Mama Kaenda kupumzika Mimi Nimebaki kukulinda

By, Melkisedeck Shine.

Juzi nilihudhuria msiba wa rafiki yangu mmoja na mkewe. Yeye na mkewe walifariki kwa ajali ya gari, wameacha watoto wawili mmoja wa miaka kumi na mwingine wa miaka minne wakike, mkubwa ni wakiume.

Sasa tukiwa kwenye ule msiba, mimi kama rafiki nilikua karibu sana na wale watoto kwani wananifahamu kama Baba mdogo, kusema kweli nilichokishuhuduia kilinifanya nije nimpende mke wangu mara mia zaidi.

Kweli nampenda sana mke wangu lakini kuna wakati namchukuliaga poa nikiwa na mambo yangu najifanya kidume na namuudhi. Kwasiku tatu zote nilikua karibu na ile familia tukimalizia msiba, katika kipindi chote hicho watoto walikua wakimlilia Mama yao.

Yaani wakilala wakiamka ni kuniuliza, wananiita anko, Mama yuko wapi (Mara nyingi wnaaniita anko), wanmauuliza Bibi yao Mama yuko wapi. Sasa kilichonifanya nilie nipale ambapo mtoto mkubwa wa miaka kumi ambaye anaelewa kitu kidogo alikua anampembeleza mdogo wake alikua anamuambia.

“Usilie Mama kaenda sehemu nzuri, kaenda kupumzika kwa Mungu na Malaika…” Mdogo wake ndipo alipouliza Baba nayeye, akasema “Amemsindikiza Mama watakaa huko na mimi ndiyo nitakulinda, usiogope nipo hapa. Unakumbuka siku ile Mama alivyotuambia twende kwa Bibi kukaa wenyewe…”

Alimuuliza… “Mimi si nilikulinda…nitakulinda na sasa…Mama anatuangalia lakini sisi hatumuoni….” Kama hapo umelia basi subiri majibu ya yule mdogo wake. Huku akijaribu kujizuia kulia alimuuliza Kaka yake.

“Sasa kama Baba ameenda na Mama si atampiga tena, mimi sitaki Mama apigwe, kwanini asingeenda peke yake….” Nilianza kuwaza namna ambavyo rafiki yangu yule alikua akimnyanyasa mkewe, namna alivyokua akimpiga na kumsimanga, nilishaongea naye mara nyingi lakini hakujali.

Lakini alikua anawapenda watoto wake na kila siku aliwadekeza ila hawakumkumbuka. Jibu la kijana wake ndiyo lilinifanya niamini kuwa wanadamu si chochote. “Huko hawezi kumpiga, Mama ameenda kwa Mungu, huyo ana nguvu zaidi kuliko Baba. Akimsogelea tu atamchanachana kamakaratasi! Mungu ana upendo hapigi watu wema kama Mama!”

Hapo yule mtoto alikua akiongea kwa uchungu lakini kwa hasira na kwa imani kabisa. Sikuweza kuendelea kuvumilia kuwasikiliza, niliwaacha na kwenda kumuangalia mke wangu, nilimkumbatia na kumuuliza “Mke wangu hivi na mimi nakunyanyasa?”

Aliniangalia kwa mshanagao, aliniulzia kwanini unasema hivyo, nilimuambia hapana niambie tu. Niambie kama kuna kitu nakifanya kinakukwaza ambacho watoto wangu watakiona. Nilimuambia “Nataka wanangu waniulizie nikifa, sitaki wanangu wafurahie kifo changu.”

Mke wangu alinikumbatia huku akitokwa na machozi aliniambia “Hakuna mume wangu, wewe ni mume bora, sema uache tu kuweka soksi kwenye makochi na kuacha sahani kitandani.” Nilijikuta natabasmau kidogo, kwani mke wangu alikua na furaha.

