuoa. Tafadhali subiri. Mungu atakupa kwa wakati wake unaofaa.

#Lesson_2: Ishi katika misimamo. Baba yake Mary Todd alipoona mwanae amemuacha "Mbunge" akaolewa na Mtoto wa mkulima alimuona kama vile amepoteza dira. Lakini binti alijua ipo siku Mungu atatenda. Na Mungu alivyo mwaminifu hakumruhusu baba yake Mary kufa kabla hajashuhudia Mwanae akiwa "first lady" wa Marekani. Point hapa ni kwamba jifunze kushikilia imani yako na uwe na msimamo usioyumba hata kama dunia nzima itakuacha. Wengi waliobarikiwa ni wenye misimamo. Jifunze kuwa focused and visionary. Usitazame vinavyong'ara leo, tazama vitakavyong'ara milele.

#Lesson_3: kuna kitu kinaitwa "Hidden Power" yani nguvu iliyofichwa. Ni nguvu ambayo unakuwa nayo wewe lakini inatokana na watu wengine. Unaweza kufanikiwa sana, lakini si kwa juhudi zako bali kwa sababu nyuma yako kuna watu wanaofanya wewe ufanikiwe. Wanakuombea, wanafunga kwa ajili yako, wanamsihi Mungu kwa ajili yako, wanaomba ulinzi, baraka, na neema kwako. Wanaweza kuwa wazazi wako, mwenzi wako, watoto wako, rafiki zako, ndugu zako etc.

Lincoln alikuwa na nguvu iliyofichwa kupitia mkewe. Yani mke wa Lincoln (Mary) ndiye aliyemfanya mumewe kuwa Rais. Kama Lincoln asingemuoa Mary Todd asingekuwa Rais wa Marekani. Na hata Lincoln mwenyewe aliwahi kukiri kwamba "Urais haukuwahi kuwa ndoto zake katika maisha"

#Lesson_4: Our GOD is the GOD of imposibilities. Yale tunayoona na kudhani hayawezekani, kwa Mungu yanawezekana. Wakati Mary akiwaza atakuwa first lady wa Marekani, Lincoln hakuwahi kuwaza kama angekaa awe Rais. Sijui kama unauona ugumu huu.! Imagine Mungu anakuahidi utakua "first lady", halafu anakataa usichumbiwe na Mbunge. Anakupa mchumba mwingine, halafu huyo mchumba anakwambia "sina hata ndoto za Urais". Ingekua ni wewe ungejisikiaje? Wengine mngemlaumu Mungu na kutamani kurudi kwa mbunge, right? Lakini Mungu akiahidi ni lazima atimize.

#Lesson_5: Mungu huinua vyenye nguvu katikati ya vinyonge. Unakumbuka hadithi ya Daudi? Yesse alipoambiwa aite watoto wake wote maana mmoja wao atakua Mfalme, aliita wote akamsahau Daudi. Imagine baba yako mzazi anakusahau. Lakini Mungu akamfanya huyohuyo mdogo, mnyonge, aliyesahaulika kuwa Mfalme. Lincoln nae pengine alionekana mnyonge, lakini Mungu akasema "huyu ndiye"

Katika maisha usimdharau mtu yoyote. Heshimu kila mmoja. Unayemdharau leo aweza kuinuliwa kesho ukabaki unashangaa. Ipo nguvu iliyofichwa (the hidden power) kwa kila mmoja wetu. Unaweza usiione nguvu hiyo leo lakini ipo siku itafanya kazi.

The hidden power.!!!

[kitendawili Kwako] ๐Ÿ‘‰Dume wa baba anangurumia malishoni

[chemsha_bongo Kwako] ๐Ÿ‘‰Ni namba gani inayofuata hapa chini mwisho?

Endelea kusoma makala hizi zifuatazo;

a.gif Ndoa sio utani. Soma stori hii

"Mkeo amefariki. Rudi nyumbani kwako haraka sana" Hezron alimwambia Daniel katika simu… soma zaidi

a.gif FUNZO: Maisha ni kuchagua

Siku hizi kuna tangazo moja la kampuni ya simu za mikononi, Tigo, likimuonesha mama akiwa _busy_ na pembeni yupo mwanae mdogo apo akijisemesha na akatamka maneno ambapo mama akaona ni kama ameanza kuongea. Kwa furaha anampigia simu mumewe akimtaka amsikilize mwanae akiongea. Hapo mama anamtaka mwanae aseme "mama" na baba naye anavutia kwake akimtaka aseme "baba". Kwa maajabu kabisa mtoto anawapotezea wote na kutamka "ni Tigo peesa". Wazazi wakashikwa na butwaa lakini huku wakitabasamu… soma zaidi

a.gif Ushauri kuhusu mwanamke wa kufaa kuoa

Nawaandikia ninyi vijana wa kiume na wanaume wote, maana mna nguvu na mmejaliwa na mwenyezi Mungu utashi, hekima na busara. Yote hayo ni ili muweze kutawala kila kitu tokea kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu huu. Wekeni wivu pembeni na Yafuateni haya;.. soma zaidi

UJUMBE-POLE-NDUGU.JPG

a.gif Je, ni kweli kwamba uvutaji wa bangi hukufanya uwe na nguvu?

Si kweli kabisa! Baada ya kuvuta bangi mtu hujiona kama jasiri sana na mwenye nguvu. Lakini madhara ya bangi ni kinyume na matarajio ya mtumiaji kwani mishipa husinyaa na ubongo hushindwa kufanya kazi zake vyema na kutoa uamuzi usio sahihi wa utendaji sahihi wa kazi za mwili… soma zaidi

a.gif Jinsi ya kuanzisha mradi wa mbuzi wa maziwa

Watu wengi hutemea mifugo kwa riziki.Ufugaji wa wanyama humpa mkulima nyama na maziwa kwa matumizi ya nyumbani na mapato kutokana na mauzo ya ziada. Mifugo pia ni chanzo cha samadi. Bidhaa zingine za wanyama zinazoweza kuuzwa ili kupata pesa zinajumulisha ngozi,samadi ya kuongeza rutuba kwenye ardhi ya kupanda mimea na pia kutoa kawi ya biogas, pembe, kwato na midomo ya ndege… soma zaidi

a.gif Ni vizuri kujua haya

๐Ÿ‘‰๐ŸฟDegree au vyeti ulivyo navyo haviwezi kukupa mafanikio.
๐Ÿ‘‰๐ŸฟUzuri ulio nao hauwezi kukupeleka kwenye ndoto zako.
๐Ÿ‘‰๐ŸฟUsipobadilisha hao marafiki ulio nao hutofika mahali popote… soma zaidi

a.gif SHAIRI: Kama mnataka mali, mtaipata shambani.

1. Karudi baba mmoja,
toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja,
na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja,
ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli iwafae maishani… soma zaidi

a.gif Madhara ya kuangalia picha za ngono

Kuna watu wanapenda sana kuangalia sinema za ngono… soma zaidi

Usipitwe na Nafasi za kazi kwa leo

<<Bofya HAPA kujua zaidi>>

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.