Sasa hivi najifunza nisiache soksi kwenye makochi wala sahani kitandani. Najua alikua anatania ila kama kinamkera nitaacha, maisha hapa duniani ni mafupi, watoto ndiyo kitu tunaacha kwaajili ya kututambulisha, sitaki wnaangu wanaitambue kama Baba mkatili.

Watumie wengine kuwakumbusha wanaume wenye tabia za kuwanyanyasa wake zao kuwa hawana nguvu kuliko MUNGU na ipo siku watafika huko.

[kitendawili Kwako] 👉'Jejere jeje'

Endelea kusoma makala hizi zifuatazo;

a.gif Wachaga Na Tofauti Zao

Warombo wajanja sana kibiashara/wezi pia.wameajiri wamarangu mjini ni walevi sana hupeleka wake zao vijijini wakileta kiburi mjini… soma zaidi

a.gif Matumizi ya mihogo kama dawa ya kuzuia wadudu kwenye mimea

Muhogo Inazuia Minyoo na vidukari… soma zaidi

a.gif Jinsi ya kutumia mashonanguo kama dawa ya kuzuia wadudu kwenye mimea

MASHONANGUO.jpg

Mashonanguo kwa kiingereza ni Blackjack au kwa kisayansi yanajulikana kama (Bidens
pilosa)
Mashona nguo yanazuia wadudukama vile Vidukari, Siafu, bungo, katapila, chenene (crickets), nyenyere, siafu na inzi weupe… soma zaidi

Ndugu.gif

a.gif Watu wafanye nini iwapo wamelazimishwa kufunga ndoa na mtu wasiyemtaka?

Iwapo mtu amelazimishwa
kuingia katika hali ya ndoa
(kuoa/kuolewa) na msichana/
mvulana ambaye hampendi,
hatua ya kwanza ni kukataa
ndoa hiyo na kuonyesha wazi
wazi. Jadiliana suala hili na
wazazi wako. Waeleze kwa
heshima kwa nini hukubaliani
na ndoa hiyo… soma zaidi

a.gif Mapishi ya Mihogo ya nazi na kuku

Mihogo kilo 1
Kidali cha kuku 1 kikubwa
Nyanya 1 kubwa
Kitunguu maji 1 cha wastani
Swaum/tangawizi i kijiko cha chai
Nazi kopo 1
curry powder 1 kijiko cha chai
Binzari manjano 1/2 kijiko cha chai
Limao 1/2
Pilipili 1
Chumvi kiasi.. soma zaidi

a.gif Mapishi ya Wali maharage,mchuzi wa samaki na spinach

Mchele (rice 1/2 kilo)
Maharage yaliyochemshwa (boiled red kidney beans 1 kikombe cha chai)
Samaki waliokaangwa ( 2 fried fish)
Nyanya ya kopo (tin tomato 1/2 ya tin)
Vitunguu vilivyokatwa (onion 2)
Kitunguu swaum (garlic 3 cloves)
Tangawizi (ginger kiasi)
Limao (lemon 1/2)
Chumvi (salt)
Pilipili (scotch bonnet pepper 2)
Mafuta (vegetable oil)
Spinach
Tui la nazi (coconut milk 1 kikombe cha chai).. soma zaidi

a.gif Njia za kutibu shinikizo la chini la damu au presha ya kushuka

Nyia hizo ni kama ifuatavyo;.. soma zaidi

a.gif Kisa kilichombadilisha mume tabia

Mume alirejea nyumbani na kukuta ujumbe juu ya meza umeandikwa "NIMEONDOKA" ilikuwa jioni, alienda jikoni na kukuta kukavu, aliwaita watoto na kuwauliza wakasema walimuona Mama akiondoka na begi lakini hakuwaambia anaenda wapi. Mume alichanganyikiwa, alijaribu kuchukua simu kumpigia lakini ilikuwa haipatikani, kabla hajafanya chochote mtoto wao wa mwaka mmoja alikuja akilia na kusema ana njaaa… soma zaidi

Usipitwe na Nafasi za kazi kwa leo

<<Bofya HAPA kujua zaidi>>

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.